Arusha: Mrisho Gambo awapatia msaada wa vyakula Wajane 160 kwa ajili ya sikukuu ya Eid-el-Fitr

jembejembe

JF-Expert Member
Jun 9, 2016
667
1,000
Kina mama wajane wapatao 160 kutoka kata nne za jiji la Arusha wamepatiwa msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Iddy.

Msaada huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo baada ya kutambua uhitaji wa kina mama hao ambao wengi wao wanaumri mkubwa na hawanauwezo wa kumudu sherehe hiyo.

Wakiongea Mara baada ya kupokea msaada huo ambao ni pamoja na Mafuta ya kula ,sukari, unga wa ngano ,Mchele ,wamemshukuru mbunge huyo wakidai kwamba hawakuwahi kupokea msaada wa aina hiyo tangu enzi za baba wa Taifa mwalimu Julias Nyerere.

Mmoja ya wanawake hao,Vicky John kutoka kata ya Olasiti alisema wanamshukuru Mbunge huyo kwa msaada huu utakaowafanya washerehekee vizuri Kama watu wengine wenye uwezo wa kipato.

"Tunamshukuru Sana Mbunge kwa moyo wake wa kizalendo kwa msaada huu ambao umekuja wakati mwafaka,kwakweli hatuna shaka tena na sikuukuu ya Idd kwani tayari tumepata kianzio"alisema.

Mjane mwingine kutoka kata ya Olmoti Selina Thobias alisema kwamba hawakutegemea kupata msaada huo kwani umewakumbushaenzi za Mwl. Julias Nyerere wakati wakigawiwa misaada Kama hiyo.

Baadhi ya madiwani waliohusika kuratibu akina mama hao wajane kutoka kata za Olmoti, Sombetini, Simon na Olasiti wameeleza kufurahishwa na mpango wa mbunge huyo kuwakumbuka akina mama wajane hasa kipindi hiki cha sikuukuu.

Diwani wa kata ya Olasiti,Alex Martin alisema kuwa msaada huo utawasaidi Sana kina mama hao kufurahia sherehe hiyo ya Idd kwani wengi wao hawana uwezo wa kipato.

Naye naibu meya wa jiji la Arusha Veronica Hosea amemshukuru Mrisho Gambo kwa msaada huo ambao umegusa mioyo ya wahitaji ambao hawajui tumaini la kesho nankuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia makundi ya aina hiuo ikiwemo watoto yatima.

Kwa upande wake Mrisho Gambo alisema ameamua kutoa kidogo kwa wananchi wake ikiwa ni mchango wake kwa makundi yenye uhitaji Kama wajane na watoto yatima ili washerehekee Sikukuu ya IDD kwa Amani .

Ends....

IMG_20210512_145729_490.jpg
IMG_20210512_143840_638.jpg
IMG_20210512_143740_060.jpg
 
Faana

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
17,687
2,000
Udhalilishaji tu, kwani angewapa bila kuwapiga picha angepungukiwa nini? Maandiko yasema utoapo kwa mkono wa kuume hata mkono wa kushoto usijue.
 
the kind

JF-Expert Member
Nov 6, 2019
378
500
Umefanya vizuri kutoa sadaka.
Sadaka ya eid el fitr hutolewa
Kina mama wajane wapatao 160 kutoka kata nne za jiji la Arusha wamepatiwa msaada wa vyakula mbalimbali kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Iddy.

Msaada huo umetolewa na Mbunge wa jimbo la Arusha mjini Mrisho Gambo baada ya kutambua uhitaji wa kina mama hao ambao wengi wao wanaumri mkubwa na hawanauwezo wa kumudu sherehe hiyo.

Wakiongea Mara baada ya kupokea msaada huo ambao ni pamoja na Mafuta ya kula ,sukari, unga wa ngano ,Mchele ,wamemshukuru mbunge huyo wakidai kwamba hawakuwahi kupokea msaada wa aina hiyo tangu enzi za baba wa Taifa mwalimu Julias Nyerere.

Mmoja ya wanawake hao,Vicky John kutoka kata ya Olasiti alisema wanamshukuru Mbunge huyo kwa msaada huu utakaowafanya washerehekee vizuri Kama watu wengine wenye uwezo wa kipato.

"Tunamshukuru Sana Mbunge kwa moyo wake wa kizalendo kwa msaada huu ambao umekuja wakati mwafaka,kwakweli hatuna shaka tena na sikuukuu ya Idd kwani tayari tumepata kianzio"alisema.

Mjane mwingine kutoka kata ya Olmoti Selina Thobias alisema kwamba hawakutegemea kupata msaada huo kwani umewakumbushaenzi za Mwl. Julias Nyerere wakati wakigawiwa misaada Kama hiyo.

Baadhi ya madiwani waliohusika kuratibu akina mama hao wajane kutoka kata za Olmoti, Sombetini, Simon na Olasiti wameeleza kufurahishwa na mpango wa mbunge huyo kuwakumbuka akina mama wajane hasa kipindi hiki cha sikuukuu.

Diwani wa kata ya Olasiti,Alex Martin alisema kuwa msaada huo utawasaidi Sana kina mama hao kufurahia sherehe hiyo ya Idd kwani wengi wao hawana uwezo wa kipato.

Naye naibu meya wa jiji la Arusha Veronica Hosea amemshukuru Mrisho Gambo kwa msaada huo ambao umegusa mioyo ya wahitaji ambao hawajui tumaini la kesho nankuwataka wadau wengine kujitokeza kusaidia makundi ya aina hiuo ikiwemo watoto yatima.

Kwa upande wake Mrisho Gambo alisema ameamua kutoa kidogo kwa wananchi wake ikiwa ni mchango wake kwa makundi yenye uhitaji Kama wajane na watoto yatima ili washerehekee Sikukuu ya IDD kwa Amani .

Ends....

MWENYEZIMUNGU (SW) analipa NIA,yaani kisudio la kufanya jambo lako

Kama nia yake ni kuwaanika masikini hao na kupata popularity basi itaitikia vizuri sana na kama alitoa kama sadaka ya eid el fitr ambayo kimsingi hutolewa siku chache kabla ya sikukuu ya eid el fitr angalau siku 1 au 2 kabla ya eid au kabla ya kuswali eid hapo naona ukakasi

Na kama ametoa sadaka ya kawaida ALLAH atamlipa kwa nia yake hiyo

Ila wanasiasa wanafurahisha sana😜😜😜
 
legend Babushka

JF-Expert Member
Jun 29, 2015
520
1,000
Wakiongea Mara baada ya kupokea msaada huo ambao ni pamoja na Mafuta ya kula ,sukari, unga wa ngano ,Mchele ,wamemshukuru mbunge huyo wakidai kwamba hawakuwahi kupokea msaada wa aina hiyo tangu enzi za baba wa Taifa mwalimu Julias Nyerere.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom