Hawa ni watoto au maharamia?

Hawa ni watoto au maharamia?

Wide Open EYES

Senior Member
Joined
Jul 16, 2015
Posts
140
Reaction score
57
Siku yangu imeisha vibaya sana leo.

Niko kijiwe changu cha kuuza mbao, biashara hamna kabisa. Napigiwa simu na mama tunafahamiana kwa karibu anatuma watoto wake kuja kununua mbao. Nikaanza kujipanga na kufurahi kimoyo moyo, jf weka kule kwa sababu ndo iliyoniweka busy huku nikihesabu magari yanayopita barabarani.

Vijana wakafika wa kike na wa kiume tukaanza kupimiana mbao, shughuli ikiendelea yule wa kike akanifuata anataka nimdanganye mama yao bei ya mbao ili wabaki na hela. Watoto bila hata soni wataka kumuiba mama yao. Karibu nikubaliane nao sijauza hata mabanzi na wiki ndio inakata hii.

Hivi kuna haja gani ya kumuibia mzazi wako? Hela ya huyu mama ni pension yake baada ya kustaafu, watoto wake wa kuwazaa wasipoona huruma nani atamuhurumia?

Cha juu zipo nyingi lakini hii wacha inipite
 
Hivi ndo CCM ilipotufikisha.
Kila mahala tunapiga dili
 
kiukweli utu umetoweka ktk kizazi hiki. unaweza ukasikia mzazi fulani akilalamika kuhusu mtoto wake asivyomjali,akakukumbusha jinsi mtoto wa jirani yako asivyowajaliwazazi wake. jirani yako naye akilalamika unakumbuka mtoto wako alivyojali mambo yake na kupuuzia shida zako. huu ni utamaduni mpya wenye sura ya jinamizi. haishangazi lakini inatisha. tufanye nini ? hiyo ndiyo issue.
 
Dhambi zipo nyingi tu, labda hii ingetokea miaka mitano iliyopita sidhani kama ningeiacha. Nimeshashiriki hii dhambi ya cha juu mara kibao, hii ya leo sijawahi kuiona.

kama ni kweli, basi Mungu akusamehe dhambi ( kama unazo) maana ni wafanyabiashara wachache wa aina hii. Be blessed.
 
We unashangaa hao madogo mi kuna mzee wa kanisa nime enda nae sawa kiroho safi!
 
Siku yangu imeisha vibaya sana leo.

Niko kijiwe changu cha kuuza mbao, biashara hamna kabisa. Napigiwa simu na mama tunafahamiana kwa karibu anatuma watoto wake kuja kununua mbao. Nikaanza kujipanga na kufurahi kimoyo moyo, jf weka kule kwa sababu ndo iliyoniweka busy huku nikihesabu magari yanayopita barabarani.

Vijana wakafika wa kike na wa kiume tukaanza kupimiana mbao, shughuli ikiendelea yule wa kike akanifuata anataka nimdanganye mama yao bei ya mbao ili wabaki na hela. Watoto bila hata soni wataka kumuiba mama yao. Karibu nikubaliane nao sijauza hata mabanzi na wiki ndio inakata hii.

Hivi kuna haja gani ya kumuibia mzazi wako? Hela ya huyu mama ni pension yake baada ya kustaafu, watoto wake wa kuwazaa wasipoona huruma nani atamuhurumia?

Cha juu zipo nyingi lakini hii wacha inipite

uzao wa ccm hao
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom