Hawa ‘Wakimbizi walioteuliwa kwenye nafasi za maamuzi’ ni kina nani?

Kwa mujibu wa mkuu wa majeshi Gen Jacob John Mkunda amemueleza Rais kuwa Kuna wakimbizi wapo Hadi Serikalini na wamepewa nafsi za juu kabisa za kimaamuzi

Hili inashangza na kufikirisha Sana inakuwaje Hadi mkuu wa majeshi anawajua wakimbizi na wameteuliwa na wala hajawasiliana na mamlaka za uteuzi kuzuia uteuzi wao yeye amekaa kimya Hadi leo ndio Kuja kumueleza Rais by suprise.

Mimi najiuliza hivi Rais leo atapata usingizi Kweli? Atakuwa anajiuliza ni Nani huyu nimemteua ambae Ni mkimbizi?

Lazima Rais atapitia mafail yake kwa upya mnk kwa taarifa ya leo wa kamanda wake CDF kusema wasiwasi kuwa unawateua hadi wakimbizi inamaana kwamba wasaidizi wake wanamuingiza Chaka.

Anyway Kama Kuna kiongozi au afsa tunamuhisi siyo mtanzania mwenzetu Basi tumtaje hapa hajui kuwa siyo mwenzetu.

- Mtikila: Kagame amepenyeza Wanyarwanda 35,000 Tanzania, Burigi, katika Wilaya ya Muleba

Pitieni huu uzi
Haya mambo ya uraia yanafikirisha sana.

Kwanza watu hawataki kujifunza historia ya kweli.

Pili historia ya kweli inapotoshwa na hata inayojulikana haizingatiwi sababu ya wivu na chuki dhidi ya watu wengine.

Kuhusu historia ya kweli mambo mawili ya kuzingatia. Kabla ya 1884 na 1885, hii nchi inayotufanya tugombanie umiliki wake, ilikuwa inaitwaje? Watu wake ni watu gani? Kiongozi wao ni yupi? Mamlaka ya kiutawala yalikuwa yapi? Ardhi na maji yao yalikuwa yapi? Je, wageni waliingia na kutoka kwa utaratibu gani?

Nini ilikuwa tofauti ya masai, mchaga, mpare, msambaa, mdigo anayekaa kaskazini mwa Tanganyika ya 1885 na mtu wa jamii hiyo anayeishi kusini mwa Kenya ya 1885?

Nini ilikuwa tofauti ya mkazi wa kusini mwa Tanganyika ya 1885 na mkazi wa kaskazini mwa Msumbiji, Zambia na Malawi za 1885?

Nini tofauti ya wakazi wa mwambao wa ziwa Tanganyika la 1885 katika mikoa ya magharibi kama Rukwa, Katavi na Kigoma lakini pia wakazi wa Kagera na wakazi wa nchi zilizoitwa Uganda, Rwanda, Burundi, DRC na Malawi vyote vya 1885?

Lakini tukija wakazi wa kaskazini magharibi mwa Tanganyika ya 1884, nini tofauti ya makabila ya kijita, kijaluo na wakurya wa Tanganyika ya 1885 na wale wa upande wa Kenya ya 1885? Tofauti za watu hao ni nini hasa kwa kuzingatia ugawaji wa Africa wa 1884/85? Kabla ya kulazimishwa mipaka, waliitwaje? Walibaguana?

Hoja ya pili ni mwenyeji wa nchi ya Tanganyika ni nani? Historia iko wazi, wabantu wote wametokea west Africa wakashuka kati ya Africa kwa makundi yao na wengine kusini na makundi yao hadi wakaifikia ardhi ya inayoitwa Tanganyika ya 1885.

Lakini pia wapo wasio wabantu kama Nilotics waliofuata mto nile mfano wajaluo na Hamitics. Yapo makabila asili yao ni Sudan, Ethiopia na jamii nyingine za kimasai, kisandawe n.k ambao walikotokea kunajulikana kupitia historia.

Wangoni ambao ni wabantu na vitabu wameandika kabisa kuwa wameingia nchi hii kutokea kusini mwa Africa na wote tumesoma historia yao ya Nguni Migration

Jamii nyingi zimeingia ardhi hii zikitokea maeneo mengine. Sasa huyo mnayetaka awe mtanganyika kwa mgao wa 1885 ni yupi?

Maswali ya kujiuliza.

1. Tanganyika ina mipaka mingi na watu wa mipakani wanapatana kwa vitu vingi. Kwa nini mipaka ya magharibi mwa Tanganyika ndio wahanga wa huu ubaguzi wakati mipaka mingine ikiwa shwari bila chokochoko? Watu wengi wameumizwa sababu ya chuki hizi.

2. Wenye historia zilizoandikwa hasa wangoni kwa nini wao nchini wanakubalika ma hawabugudhiwi sawa na watu wa magharibi? Je makabila yote ya kusini, mbona hawabaguliwi wakati nao asili zao zinajulikana?

Inafikirisha sana
 
Hoja yangu kwenye hili, tunapoimarisha Jumuiya ya Africa mashariki, haya mambo yakomeshwe. Free movement of goods, service and people ziachiwe. Kenya sasa ni Visa free Nation. Nchi wanachama zijifunze kwa Kenya, ziandikishe kwa wingi passport ili watu wayasake maisha popote yalipo. Huu usingizi tulionao ndio umetufanya tuishi kipuuzipuuzi tu na maendeleo yako chini sababu tunawaza kuitana ukimbizi, tunalima kwa ajili ya chakula, kila jambo tunalifanya chini ya kiwango. Turuhusu fikra zivhangamke
 
Back
Top Bottom