Kambi ya Fisi
JF-Expert Member
- Feb 3, 2018
- 13,480
- 21,955
Yaani wananikera sana hawa watu watatu...
1. Watu wenye PhD feki
Ni watu wanaojivika PhD pasipo kuhudhuria masomo yoyote chuo kikuu.
Hivi kwa nini wadanganye kile wanacho weza kukipata kwa heshima?
Kuna vyuo vingi sana vinavyoaminika hivyo badala ya kujipachika PhD feki waende chuo kikuu na wakafurahie uzoefu wote wa masomo ndipo waipate hiyo PhD.
2. Watenda miujiza feki makanisani
Watu hawa hudanganya kwamba wana nguvu za Mungu na wengi wao hutembea huku wakilindwa na mabaunsa walio Waajiri
Ni waongo na hata hiyo miujiza feki huwauzia watu kwa kutoza hela nyingi (sadaka) ili wajipatie hela za kula bata na makahaba huko nightclubs ila kiukweli sio watumishi wa Mungu bali ni wahuni fulani tu.
3. Marais wala rushwa
Wanapata mshahara zaidi kuliko raia,hawalipi bili yoyote lakini hawaridhiki.
Wao hufurahi wanapoona mamilioni ya watu wakitumbukia katika umaskini, huwa hawana mipango ya kustawisha jamii, bali mipango yao ni kujinufaisha kibinafsi na familia zao.
Kiukweli kiongozi wa juu anapokuwa fisadi huiporomosha serikali yake yote.
Mabadiliko huanza na kichwa. Kichwa kinapoharibika mwili wote huharibika.
#Nani anakukera zaidi?