Utotole
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 6,606
- 4,262
Focus ya uzi huu ni habari inayomhusu First Lady
Jana nilitazama na kusikiliza taarifa ya habari toka vyombo mbalimbali vya habari na mojawapo ya habari zilizotawala ilikuwa ile ya Mke wa Rais kutembelea makazi maalum ya wazee na walemavu, Nunge, Kigamboni jijini Dar es salaam. Akiwa huko alitoa msaada wa chakula kwa wazee hao kwa kiwango ambacho labda walikuwa hawajazoea.
Nilitegemea magazeti leo yataandika kuhusu habari hiyo, na huenda yameandika maana sijayatafuta ili nijionee. Ila nimebahatika kulipata hili lililopo kwenye picha hii na kilichonishangaza ni hiyo headline iliyotumika: "Mama Magufuli atumbua majipu". Yaani siku hizi kila alifanyalo mtu aidha ni jipu ama kutumbua jipu? Yaani kutoa msaada wa chakula kwa waze na wagonjwa nako ni kutumbua jipu? Huu uandishi wa ajabu ajabu namna hii unatupeleka wapi?
Waandishi jaribuni kidogo basi kutumia akili na weledi katika kazi yenu!