Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni nani aliyeingiza udini kwenye kampeni hizi?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Nyambala, Oct 6, 2010.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  M. M. Mwanakijiji ​

  SIJUI kama mwenzangu umegundua kuwa siku za karibuni wanasiasa wetu na watawala wetu walioshindwa wameanza kulalamika kuwa kuna udini unaingizwa katika kampeni hizi huku baadhi yao wakidai kuwa kuna watu wanawashawishi watu kupiga kura kwa misingi ya dini.Ukiwasikiliza vile unaweza kuamini kabisa kuwa hawajui jinsi gani suala la udini limeingia kwenye kampeni na sasa wameshtuka kuwa linaweza kuwagharimu uchaguzi, kuzaa vurugu na hata kusababisha machafuko nchini. Lakini mtu mwenye hekima hana budi kujiuliza tulifikaje mahali ambapo dini inaonekana kuwa sehemu ya kampeni hii?

  Labda nitumie fursa hii kukumbushia tu matukio kadhaa ambayo yatatudokeza kwanini kuna hisia za kuingizwa kwa mambo ya kidini katika kampeni hizi. Sote tunafahamu kuwa Dk. Slaa kwa muda wa miaka kumi na mitano amekuwa ni mbunge wa Jimbo la Karatu na ni jambo linalojulikana kuwa aliingia katika siasa akitoka kuwa padri wa Kanisa Katoliki akiwa ameshika nafasi mbalimbali kuanzia jimboni kwake hadi makao makuu ya Baraza la Maaskofu Katoliki pale Kurasini.

  Alipotaka kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM kule Karatu, CCM ilimuengua kwa kumpendekeza mtu mwingine na Dk. Slaa akaamua kuhamia CHADEMA wakati huo kikiwa bado ni chama kichanga kabisa. Kuingia kwake CHADEMA kulidhaniwa kutakuwa ni mwisho wake kisiasa na wananchi wa Karatu baada ya uchaguzi mmoja tu wangemtema na kurudisha CCM. Miaka kumi na tano imepita na Dk. Slaa amekuwa ni mbunge wa Karatu huku chama chake kikishika na Halmashauri ya Karatu mojawapo ya halmashauri chache ambazo zimeshikiliwa na upinzani.

  Katika kipindi chote hicho cha miaka kumi na mitano suala la kuwa Dk. Slaa alikuwa ni padre halijawahi kuwa jambo la kuwakwaza watu. Aliposimama kuwanyoshea vidole mafisadi bungeni alimtaja miongoni mwao mtu ambaye alikuwa ni Mkristu, Gavana David Balali.

  Suala la kuwa aliwahi kuwa Padri halikuwa suala kubwa. Na aliposimama pale Mwembe Yanga alitaja majina ya watu mbalimbali kuwatuhumu vitendo vya ufisadi. Hakukuwa na mtu yeyote aliyesimama na kusema ‘imekuwaje mbunge aliyewahi kuwa padri kufanya jambo hili"?

  Ukweli ulibakia ni kuwa Watanzania hawakujali dini ya Dk. Slaa wala hali yake ya upadre. Watanzania walitamani na hatimaye walipata mwanasiasa mwenye ujasiri wa kuita embe embe, chungwa chungwa, na kitunguu kitunguu!

  Hadi pale chama chake kilipompendekeza kuwa mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muuangano wa Tanzania. Hapo ndipo tulipoona wabaguzi wa kidini wakianza kujitokeza na kufanya suala la upadri wa Dk. Slaa kuwa hoja.

  Kwanza walianza kuhoji ana "udaktari" wa kitu gani? Wakaanza kubeza kuwa udaktari wake ni wa "Elimu ya Kanisa" na hivyo siyo elimu hasa na wengine wakajenga hata hoja kuwa labda hastahili kuitwa daktari. Licha ya maelezo ambayo yalitolewa wakati ule na kuwapa watu elimu kuwa shahada ya uzamivu aliyonayo inatoka kwenye chuo kinachotambulika na siyo ya kununua kama ya kina fulani bado wengine hawakuridhika.

  Wakatoka kwenye hoja hiyo wakaongeza kuwa Dk. Slaa bado ni padri wa Kikatoliki na magazeti yenye mrengo wa kifisadi yakaandika kwa mmbwembwe na kuwatisha baadhi ya wananchi kuwa Dk. Slaa atakuwa ni mtumishi wa Baraza la Maaskofu. Licha ya maelezo ya utaratibu unaotumika kwa padri kuacha upadri bado wenye hisia za udini wakaendeleza hoja hiyo.

  Lengo lao walikuwa wanataka kuonesha kuwa mtu aliyewahi kuwa padri hastahili kuwa Rais wa Muungano. Lakini kwa kufanya hivyo wakaenda mbele zaidi kwani wakaanzisha ile hisia dhidi ya "ukatoliki" wa mtu ambayo imekuwepo kwenye baadhi ya watu.

  Suala hili la udini liliwahi kutumika katika historia ya Wamarekani pale Seneta John F. Kennedy alipotaka kugombea urais wa taifa hilo kubwa wakati wa kilele cha vita baridi. Ilimlazimu Seneta Kennedy kutetea ukatoliki na kutofautisha na nafasi yake ya urais aliyokuwa anagombea.

  Katika chakula cha jioni kwenye mji mmoja huko Marekani Seneta Kennedy aliwaondoa hofu Wamarekani kwa kuwaambia kuwa "mimi siyo mgombea Mkatoliki wa nafasi ya urais wa Marekani, bali ni mgombea wa nafasi ya urais wa Marekani ambaye pia ni Mkatoliki".

  Waliokuwa na hofu hasa Waprotestant ambao ni wengi katika Marekani waliondolewa hofu hiyo na Kennedy akachaguliwa kuwa Rais wa 35 wa Marekani. Na hadi leo amebakia kuwa ni miongoni mwa marais waliopendwa sana Marekani.

  Kumbe suala la dini ya mtu halipaswi kuwa sehemu kabisa ya mjadala wa siasa za kidemokrasia. Vigezo vya msingi vilivyoainishwa na Katiba yetu ndivyo pekee vinatakiwa kuzingatiwa wakati wa kufikiria nani awe rais wetu. Na ni kutokana na uelewa potofu wa makada wa CCM na mashabiki walioeneza siasa hizo za udini CCM ikajikuta imetegwa ikategeka.

  Wakaanza kuzungumzia "kama alikosa uaminifu katika upadre ataweza vipi kuwa mwaminifu kwa taifa". Hawakujua wanauliza nini; hawakujua wanapandikiza mbegu za chuki za kidini, utengano na hisia ya shuku. Lakini kilichonikera mimi zaidi ni kuwa katika muda wote huo hakuna kiongozi yeyote wa juu wa CCM na serikali yake aliyejitokeza kukemea tabia hiyo ya makada wao.

  Hakuna aliyesimama na kusema kuwa suala la upadri wa Dk. Slaa siyo hoja na suala la imani yake halihusu wananchi. Mpaka pale wachache wetu tulipojenga hoja za kuonesha upuuzi wa hoja za kibaguzi zilizopandikizwa.

  Lakini juhudi zetu zilikuwa zimechelewa. Tayari madhara yalikuwa yameshafanyika; walioamini kuwa Dk. Slaa ni kibaraka wa Wakatoliki wakaendelea kuamini hivyo na hao hadi sasa wamekwazika kwa Dk. Slaa kugombea urais.

  Wale ambao tayari wameaminishwa kuwa Wakristu ndio maadui zao basi wakaona ndani ya Dk. Slaa mtu ambaye atawakilisha maslahi ya Wakristu. Na jambo baya zaidi lililotokea ni kuwa Dk. Slaa anagombea dhidi ya mgombea wa CCM ambaye ni Muislamu. Hisia zikaanza kujengeka kuwa kuonesha mapungufu ya serikali ya Rais Kikwete au kuhoji maamuzi yake ilikuwa ni sawa na kumshambulia kwa sababu ni "Mwislamu".

  Matokeo yake kimetokea kitu gani? Baadhi ya Wakristu wakaanza kuona kuwa Dk. Slaa hatendewi haki na anashambuliwa kwa sababu ya Ukatoliki wake na hasa pale tuhuma zilikuwa zikiongozwa na viongozi wa CCM ambao pia ni Waislamu (Makamba na Kinana) na Waislamu nao wakaona kuwa Kikwete anashambuliwa kwa sababu ni Mwislamu na hasa baada ya kauli ya viongozi wa Kikristu kama Mch. Kakobe.

  Na kwa kadiri siku zinavyoendelea kila kundi linazidi kwenda mbali ya jingine na kugawa mashabiki wao vivyo hivyo. Hata hivyo ukweli ni kuwa fikra za namna hii zinatokana na ujinga yaani, kutokujua. Hata hivyo uzuri wa ujinga ni kuwa huweza kuondolewa kwa kuelimishwa.

