Hawa NHC wanachofanya ni sawa?

Rutunga M

JF-Expert Member
Mar 16, 2009
1,769
1,382
kwa muda wa siku mbili sasa NHC wanafurusha wapangaji wasiolipa huku wakiwa na Lundo la waandishi wa TV,leo kwa waliotazama channel ten habari ya saa 1;00 usiku,kwakweli nimeona move ya bure pale MAELEZO.

Serikali Vs Serikali kugombana vile siyo sawa!

Je wataendelea AU leo ndiyo mwisho
 
Naona wanafanya vizuri kabasa,Kama mtu unashindwa kulipa kodi kwanini uachwe? Na kwa serikali ni vzuri sana kwani bajeti wanayotengewa wanaweka wapi? Mbona posho wanalipana soon! Why not rant?
 
Naona wanafanya vizuri kabasa,Kama mtu unashindwa kulipa kodi kwanini uachwe? Na kwa serikali ni vzuri sana kwani bajeti wanayotengewa wanaweka wapi? Mbona posho wanalipana soon! Why not rant?


Kwa sekta binafsi sawa,lakini kwa idara za serikali siyo sawa kwani fedha hiyo hiyo ya NHC ndiyo inayoendesha idara zenyewe
 
hata tanesco iliwahi kuendesha zoezi kama hili kwa idara zote za serikari, tofauti ya hawa ni kuwa lazima watoe vyombo nje hapo ndipo zoezi linapoonekana maana vitu ni vingi tofauti na hapo usingefahamu au kuona zoezi la jinsi hii.
 
Tena nadhani Wizara ndizo zilipaswa kuonyesha mfano bora wa ulipaji kodi ya pango kwa Ofisi zao. Lakini imekuwa kinyume, wizara zimekuwa zikilimbikiza madeni ya malipo kama pango, umeme, maji nk. Cha kushangaza, kila mwaka huko Dodoma Bungeni huwa zinapitishwa bajeti kwa matumizi ya Wizara hizo na Idara zake, je fedha hizo huwa zinatumikaje? Audit reports huwa hazionyeshi namna fedha zilivyotumika? Kuna mengi ya kuuliza... Ni sahihi kabisa wafanyavyo NHC.
 
National Housing wameonesha mfano, sasa TANESCO nao wafuate, kwani wadaiwa sugu wa TANESCO ni serikali yenyewe! Waende tu kukata umeme, mpaka bili zote zilipwe. Wanajiwekea mafungu ya mabilioni kwenye chai na soda kwa wageni, kila mwaka wa bajeti, lakini kwenye umeme wanaweka kiasi kidogo sana! Ulaji, ulaji, ulaji! Sasa basi! Hongera MCHECHU, ila MMECHEMKA kuibomoa ile nyumba nzuri ya Mtaa wa Tosamanganga, Masaki!
 
Ni vyema kabisa na nawaunga mkono 100% Tujiondoe kutoka Taifa omba omba.
 
Ni vyema kabisa na nawaunga mkono 100% Tujiondoe kutoka Taifa omba omba.
Well said FF... inakera sana kuona mijitu iko na masuti tena hapa nazungumzia finance managers wa idara za serikali lakini wanashindwa hata kutumia basics zao za shule kujua maana ya kubalance vitabu

Hivi wanategemea nani awalipie kodi??

ingekua ni muhimbili au mashule sawa, sasa hata maelezo jamani?? wameshindwa hata kuuza video na vitabu vya viongozi wetu na matukio muhimu??

mambaff
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom