Hawa Waha wanaokopesha vyombo ni wachawi kweli kweli

Kuna mama mmoja hpa kitaa deni lilikuwa kubwa akataka akimbie, ile siku ya kuhama Muha amefika ngoma ikaenda hadi kwa mjumbe ikabidi wagawane vyombo
Sa jamaa alikimbia tena ama aliendelea na maisha yake...?
 
Dah Mleta mada umenikumbusha enzi zangu
... Kumbe nyie ndo Huwa mnatusumbua eeh

Ngoja nikwambie kitu kidogo usiojua, Pamoja na kuwa mim muha lakini sio wote wanatumia uchawi na wakat nafanya hiyo kazi na vijana Wangu wote hatukuwahi tumia uchawi ata punje na Bado unasema na wateja Kama kawa.

Huwa ipo hiv
Mim napo nunua mzigo Huwa najua kabisa katika pisi hizi kumi Nane ndio tapata pesa hizi mbili zinaweza kutana na wezi au matapeli kama nyie
kwahiyo hata ikitokea siwezi toka mchezoni.

Pia iko hivii Huwezi kopesha Sehem moja Kila siku naweza kopesha Vingunguti miezi mitatu Nikahamia Ubungo Kimala nikaenda Mbagala then Nikaludi Vingunguti tena. Sas Kuna ile mtu umemkopeshea Buza akahia Ubungo na Mungu alivyo Mkubwa Ile Nahamishia Kambi Ubungo Mala paa tunabambana uso kwa uso
Apo ndo shoo Panakuwaga hapatoshii.
Hasa dada zangu wauza Bar anakumbia bila kukwambia Alafu ile Bar aliyo hamia kumbe ndo maeneo yako ya kujidai unawateja Kama wote
, ukimkuta anakuwa mpole kinoma so mnafanya kuanzia mlipo ishia.

Yote kwa yote Ni kazi ambayo ukizoea kudai watu raha sana asee
 
Ivi kwanini mtu anakua na roho ya utapeli,kwanini mtu anachukua kitu Cha mtu unajua kabisa sitomlipa.

Aisee tubadilike.
Mkuu unapokopa wala hupangi kua hutolipa , na unakua na mipango hasa kua mtalipa hivi au vile. Sasa Kwa kua kukopa ni Pepo , hivi ukipata hela ya kulipa linakuja wazo ngoja nimpe robo wakat mfukoni ipo yote . Hapo ndio shida huanzia mkuu
 
Kununua kitu kwa kulipa kidogo kidogo ni hasara.
Simu ya 300000 mtu hulipia 700000
 
Muha hadi afike kariakoo anauwa amejizatiti saaanaa...
Nyie kigoma ni level nyingine
 
Ukijua ni kukopa ujue na kulipa ukiweza kukopesha na kudai uweze
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…