  Ndugu zangu, anayedhani kuwa Wakristu wa Tanzania watahama sijui waende sayari ya Zebaki anajidanganya na yule anayedhani kuwa Waislamu wa Tanzania watahamia Zuhura nao wanajidanganya.
  Ni wapuuzi wale wote wanaofikiria kuwa nchi hii itakuja kumegwa kwa ajili ya vikundi mbalimbali kuridhishwa. Ni taifa letu sote. Ni taifa la Wandengereko na Wazinza kama lilivyo taifa la Wambulu na Wabarbaig; ni taifa la Wamwera na Wagweno kama lilivyo taifa la Wasafwa na Wamatengo!

  Ni taifa la Wahindi na Waarabu kama lilivyo leo hii taifa la Washirazi na Wakomoro. Historia imetufunga pamoja milele kiasi kwamba wanaodhani kuwa tunaweza kutenganishwa kwa sababu za dini na ukabila wanajidanganya na sala yao hata shetani hawezi kuitekeleza!

  Hakuna mwenye haki zaidi katika taifa hili au mwenye kustahili zaidi. Hakuna mtu ambaye ati kwa vile babu yake alipigania uhuru basi yeye anastahili zaidi!

  Ni katika kutambua ukweli huu ndipo wale wachache ambao tunajitambua kuwa ni Watanzania kwanza tunasimama na kuyabeza makundi yote mawili. Tanzania itatawaliwa na Watanzania wote. Lakini katika kutambua hili hatutaogopana ati kwa sababu fulani ni Mkristu au Mwislamu mwenzetu basi hatutamkemea.

  Lakini vile vile hatutaogopana ati kwa sababu mtu ni tofauti na sisi katika dini au kabila, basi tutamkandamiza. Yote ni ya hatari kwa mustakabali wa taifa. Binafsi napenda kuona viongozi wa Kikristu wakimkemea Mkapa na kutaka awajibike kwa yale aliyoyafanya na kuliomba taifa pasipo kumuonea haya na ningependa viongozi wa Kiislamu wakimkemea Kikwete pasipo kupepesa macho. Na ni matarajio yangu kuwa endapo Dk. Slaa atashinda Wakristu wa Tanzania hawatajaribu kummezea pale akianza kuleta yale yale tuliyoyakataa chini ya Kikwete na Mkapa.

  Ni lazima tuwe na ujasiri wa kuweka Tanzania mbele kuliko dini zetu, makabila yetu na vyama vyetu. Ni kutokana na ukweli huo naamini mkorogano wa sasa umeletwa na CCM na ni CCM wenyewe wausafishe.
  Kwanza ni lazima wakiri kuwa Dk. Slaa ana haki ya kugombea kama Rais wa Muungano licha ya kwamba aliwahi kuwa padri na kuwa suala la yeye kuwa padri si kikwazo wala sababu ya kutokuchaguliwa.

  Pili, CCM iache mara moja hizi siasa zenye kudokeza ubaguzi wa kidini au kikabila ambazo imezifanya miaka kadhaa huko nyuma (tunakumbuka walivyosakama CHADEMA kuwa ni chama cha kikabila).

  Endapo CCM haitasahihisha makosa yake yenyewe katika kupandikiza mbegu za chuki za kidini kupitia makada wake kama alivyofanya kiongozi wao wa Umoja wa Vijana Benno Malisa huko Geita mwishoni mwa juma basi wajue kuwa baadhi ya Watanzania wataona kuwa njia pekee ya kujibu mashambulizi hayo ni wao wenyewe vile vile kuendeleza siasa za kidini.

  Hii itakuwa ni hatari kwa taifa na Watanzania wote ni lazima tusimame katika ulinzi kuwakataa wana CCM wenye kupandikiza mbegu za chuki za kidini kwa kisingizio chochote na wakati huo huo kuwakana wapinzania ambao watasimama na kutoa mashambulizi ambayo yana misingi ya kidini dhidi ya CCM.

  Ni katika kufanya hivyo tu ndipo tutajikuta tunalipa taifa letu nafasi ya kuendelea kwani katika hili sote hatima yetu ni moja; nchi moja, hatima moja!

