Hawa SSRA wanatumiwa na nani?

Hawa SSRA wanatumiwa na nani?

Joined
Jun 21, 2012
Posts
27
Reaction score
8
Ndugu wana JF kuna dhana mbalimbali zimeibuka juu ya sababu ya mabadiliko ya sheria ya mafao ya kujitoa, dhana hizi ni
1. Inasemekana NSSF na PPF wanajiandaa kuwachotea CCM fedha za kampeni 2015

2. Inasemekana baada ya serikali kukopa fedha nyingi kwenye haya mashirika yaani NSSF na PPF sasa yanaelekea kufilisika.wadau km kuna yeyote ana tetesi zaidi aziweke ili zitusaidie kuwaeleza waTz wengi zaidi.
nawasilisha
 
sababu kubwa ni
makampuni yenyewe kufuja pesa
maandalizi ya kukwapua pesa nyingi ku-fund ***** wa CCM
incompetence ya CEO wa SSRA na vyeo vya kupeana
myopic vision ya leaders wetu
ububu wa wabunge wetu

siasa imeharibu tanzania
 
hivi ***** ni tusi?

yani uppupu' imekua tusi siku hizi?
 
sababu kubwa ni
makampuni yenyewe kufuja pesa
maandalizi ya kukwapua pesa nyingi ku-fund ***** wa CCM
incompetence ya CEO wa SSRA na vyeo vya kupeana
myopic vision ya leaders wetu
ububu wa wabunge wetu

siasa imeharibu tanzania

dadavua kidogo hapo kwenye red
 
Watanzania tunashuhudia kulewa kwa madaraka kwa chombo hiki ambacho kimeshindwa kudhibiti ubadhirifu uliokithiri katika mifuko ya hifadhi ya jamii na badala yake kuwageukia wachangiaji na kutaka kuwadhiti bila hata kuwajua. Hivi mnajua tofauti ya wachangiaji wa mifuko hii? Mfano mdogo tu hivi hii sheria ilifikiria athari yake kwa makundi mbalimbali yaliyotofauti?

Mimi nina mkataba wa kazi wa miaka miwili kuishia Dec 2012.
Baada ya hapo sina kazi nilitegemea nichukue mchango wangu unisaidiekatika kujikimu mpaka nitakapopata kazi nyingine au nijiajiri mwenywe kwa kuwekeza pesa hii. Unaposema nisubiri nifikie umri wa miaka 55 unampango gani wa kunihudumia na kujikimu?
Je, unaniahidi kazi kwa miaka iliyobaki hadi miaka 55?

Huu ni mfano mmoja tu katika mingi ya kuonesha kuwa mmekurupuka katika sharia hii na kwa bahati mbaya wabunge wetu waliishia kurebisha spelling na semantics badala ya content na construction ya sheria yenyewe.


Tumewasikia mkianza kunywea kwa wafanyakazi wa migodii lakini jueni wao ni 'tip of iceberg


Katika hili sina wasiwasi kuwa serikali msipolishughulikia kwa haraka na kusitisha sheria hii kwa ujumla wake mtakuwa mnachezea ukomo wa uvumilivu wetu ambao nadiriki kusema hamuujui!
 
Katika kile kinachoonekana kama kelele za mpita njia hazimzuii mwenye nyumba kulala Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii-SSRA imesema haishtushwi na kelele zinazopigwa na wafanyakazi kote nchini kuhusu sheria mpya inayopiga marufuku wafanyakazi kuchukua stahiki zao wanapostaafu hadi wafikishe miaka 55 na badala ya ke imesema tayari sheria hiyo mpya imeanza kutumika tangu Julai 20.

Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji cha SSRA, imefafanua kuwa sheria hiyo imeshaanza kutumika na maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi muongozo mwingine utakapotolewa.

Ilibainisha kuwa lengo la kusitisha maombi ya kujitoa uanachama ni mamlaka na mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa elimu kwa wadau ambao ndio wanachama wa sekta hiyo.

Taarifa hiyo ilisema wamesitisha fao la kujitoa si kwa sababu ya serikali au mifuko ya hifadhi kufilisika kama baadhi ya watu wanavyodai bali inalenga kuboresha maslahi ya wanachama.
"Tunapenda kuwahakikishia wanachama kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ni thabiti na michango yote ya wanachama iko salama.
"Tunawaomba wanachama na wadau wote wa sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu mchakato huu ukiwa unaendelea kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya wanachama," ilisema.

Source:Tanzania Daima
 
Hivi ni nini tofauti ya pension na social security? Je kwa hapa TZ kuna hiyo tofauti? Inaweza ikatusaidia ktk hii debate inayoendelea kuhusu withdraw benefits.
 
Hapa ndio naona kuwa bunge letu ni dhaifu na rais wake dhaifu,hivi unaweza kupitisha kitu kama hiki kweli''''''pia nashangaa ssr wametoa wapi jeuri ya kusema hawatishwi na kelele za wafanyakazi wakati ndiyo wateja wao'.

Lakini msemo mmoja unasema ikibidi kufa tufe tukidai haki zetu,wafanyakazi acheni woga amkeni mdai haki zenu kwani wabunge hawasaidii kitu angalia hata mshahara hayawasaidii lakini menyewe yajipigia debe kupanda hata huyo rais ni nani tusimpindue kwani lazima tufike 2015
 
Katika kile kinachoonekana kama kelele za mpita njia hazimzuii mwenye nyumba kulala Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii-SSRA imesema haishtushwi na kelele zinazopigwa na wafanyakazi kote nchini kuhusu sheria mpya inayopiga marufuku wafanyakazi kuchukua stahiki zao wanapostaafu hadi wafikishe miaka 55 na badala ya ke imesema tayari sheria hiyo mpya imeanza kutumika tangu Julai 20.Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji cha SSRA, imefafanua kuwa sheria hiyo imeshaanza kutumika na maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi muongozo mwingine utakapotolewa.
Ilibainisha kuwa lengo la kusitisha maombi ya kujitoa uanachama ni mamlaka na mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa elimu kwa wadau ambao ndio wanachama wa sekta hiyo.
Taarifa hiyo ilisema wamesitisha fao la kujitoa si kwa sababu ya serikali au mifuko ya hifadhi kufilisika kama baadhi ya watu wanavyodai bali inalenga kuboresha maslahi ya wanachama.
“Tunapenda kuwahakikishia wanachama kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ni thabiti na michango yote ya wanachama iko salama.
“Tunawaomba wanachama na wadau wote wa sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu mchakato huu ukiwa unaendelea kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya wanachama,” ilisema.

Source:Tanzania Daima

Huu ni ufedhuli na kiburi cha hali ya juu.Mlaaniwe wote mnaotaka kuangamiza maisha ya watanzania.
 
Mbali ya kuwa na Mkakataba wa Muda maalum, pia kuna tatizo la kutunza kumbukumbu!
Kuna baadhi ya makampuni yapo yapo tu ambayo ni ya watu binafsi, ambayo muda wowote yanaweza kuaga. na inafikia mfanyakazi anaachishwa kazi akiwa na umri wa miaka 30.
Je, ni nani atakayekuwa anatunza document za mfanyakazi kwa muda wakati anasubiri afikishe umri wa miaka 55?
Nimeshuhudia baadhi ya makampunzi zinatunza documents kwa muda wa miaka 6, baada ya hapo wanateketeza za zamani.
 
Mwanzo si alikuwa anapenda kuuza sura kwenye vyombo vya habari
naona sasa ameanza kukimbia kila anpoitwa hatokei.
Kila mtu ana usongo nae.....

Nafikiri hana kosa. Wenye makosa ni wabunge tuliowatuma watuwakilishe kuipitisha hiyo sheria mbovu na kandamizi. Sasa unaweza kuelewa ni kwa nini kila kona ya nchi ni ufisadi na mikataba mibovu
 
Wakuu,

Hivi huyu mama Irene Isaka wa SSRA ni nani? Ametokea wapi? Amesoma wapi na kasomea nini?

Asante.
 
Mwanzo si alikuwa anapenda kuuza sura kwenye vyombo vya habari
naona sasa ameanza kukimbia kila anpoitwa hatokei.
Kila mtu ana usongo nae.....

nasikia amesema hatishiki na kelele za wafanyakazi, nao naye anatumia kale kamsemo ketu "liwalo na liwe".
 
Jinsi tulivyokuwa ndio mzee, na hili litafanikiwa na kukaa kimyaa huku haki yetu ikizama, tumakenii nakuacha porojo za mitandao.
 
Back
Top Bottom