Hawa SSRA wanatumiwa na nani?

Katika kile kinachoonekana kama kelele za mpita njia hazimzuii mwenye nyumba kulala Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii-SSRA imesema haishtushwi na kelele zinazopigwa na wafanyakazi kote nchini kuhusu sheria mpya inayopiga marufuku wafanyakazi kuchukua stahiki zao wanapostaafu hadi wafikishe miaka 55 na badala ya ke imesema tayari sheria hiyo mpya imeanza kutumika tangu Julai 20.

Taarifa iliyotolewa jana jijini Dar es Salaam na kitengo cha Mawasiliano na Uhamasishaji cha SSRA, imefafanua kuwa sheria hiyo imeshaanza kutumika na maombi mapya ya kujitoa yamesitishwa kwa kipindi cha miezi sita hadi muongozo mwingine utakapotolewa.

Ilibainisha kuwa lengo la kusitisha maombi ya kujitoa uanachama ni mamlaka na mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa elimu kwa wadau ambao ndio wanachama wa sekta hiyo.

Taarifa hiyo ilisema wamesitisha fao la kujitoa si kwa sababu ya serikali au mifuko ya hifadhi kufilisika kama baadhi ya watu wanavyodai bali inalenga kuboresha maslahi ya wanachama.
“Tunapenda kuwahakikishia wanachama kuwa mifuko ya hifadhi ya jamii ni thabiti na michango yote ya wanachama iko salama.
“Tunawaomba wanachama na wadau wote wa sekta ya Hifadhi ya Jamii kuwa na utulivu mchakato huu ukiwa unaendelea kwa lengo la kulinda na kutetea maslahi ya wanachama,” ilisema.

Source:Tanzania Daima

Huo ni ujasiri wa kifisadi kabisa.........shame on you na yeyote aliyekua nyuma ya hilo tamko. Wezi wakubwa nyie na siku yenu inakuja hata kama sio kesho lakini iko njiani.
 
it was VERY STUPID DECISION, sijui ni ya wabunge au SSRA wamekurupuka!
Wangekuwa na upeo wangeweza kurekebisha wizi wa miaka yote unaofanyika, mtu unachangia miaka 1, 5, 20, 40… halafu unakuja kupewa mchango wako tu eti na riba ya 1%, it was nonsense. Sasa wanakuja na kubwa kuliko…

Nalipa PAYE almost 30-40% ya mshahara wangu, uliobaki nalipia kodi tena kwa kila ninachokinunua 18%! Nakatwa NSSF 10%, mwajiri wangu ananibana kunipa mshahara mkubwa akidai anatoa 10% kunilipia NSSF. ina maana zaidi ya nusu ya kipato changu kinarudi serikalini kwa ajili ya kodi na PAYE..... wadau mnalijua hilo?

maskini huyu mtu amefanya kazi karibu 12 years, na mchango wake sasa ni zaidi ya 70M! hata utaratibu wa sasa hususani NSSF kwamba ukifika 15 years ya kazi, unakuwa pensinabo! hata ukiacha kazi na umefikisha miaka hiyo 55, unalipwa robo, ingine unaanza kulipwa kidogo kidogo kwa mwezi sooo kigodo huku wakiombea ufe! then that is the end! Halafu huyu ndugu akifa leo, ati sharia inasema wraith wapewe mchango wake tu wa mwajiri wanabaki nao… imagine!

life span ni ndogo so mabilion ya pesa yamekuwa yakiachwa hata kwa utaratibu uliopo juzi! sasa wakaona hizo zinazobaki hazitoshi badala yake wanataka watu wafe wengi na zibaki zaidi... ndio lengo la SSRA na serikali yake ambayo niliitiii hadi juzi nilipochoma kadi ya CCM! kwa mara ya kwanza nimewaelewa wa Tunisia/Libya/Egypty.

Mama huyu wa SSRA anatuambia eri unakatwa 10% tu na kama maendeleoa ungefanya na hio 90% (kasema Jahazi) eti hio 10% itakusaidia nini! what the hell is this?

nilitaka niache sawa kazi za mwajiri wangu ili nichukue mtaji nijianzishie ujasiliamali na niajiri wa Tz wenzangu wapo mtaani, sasa wanakuja na uchawi huu.

siamnini kama wabunge walijadili, watu kwa sasa tunafuatilia sana n bunge, iweje hii ipite hivi hivi? ona maoni ya watu hapo juu, nenda jamii forum.. ina maana hatukuona haya yote, walichojadili ni kinachofanana tu wala sio direct la kusitisha mchango wa kujitoa. au vile wabunge mafao yao hupokea baada ya miaka 5 hawayaoni haya?

If wabunge wetu walijadili na kulielewa hili, basi wanastahili tuanze kwa kuwapiga mawe! ndio
tumechoka na vitu kama hivi ambavyo vinahitaji kufikia kwa kichwa chepesi.

nina hasira sana

mdau
Nokoyani Sijwagu.
 
Huyu kila Irine Isaka eti ni Daktari wa uchumi!!! but to me ni wa mangumashi as far as I know her, well!!!! She is incompetent!!! Na jibu alilotoa ni very low for a PhD holder. I doubt kama hakupata zile maksi za Chuuuuuuu ppppppi!!! Aondolewe hiyo taasisi!!! Tatizo ni kwamba hizo Security funds zote PSPF, GEPF, NSSSF, PPF na LAPF walikubali kuingia miradi ya real estate ambayo inahitaji hela nyingi na wateja wakiwa ni serikali (angalia ujenzi wa UDOM, nyumba za askiri, and the like) na payback period ni muda mrefu!! Na sina hakika kama kila mwezi kuna repayment!! Kwa mantiki hii haya mashirika ya Social security financially are inshamble hasa the NSSF!!!!!! Na ndiyo yanashauri sana sheria ibane kwa makosa yao ya poor investment planning!!!!! Sasa badala ya huyu mama Daktari wa uchumi awashauri wawekeze hela ya wanachama katika viable and short term paying ivestments inataka eti watu waache hela zao kule. Siku hizi watu hawategemei kazi za kuajiriwa milele. Vijana wanafanya kazi for a certain perion of time anaamua kufanya shughuli zake na pension contribution yake inatumika as part of his/her seed capital. Irine I know you, use your common sense. Ukishindwa consult kina Dr. Mkenda and others can help you madam. Utasababisha sekeseke mbaya na mwishowe hapo utaondolewa!!!
 
Mkuu mimi naona tunawaonea SSRA, Kwani wao wanatakeleza sheria iliyotungwa na wawakilishi wetu! Tuwe makini kuachagua wabunge, Tukiendelea kuchagua watu wanapitisha na kuunga mkono 100/100 matokeo yake ndiyo haya Mkuu!

Kama haujui kaa kimya SSRA ni ma****(Bonge la tusi) wao,wakurugenzi wa mifuko na jinga kubwa(dhaifu) ndio waliofanya huu ufirahuni,ssra ni vilaza yani Dr mzima irene anashindwa kitu kidogo kama hichi kweli udr wake ni wa pichu kabisa!
 
Gazeti la Mwananchi la tarehe 24/07/2012 limeandika hivi "Hata hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Irene Isaka alisema jana kuwa: “Hakuna haja ya watu kuwa na wasiwasi, maana sheria hii itafuatiwa na kanuni na miogozo mingine ambayo ninaamini kwamba itaondoa wasiwasi uliopo”.
Isaka alisema miongoni mwa mambo yatakayozingatiwa katika miongozo hiyo ni iwapo mwanachama atafukuzwa au kuachishwa kazi, wanachama ambao wako kwenye kazi za mikataba na wale wanaopata ulemavu wa kudumu wakiwa kazini.

“Kimsingi ni kwamba suala la mafao ya kuacha kazi kabla ya umri wa kisheria wa kustaafu limefutwa kwa mifuko yote, isipokuwa katika mazingira hayo niliyoyaeleza litawekewa miongozo, na hii ni kwa faida ya wachangiaji,”alisema Isaka.

Alisema baada ya sheria hiyo kuwa imepitishwa na Bunge, kisha kusainiwa na Rais Jakaya Kikwete mwezi Juni mwaka huu, SSRA ilianza mchakato wa kuweka miongozo na baada ya hapo kinachofuatia ni kutoa elimu kwa umma na baadaye kuanza kutumika kwake rasmi.

“Lakini sasa tumelazimika kuanza kutekeleza sheria hiyo mapema kuliko tulivyopanga hasa baada ya kutokea kwa suala hili kwenye public (umma) kabla ya muda tuliokuwa tumekusudia,”alisema mkurugenzi huyo.

Isaka aliongeza kuwa chimbuko la sintofahamu iliyojitokeza ni baadhi ya mifuko kuchezeana rafu kwa lengo la kupata wanachama wapya kwenye migodi na kwamba wao kama wadhibiti tayari wametoa onyo kwa mifuko iliyohusika.

“Kwanza hakuna mfuko wowote ambao una mamlaka ya kutangaza kuanza kutumika kwa sheria, ni SSRA tu wenye mamlaka hayo, kwa hiyo tumewapa onyo, kama wanajitangaza wajitangaze kwa kueleza uzuri wa mfuko wao ni siyo kuchafuana au kuchafua wengine,” alisisitiza".

Kauli hizi za Mtendaji mkuu wa SSRA zingekuwa na maana kwa sasa kama angejitokeza katika redio na TV zilizopo nchini akadokeza hayo anayodai kuwa yatajitokeza na kumaliza mzozo na mgogoro unaojitokeza kati ya wafanyakazi
 
Back
Top Bottom