  Natamani nione viongozi wetu wa kisiasa na kidini wakiandaa maandamano ya umoja wa kitaifa yenye kushinikiza umoja wetu zaidi na siyo tofauti zetu mbalimbali. Ni kwa kufanya hivyo tu watawala na viongozi wenye hisia za ubaguzi wataumbuliwa na ajenda zao za utengano kufichuliwa.

   
 2. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  Mwanakijiji

  Huu udini unaelekea kuwarudi waliokuwa wanauendekeza. Wiki iliyopita jopo la viongozi wa dini zote kubwa nchini, walianza matembezi ya kuongea na wagombea urais. Tumeshangaa jana kuona kundi la mashehe wanakuja tena mbele ya vyombo vya habari kutoa tamko lao peke yao. Tunajiuliza ikiwa katika matembezi ya kuwaona wagombea wanakuwa wote, inakuwaje sasa wanakuja na tamko la peke yao?

  Mbaya zaidi, katika umoja wao wa madhehebu yote, walisema mambo binafsi ya wogombea yasipate nafasi katika mijadala. Jana Mufti Simba akasema, yawe na nafasi. Je alimaanisha tuanze kazi ya kupima DNA za watoto wa mitaani?

  Naomba niseme kwa sauti, kuwa tamko la mashehe lina agenda ya siri na ndiyo maana walishindwa hata kutamka hata jina la mtu mmoja wanayemtuhumu kuwa anaelekeza watu kupiga kura kwa misingi ya udini.
   
 3. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Naamini matatizo haya ya mambo ya udini kama ilivyo tuhuma za Ukabila husababishwa na CCM halafu ndio wanakuwa wa kwanza kuruka na kushangaa katika dizaini za "hatujui"
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mashehe: Msichague kwa misingi ya dini

  Imeandikwa na Gloria Tesha; Tarehe: 6th October 2010

  Source: Habari leo  Habari Zaidi:

  Habari zinazosomwa zaidi:

  JOPO la mashehe wa Kiislamu nchini likiongozwa na Mufti Issa Shaaban bin Simba limewataka Watanzania watakaopiga kura mwaka huu kuchagua kiongozi kwa misingi ya sera na si dini.

  Aidha, wamewaonya baadhi ya viongozi wa dini wanaotumia nafasi zao kuhamasisha waumini wao kuchagua kiongozi kwa misingi ya dini, kuacha kwani si jambo jema na linapingana na malengo ya waasisi wa Taifa hili.

  Akisoma tamko lao kwa waandishi wa habari Dar es Salaam jana, katika ofisi za makao makuu ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata), Shehe Simba alisema hivi sasa kuna vuguvugu la kisiasa lenye mwelekeo wa kushawishi fikra za wananchi, kuchagua kiongozi kwa misingi ya dini.

  "Hivi karibuni, utamaduni wa kuchagua viongozi wenye sifa na sera zinazokubalika, umebadilika kwa sura ya wazi kabisa, kwa kujitokeza baadhi ya viongozi wa dini kutumia majukwaa ya kidini kuhimiza waumini wachague wafuasi wa dini zao," alisema Mufti katika mkutano huo ulioshirikisha mashehe wa taasisi zote za kiislamu zilizosajiliwa nchini.

  Mufti Simba aliyezungumza akiwa msemaji wa jopo hilo, alisema jambo hilo linaashiria kuigawa nchi na kuiingiza katika matatizo makubwa, na aliwataka viongozi wa dini kurejea utamaduni wa kuhamasisha waumini kuchagua viongozi wanaofaa kwa sifa zao na sera za vyama vyao.

  Katika hatua nyingine, jopo hilo katika tamko lake, lilikemea baadhi ya vyombo vya habari kwa lilichodai ni kupotosha kauli za viongozi wa dini na kusomeka namna isiyofaa.

  Alitolea mfano wa gazeti moja la kila siku lililoandika habari kuhusu mashehe na maaskofu kumtakasa mmoja wa wagombea, ambapo alikanusha na kukemea habari hiyo, akisema imewadhalilisha, kwa kuwa katika imani ya kiislamu, hakuna mwenye uwezo wa kutakasa mtu kwa dhambi zake, bali Mungu pekee.

  Katika tamko hilo, mashehe waliwataka waumini wa dini yoyote na wananchi kwa jumla, wakatae kupotoshwa na mtu yeyote awe wa dini au siasa katika suala linalohusu uchaguzi, ili kuimarisha amani nchini.
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Iko wapi dhambi ya Askofu Kakobe?

  Imeandikwa na Shadrack Sagati;

  Source: Habari leo

  KABLA hajaanza somo lake la Mkristo na Uchaguzi, Askofu Zacharia Kakobe alihadharisha kuwa licha ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kuwaomba viongozi wa dini kutoa elimu ya uraia kwa waumini wao, lakini pale maneno ya viongozi hao yasipowafurahisha ‘wakubwa', hushutumiwa kuwa amechanganya dini na siasa.

  Jumapili ambayo Askofu Kakobe alitoa somo hilo maalumu, nilikuwa mmoja wa watu walioalikwa kutokana na nafasi yangu ya uanahabari.

  Nadhani uongozi wa Kanisa la Full Gospel Bible Fellowship, uliwaalika wanahabari kwa madhumuni ya kupeleka ujumbe wa kiongozi wao kwa umma wa Watanzania, ambao wanajiandaa kumchagua Rais, wabunge na madiwani Oktoba 31.

  Tangu Askofu Kakobe atoe somo hilo, yamezuka maneno mengi yakiwamo ya kumshutumu kupiga kampeni kwa kisingizio cha kutoa elimu ya uraia.

  Miongoni mwa waliomshutumu ni Msajili wa Vyama vya Siasa, John Tendwa, kuwa ni mtu hatari ambaye anaweza kuvuruga amani ya nchi kwa uamuzi wake wa kutoa elimu ya uraia.

  Tamko la hivi karibuni la vyombo vya ulinzi na usalama, licha ya kutomtaja Askofu Kakobe, lakini pia ilionekana ni mmoja wa watu walioshutumiwa kuwa wanatoa kauli za hatari kwa kisingizio cha kutoa elimu ya uraia.

  Ninachojiuliza; Askofu Kakobe alikurupuka kutoa elimu ya uraia au ni kweli viongozi hao wa kidini wameagizwa na NEC!

  Mbona NEC kama haikuwatuma kutoa elimu ya uraia haijatoa taarifa ya kumkana Askofu Kakobe! Kukaa kimya kwa Mamlaka hiyo, ina maana kuwa ni kweli imewaagiza viongozi hao kutoa elimu ya uraia.

  Kama ni kweli, kosa la Askofu Kakobe liko wapi? Mimi si mfuasi wa Askofu Kakobe kiimani!

  Lakini kwa hili namtetea kiongozi huyo, kwani siku hiyo alitumia muda mwingi kuwaelimisha waumini wake faida za kwenda kupiga kura na kuhudhuria mikutano ya kampeni, ili kupata ujumbe wa wagombea, ilimradi waepuke alichodai ni siasa nyepesi nyepesi, zinazotolewa na baadhi ya wagombea.

  Lakini pia alieleza sababu ya mtu kutopiga kura. Kiongozi huyo pia alieleza vikwazo vinavyochangia Wakristo na wananchi wengine wasipige kura.

  Kikwazo cha kwanza Wakristo kuacha kwenda kupiga kura kwa kuamini kuwa Mungu anawachagulia wanadamu kiongozi wa kuwaongoza.Sababu ya pili ni Wakristo siku ya kupiga kuwa makanisani, hivyo kuacha kwenda kupiga kura.

  Sababu ya tatu aliielekeza kwa wananchi wengine kuamini kuwa kura moja haiwezi kuleta athari, nne ni kudhani kuwa kuna wizi wa kura na sababu ya tano ni kukithiri kwa umasikini, jambo linalowakatisha tamaa wananchi, kuwa hata wakienda kupiga kura hali zao kimaisha haziwezi kubadilika.

  Lakini Kakobe aliwaambia vikwazo hivyo havina nafasi sasa. Pia akawataka waende na wawahi katika vituo na kuhakikisha kuwa wanachagua viongozi wanaowataka.

  Pia akawakumbusha kuwa ili kura zisiharibike, ni vyema mpiga kura akaweka alama moja tu katika karatasi ya kura, ili asiharibu kura yake.

  Lakini kwa kuonesha msisitizo, kiongozi huyo alitangaza makanisa yake kufungwa siku hiyo, ili kutoa fursa ya waumini kwenda kupiga kura.

  Katika elimu hiyo, Askofu akawaambia kuwa mtu anaweza kuchagua mgombea wa chama fulani; lakini kwa kuwa tu hampendi mgombea wa chama kingine, anapiga kura na baadaye anaweka alama katika sura ya mgombea anayemchukia, hivyo kuifanya kura hiyo iharibike.

  Namwuliza Tendwa, kiongozi wa kidini kutoa elimu hiyo, hatari iko wapi? Askofu Kakobe katika kutoa somo hilo, amekosea wapi? Je, ni dhambi kiongozi wa dini kuwasihi waumini wake wajitokeze kwa wingi kupiga kura?

  Nadhani kiongozi huyo angepongezwa kwa hatua yake ya kuthamini siku hiyo ya kupiga kura, hadi anaamua kufunga makanisa na isiwepo ibada yoyote siku hiyo.

  Lakini matokeo yake, amepokea shutuma nyingi kuwa anafanya kampeni na anahatarisha amani. Pia akawaambia waumini hao kwamba wanakwenda kuchagua kiongozi mwenye sifa kikatiba na si kiongozi wa Kanisa au Msikiti.

  Ujumbe kama huo, ndio ambao viongozi wengine wa kidini waliutoa wakati walipofanya ziara katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo
  (Chadema).

  Ujumbe wa viongozi hao hautofautiani na wa Askofu Kakobe, lakini kwa nini shutuma nyingi zimwendee Askofu huyo na si hao viongozi wengine wa kidini kama kusema hivyo ni kuhatarisha amani?

  Je, Tendwa amepata mkanda wa mahubiri ya siku hiyo, ili aweze kumsonda kidole na kumshutumu Askofu Kakobe kuwa anahatarisha amani?

  Kwa nini Askofu Kakobe asipongezwe kwa hatua yake ya kuwaambia waumini wake wachague kiongozi ambaye hakuwapa rushwa na wala wasiogope kwani wanapokwenda kupiga kura, hakuna mtu anayewaona na ni siri yao.

  Je, maneno hayo ndio yaliyomuudhi Tendwa na ndiyo yanahatarisha amani?

  Au kauli ya Askofu Kakobe kuwa kama kuna mtu anaridhika na uongozi wa chama kilichopo madarakani wakichague na kama kuna mwingine haridhiki ana uhuru wa kuchagua mgombea mwingine, je hiyo ndiyo kauli ya kuhatarisha amani?

  Au dhambi ya Kakobe ni kuwataka waumini wake wamchague kiongozi anayeweza kuwaletea maendeleo na mwenye kipaji cha uongozi?

  Kwa hili siogopi kusema Tendwa amemwonea Askofu Kakobe, kwani elimu ya uraia aliyoitoa haina athari yoyote mbaya kwa amani ya nchi.
   
 6. Pengo

  Pengo JF-Expert Member

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 579
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Inaonyesha wewe una bifu na hao mashehe kwani wakati Mokiwa na Kakobe wanatangaza nia ya kumkampenia padre slaa hukuona au kwasababu hawakuvaa ile kofia ya ubwabwa!?

  Kwanza nimeanza kupata wasiwasi na hii dini yetu ya ukristo kwani ninavyoelewa dini imeletwa na aliyetuumba na miongozo yake yote ipo tayari haiitaji kufanyiwa marekebisho sasa hii dini inayofanyiwa marekebisho kila wakati ni dhahiri imetoka kwa shetani na si mungu aliyehai.

  Baba mungu aliye hai tayari ameshaweka muda wa kufanya kazi na kuabudu hata pale aliposema nimeumba dunia na vilivyomo kwa siku sita na siku ya saba(jumapili) nikapumzika,nanyi fanyeni kazi kwa siku zote sita za wiki ila ifikapo jumapili mwende kanisani mkaniabudu mimi tuu.Sasa inashangaza leo wanaibuka mashetani fulani wanaanza kumkosoa mungu kwa kuweka siku ya jumapili ya kuabudu makanisani kwa wao kutoa amri(kumkiuka mungu) kuwa Jumapili ya tarehe 31/10/2010 wakristo tusiende makanisani huo ni upotoshwaji wa hali ya juu na haukubaliki.

  Hivi sasa nasubiri kauli ya askofu mkuu wa KKKT(Dr.Malasusa) nae akiunga mkono utumbo huo basi ni bora nikawa mpagani kuliko kufuata mambo ya akina Kibwetere na baadae kutiwa moto nikiwa hapa duniani.

