Hawa ndio washindi kuingia NEC ya CCM kwa uchaguzi wa Nov 11, 2012

Hawa ndio washindi kuingia NEC ya CCM kwa uchaguzi wa Nov 11, 2012

Hivi sasa ni waziri wa mahusiano katika hii Serikali.Cha ajabu,anashindwa kutatua migogoro ya kidini, je akiwa raisi si itakula kwetu kweli!
 
Duh, hii kali, lakini kila kitu kinawezekana!
 
Mambo hadharani.

kama hamjui basi hiko hivi.

mh. Membe ndiye mgombea urais wa CCM.

take it.
 
mi nita suggest sura yake iwekwe kwenye bank notes:becky:
 

Lakinii PIA ni AJABU kupata kura HIZO kaanza kuifanyia kazi CCM Miaka 2 iliyopita sio WENGI wanaomfahamu - Hana PURUKUSHANI kama NAPE NNAUYE au MCHEMBA

Kwahiyo HE DID VERY WELL...

Kwahiyo nchemba kampita kwa kura kutokana na purukushani? kati ya purukushani na utendaji, purukushani reigns?
 
Kwahiyo nchemba kampita kwa kura kutokana na purukushani? kati ya purukushani na utendaji, purukushani reigns?

Hauijui CCM? Ukipayuka na Purukushani za USIKU na MCHANA... Hauwaoni kwenye MIKUTANO yao ya CHAMA? Wanvyofyatua MIDOMO bila kikomo hadi MATUSI???

Lakini, Haujui hata kama kuna Katibu Mkuu wa CHAMA CHA MAPINDUZI... LOW DOWN PERSON...
 
CCM imegeuka kuwa chama cha ajabu sana; Yani Katibu Mkuu wa Chama aliyepo madarakani anaponea chupuchupu kwa kushika nafasi ya tisa kwa idadi ya kura, kati ya jumla ya idadi inayotakiwa ya watu kumi?

Mambo kama haya hayajawahi kutokea; Ina maana huyu Katibu Mkuu alikuwa anafanyeje kazi na viongozi waliomshinda kura ambao technically ni junior kwake kicheo ndani ya chama, hasa yeye akiwa ndio mtendaji mkuu - Kina nchemba, Makamba, Shigela? Hii inatoa ishara gani kuhusu nani ndio alikuwa anakiendesha chama, na nani atakiendesha chama kuelekewa 2015 na kwwa malengo yepi? Kwa kweli matokeo haya yametoa picha very interesting kuhusu jinsi gani chama hiki hakitaisha na migogoro;

Vinginevyo naona majina mawili tu ambayo yatajenga, mengine yatabomoa tu zaidi!
Da nilikuwa staki kuchangia thread hii lakini baada ya kuona mchango wako leo uko katika aina hii ya uchangiaji,kwa mara yangu ya kwanza naona leo wewe umekuwa critics wa CCM publically hivi.

Hakika kwa thread hii umeona mbali sana sana!!Ni hakika picha hiyo uliyoiona ni mbaya sana,kwa kuwa ni ishara ya kuwa mtendaji mkuu wa chama chenye kuongoza Nchi hana chake hata kama kachaguliwa kwenye hiyo NEC kwa kura ambazo zinaonyesha hatihati.Kwa ujumla ndani ya CCM kwa ujumla wake mambo si shwari.

Binafsi nakubaliana nawe kuwa waliomo kwenye list hiyo ambao wanaweza kuwa na hisia za kujenga na si kubomoa ni wachache mno binafsi namuona Membe, kwa kuwa anaukomavu wa kisiasa wenye kuliona Taifa na sio sura za kikundi cha kwetu kipi??Wengineo ndio kama hivyo,sura za pochi, binafsi uwa nawahurumia sana vijana wanaobebwa kufika kwenye hadhi za madaraka ya kijamii kubwa kama hizo, eti kwa pochi na mafuko ya mamilioni na mabilioni ya pesa ya wazee,!!!!!.Manake tukiwa kama binadamu tunaishi na kuzungumza na nafsi zetu za ndani tukiwa pekee yetu,Je vijana wanaofika kwenye ngazi za mamlaka kwa kubebwa dhamila zao uwa zinaongea vipi jamani?

Mkuu kesha sema kuna majoka ndumila kuwili kazi kwao!!uzuri kijana ambae nimejifunza ndani ya CCM anaejaribu kuonyesha kuwa anasimama pekee ni NAPE na hata shibuda mzee wa zenjishy kawaambia CCM kuhusu nape,the rest of the young CCM Leaders, sipendi matendo yao ya kukubali kutumiwa.

Manake mwisho wa yote kila upande utakaopata nafasi kushinda utahakikisha vijana waliotumika wanapotea kwenye ulimwengu wa siasa na uchumi.Hakika vijana hao hawaoni haya kuwa wamekuwa maalufu kupita mzee ambae ni BABA yao kwa umri,kwa kuwa Mzee Mukama anavijana wake pale Oysterbay wanalingana sawa na vijana waliomshinda mzee huyo alieanza kutumikia chama hicho hawajazaliwa.Tukichua mizania ya HAKI BIN HAKI vijana hao wamekitendea chama chao nini cha ajabu kuweza kumpiku Mzee Mukama umaalufu kiasi cha Mzee huyo kucheza nafasi za mabeki, licha ya kuwa pia anakofia ya ukatibu mkuu wa chama.

Hakika kwa picha hiyo, CCM wanaitaji MAPINDUZI NA SI MAGEUZI.Kwa kuwa kizazi cha vijana kutumika kwa namna hiyo ni hakika kuwa UKISIKIA ANAKWAMBIA HABARI ZA YULE,JUA KESHO ATAMWAMBIA YULE HABARI ZAKO WEWE!!!Naaaaaaaaaaaam na ndicho Mwenyekiti wao alichokiona.

Kwa sie tulioamua kuwa vijana tusio na vyama uwa natizama miendendo ya baadhi ya vijana hakika nawapa pole sana pale ambapo uamua kusimamia ITIKADI ZA WAZEE wao ndani ya vyama vyao na si Kuongozwa na KUSIMAMIA ITIKADI ZA CHAMA CHAO kama ndio mwongozo na dira yao kujenga chama chao hatimae huko mbele napredict majeruhi wengi sana vijana ndani ya chama cha mapinduzi ambao mbio zao za kisiasa kwa kutegemea migongo ya kutumwa na wazee kumchafua yule na kumjenga yule, wakiangaika !!!

Aksante kwa threa hii umeongea !!!!
 
Mkuu,
Hiyo inaonyesha kuwa demokrasia imefuata mkondo wake, pia hiyo ni 'statement' na 'verdict' kuonyesha kuwa utendaji wake kama katibu mkuu ulikuwa haukizi matarajio ya wana CCM wengi. Nitashangaa kama ataendelea tena kuwa katibu mkuu.

Ninawapongeza waasisi wa CCM kwa kuwa na maono ya mbali na kukata mrija wa demokrasia katika nafasi ya mwenyekiti taifa kwa sababu ninaamini wameepusha aibu isimfike 'incumbent' wa mwaka huu kwa sababu utendaji wake katika chama na serikali.

Labda tu niseme na kupingana nawe kidogo. Utendaji wa CCM hautegemei sana mtu mmoja kama ilivyo katika vyama vingine na ndiyo maana pamoja na udhaifu wa hali ya juu aliyoonyesha Mukama, CCM bado haikuyumba sana katika utekelezaji wa majukumu yake ya kawaida. Halafu unasahau kuwa haya majina ni muendelezo wa wajumbe wa NEC waliochaguliwa kupitia wilaya zao.

Sijui kama unaelewa pointi yangu ya msingi; Viongozi wa Chama kitaifa na pia Jumuiya yake (UVCCM), wanampiku vipi kura katibu wao mkuu ambae ndie bosi wao, huku mwenyekiti akipeta? Naomba utufafanulie mstari kwa mstari kwanini wao pamoja na mwenyekiti wao wameonekana ni bora mbele ya WAJUMBE WA MKUTANO MKUU WA TAIFA AMBAO NI WAPYA KABISA, kuliko katibu wao mkuu katika nyakazi hizi; Na kuhusu muendelezo wa wajumbe wa NEC waliochaguliwa kupitia wilaya zao nadhani kidogo ni nje ya hoja yangu ya msingi;
 
Kuna habari ziliwahi kuvuja kwamba Mukama alimuandikia barua mwenyekiti wake akitaka kuachia ngazi ya ukatibu mkuu, kwamba nape na mwigulu walikuwa wamejitwalia madaraka ya kukiendesha chama kama mali yao, nadhani hiyo inaweza kuthibitisha kwamba hakuwa na nguvu ya kutosha kukiongoza chama, na hayo matokeo yameonyesha ukweli wa mambo.

Kwa mtazamo wangu Mukama kuwania nafasi ya UNEC ni kuthibitisha kwamba ccm inatarajia kujipatia katibu mkuu mwingine kipindi hiki, atakayejaza nafasi ya Mukama.

Now you are talking, na ina maana basi hata wajumbe wa national congress wamevutiwa na watu wengine kuendesha chama kama mali yao, hivyo kuwapa kura nyingi zaidi kwa vigezo kwamba wao ndio viongozi bora kuliko mukama;
 
Mchambuzi,
Haumfahamu Mukama. Huyu ni mmoja kati viongozi wachache sana ndani ya CCM asiyejua kuhonga, asiyejua kununua kura, hana maswahiba, hana kundi wala kambi ndani ya CCM. Watu wa aina yake wanachaguliwa kwa taabu sana ndani ya CCM. Mimi nilimshangaa sana alipojitumbukiza kwenye kundi hili. Kura za KIITIFAKI zimemsaidia sana.

Hoja yako na ile ya mwita maranya kwenye bandiko namba 134 zina mashiko sana na kutufungua sana macho, kuliko hoja ya mwenzetu Ng'wamapalala kwamba kilichotokea ni demokrasia imefuata mkondo wake;
 
Huyo kwenye nyekundu ndo ambae alitakiwa awe our Presidaaa 2005 kabla ya organized mafia haijamcingizia kuhucika na mauaji ya Karume.. Naamini kama tungebahatika kuwa nae as our President tungekuwa na mafanikio zaidi.. Cidhani kama atataka tena kujihusisha na siasa tena.. Kiongozi muadilifu kama yeye ana ethics zake.. Hao wengine uliowataja mh..

Umenena kwa hakika Sosoliso huyo ndiye alitakiwa kuwa rasi 2005 sio kiraka Kikwete matokeo yake tumeyaona ubunge viti maalumu na ukuu wa wilaya umetolewa kwa njia ya chupi, maisha yamekuwa magumu na mfumuko wa bei mkubwa kabakiza misemo ya kijinga mfano tumethubutu, tumejaribu na tumeweza ujinga tupu hata akiwa anatoa hotuba unajiuliza huyu likuwaje akashinda urais? jibu linakuja alinunua ukuu wa nchi yeye na mafia wenzake.
 
...hii bidhaa ya uraisi ndani ya CCM imekuwa bei raisi sana kila mtu anauwezo wa kununua...sitoshangaa mbele ya safari kunako majaaliwa Mulugo nae akajitosa...

Hii inatokana na waTZ kupiga kura kwa mazoea bila kufanya tafakari zaidi ya kuangalia rangi ya kijani. Ipo siku watasimamishwa hata wanyama kwa rangi ya kijani na watu watachagua.
 
Back
Top Bottom