Hiki kisa mtu anaweza kudhani ni masikhara,lakini imetokea na ni kama mwezi umepita tu
Mhanga ambae ni mwalimu wa shule moja ya msingi hapa jijini Mwanza ailikuwa na mkewe wa ndoa,huyu ni mwanamke ana mvuto wa hali ya juu na vijana huwaita bomba na sio masikhara alikuwa bomba kweli
Mumewe alichukua mkopo na kumfungulia mkewe stationary ili kuongeza pato la familia,stationary hiyo alifunguliwa mwaka 2010 mwezi wa 9 hivyo ilibaki kama mwezi 1 hivi itimize miaka 4
Picha lilianza pale mkewe na mwalimu huyo kuanza kuchelewa kuja nyumbani na yule mwalimu wakati mwingine alipokuwa anapita kazini kwa mkewe alikuwa anakuta amefunga muda ambao sio sahihi na nyumbani anachelewa kurudi,mumewe akimuuliza hatoi majibu ya kuridhisha
Mumewe yule dada alikuja kuambiwa kuwa mkewe anamahusiano na jamaa mmoja hivi wa Arusha na huyo jamaa huwa anakuja huku kuponda raha mara kwa mara
Ilifikia mpaka mkewe na huyu mwalimu akawa halali nyumbani na kazini kwake haendi
Ndipo jamaa aliamua kumpa kipigo ili aseme huko anakoenda kila uchao,lakini badala ya kusema mkewe aliondoka na baada kama ya dakika 45 alirudi akiwa kwenye gari aina ya toyota vx na kushuka akiwa na yule hawara yake
Waliingia na kumkuta mumewe na yule dada akipika chakula maana alikuwa ni saa 1:45 za jioni na walikuwa na mtoto wa miaka 4, hivyo alikuwa anahitaji kula
Mkewe jamaa alipofika na hawara yake na kumkuta mumewe akipika akasema "umenipiga na kuniuliza nilikokuwa ninakwenda,sasa badala ya kukuambia nimeona nikamlete kabisa mhusika ili ujue na uone wanaume rijali na sio wewe unanitisha na kiststationary chako cha mkopo,kila siku maneno hayaishi,sasa huyu ndo mwanaume sio wewe mwanume suruali,sasa kwa taarifa yako leo ndo mwisho wako wa kuiona naondoka zangu na kama kuna chochote unachonadai sema ulipwe,sitaki unipigie simu wala kunitua sms,na mahari yako uliyowapa wazazi wangu hiyo hapo{huku akiweka burungutu la fedha mezani baadae ilikuja kugundulika kuwa zilikuwa sh 1,500,000,gharama za mahari alizolipiwa wakati anaolewa} na ole wako unifuatefuate kwa chochoye"
Mumewe hukusema kitu na baada ya kimya hicho mkewe aliondoka na hawara yake na kwa sasa wanaishi Arusha
Mwanamke huyu hadi leo ni mwezi umepita na hata hamuulizii mwanae wa miaka 4 aliemuacha huku
Mumewe ameanza maisha mengine na pale stationary ametafuta mfanyakazi!!!
Hayo ndo maisha ya kwenye baadhi ya ndoa!!!!!!!
Mnaoana kwa mbwembwe nyiiingi halafu mnatengana kijinga namna hii???????????