  Kama kweli watu tunafuata wachungaji wa uongo wa namna hii ni dhahiri hii si dini ya ukweli toka kwa yule aliyetuumba bali ni uzushi toka kwa wafuasi wa shetani kwa kutaka keneemeka hapa duniani kwa maana imeandikwa kuwa kila atangazae injili apate riziki kutokana na injili hiyohiyo sasa hawa viongozi wetu wa dini vipofu watatutumbukiza shimoni,mnukuu bwana Yesu anasema Wachungaji wamepoteza watu wangu,alijua kabisa hawa akina Kobe na wenzie lengo lao ni kutunisha mifuko yao na vitambi vyao bila ya kujali maisha baada ya kufa.

  Najua nitawaudhi wengi na mtakereka wengi lakini ni bora nikasema kuliko kufa na tai shingoni kama mzungu hilo halitowezekana,na wote watakaojibu utumbo basi nao ni wale wale wasiotumia ubongo katika kufikiri ila wanatimia yale yatokayo puani.

  Watu wamekuwa wabaya wanawaza pesa tuu hata kumjua mungu wa kweli hawataki,kutwa kuzungumzia mambo ya siasa ha makanisani hawaendi huo ni ushetani,narudia tena huo ni ushetani na ole wenu siku itapofika,siku ambayo baba hatomjua mwana.Enyi watu rudini kwa mola wenu kwa hakika mola wenu ni mwingi wa msamaha.
   
 7. njiwa

  njiwa JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 11,074
  Likes Received: 1,811
  Trophy Points: 280
  Sikuzote Maamuzi ya waislam yanaonekana UDINI, wakiona Kofia Nyingi mikutano ya CUF .. wanasema chama cha kidini!! anyways UDINI UPO! NA UTAKUWEPO.. ni sawasawa na kusema hakuna ubaguzi wa rangi nchi za magharibi.. while in reality racism ipo,majority ya waislam wenye kuelewa mustkbal wa dini yao katika TZ ya leo! kamwe hawatopiga kura kwa SLAA!!.. Ya kwangu keshaikosa!
   
 8. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  SiJAKUELEWA VIZURI, YAAANI UWE MPAGANI WEWE IMANI YAKO NDOGO SANA! BASI ASKOFU WAKO ANAKAZI KUOKOA ROHO YAKO! MUNGU AKUTIE NGUVU!!
   
 9. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  poleni sana jamani yamefika huko nilidhani tupo kwa manufaa ya nchi!
   
 10. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #10
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Safi Mwanakijiji. Lakini hapo kwenye red umeharibu.
   
 11. g

  guta Senior Member

  #11
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 179
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hi sasa ishaanza kuwa issue, kabla ya askofu Kakobe kuelimisha uma hakuna mtu aliyesema chochote, alipotoa tamko la kusali jumamosi sasa inoekana kana kwamba anataka watu wampigie kura Dr Slaa.

  Ukweli ni kwamba yeye alikuwa akielimisha juu ya upigaji kura nakutaadharisha watu juu ya siasa nyepesi. Nmemsikia na shekhe wa mkoa wa dsm asubuhi katika kipindi cha jambo,akisikitika sana ni kwa nini amefikia hatua ya kubadilisha siku ya ibada!

  Mimi ndhani hawajamuelewa vizuri kakobe, TBC1 wapelekewe mkanda watizame na waseme hapa katika kipande hiki Mtumishi umekiuka. maana sasa ligi naona inataka kuanza na hata mtangazaji Marin akamuuliza - hamuoni kwa kufanya hivi kumjadiri kakobe naye atawajibu na itakuwa kana kwamba kuendeleza malumbano? Akajibu inabidi ajitambue!
   
 12. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #12
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,175
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  Wewe na mama yako ndo mtampa jk kura
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Naposoma hoja zote humu ndani naona UDINI mtupu,... Na hizi ndio athari za viongozi wa dini wanapoingilia Siasa kwani leo kila anayeandika hapa utamjua dini yake kutokana na uchaguzi wa kura yake atampa nani na sababu gani!

  Ifikie wakati mwandishi wa hoja yeyote hapa aonyeshe ukweli kwamba yeye sii mdini kwa kumchagua mtu asiyekuwa dini yake na azungumzie sera za chama na uwezo wa mgombea huyo lakini kama tutazungumzia dini na bado chaguo lako lina influence ya dini yako basi bila shaka wewe ni mdini vile vile.
   
 14. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #14
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  ========

  Mheshimiwa Pengo

  Hivi shetani ni viongozi wa dini wanaohamisha siku ya ibada ili waumini wapige kura, au, shetani ni serikali inayoweka upigaji kura siku ya jumapili ambayo ni siku ya ibada kwa watanzania "walio wachache" sana katika taifa hili?
   
 15. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #15
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Kwani kosa la mwanakijiji ni lipi? Kuchambua chanzo cha chokochoko za kidini ndio kosa. Siku zote tumechukia ubaguzi. Nani asiyejua tulivyoumia mtandao wa kkikwete ulipoanzisha harakati za kibaguzi dhidi ya Salim Ahmed Salim? Mbona wakristu wengi walipiga kelele. Dhambi ya ubaguzi inawatafuna...ni kama kula nyama ya mtu.

  Mnaanza taratibu kudai CHADEMA ni wachagga. Lakini mbona watu tunajiandaa kukipigia kura si wachagga na wala hatuna kadi yao. Mbona na ukristu wetu tulimshabikia sana Lipumba 2000 pamoja na kuwa muislam. Ndg zangu waislam nawaomba sana mfikie mahali muwaone wakristu kama watu. Hivi unajua siri ya Mkapa kupata asilimia ndogo mara zote pamoja na uchakuchuaji wa kura? Nani ampigie kafiri?


  Kwa taarifa yako wale mashehe message waliyopeleka kwa waislam jana (indirectly) ilikuwa ni kuhamasisha dhidi ya ukristu. Muonee huruma mwenzetu anateketea. That is indirect way of delivering the message. Mjinga tu anaweza asielewe hili. Kama Mufti angeandama na watu wa imani nyingine, message ingetofautiana

  Source (knows intent)........transmitter (distortion)......Receiver (division)

  Na ile issue ya mahakama ya kadhi imeishaje (mbona mipango inafanyika nyuma ya pazia?). Nini mmeahidiwa mpaka mkawa kimya. Si bure, tutajionea.

  Mungu ibariki Tanzania, Mungu tuepushe na chokochoko zote za CCM. Amen
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu unaandika madudu gani haya?.. yaani napokusoma nahisi kutapika maanake umejaa Udini hadi kichefuchefu...

  Mtu yeyote anayejumuisha mawazo ya mtu mmoja au wawili na Uislaam au Ukristu basi jua wazi yeye mwenyewe ndiye MDINI..Na kwa nini leo unazungumzia Masheikh hali Kakobe kazungumza vile vile? au Mkapa alopata kura chache kwa sababu ya Waislaam hali akishindana na Mrema ilikuwa Udini vipi?.. Upuuzi mtupu. Mahakama ya Kadhi inakuhusu nini wewe Mgala?

  Wewe chagua Chadema kwa sababu zako iwe Udini, Ukabila au sera zake lakini usitake kuzungumzia Uislaam na CCM kama ni wadini hali robo tatu ya wagombea wa CCM ni Wakristu..Hizi fitna zinaletwa na CUF kwa sababu wanachama wa kuchovya Chadema wamekuwa wakisema kwamba CUF ni chama cha Waislaam, hivyo ujinga mnaofanya nyie wenyewe mnatafuta mchawi nje. Mwisho wa siku haya mambo yatawaponza wote......
   
 17. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #17
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  WACHA UONGO WAKIRISTO GANI WALIMPA LIPUMBA KURA!!!! SI MULISEMA CUF NI CHAMA CHA WAPEMBA NA WAISLAMU NA WANAOHUDHURIA mikutano yao huwa wanavaa kanzu na kofia? sasa unataka waislamu nao wampe kura slaa kwa sababu wakiristo walimpigia kura lipumba mwaka 2000? wacha cheap politics hapa!!!
   
 18. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #18
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Waliosema haya ni ccm au umesahau?
   
 19. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #19
  Oct 6, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Nasema kwa dhati hapa kama nilivyosema kwengine humu.Hadithi nyingi juu dkt Slaa.Makosa ya wagombea wa nchi nyengine musifananishe na kwetu.
  Huyu mbakaji kwa uwezo wa Allah asipate.Hana hekima katika uongozi wake.Akipata uraisi itakuwa ndio mwisho wa Tanzania.Hana uadilifu.Kwanza Allah atasimama kuwatetea waungwana.Waislamu nao watachemka na utakuwa ndio mwisho.
   
 20. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #20
  Oct 6, 2010
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Bwa ha ha ha ... hii ungeitoa somalia kwa al shabash ingeeleweka zaidi
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...