Hawa ndio washindi kuingia NEC ya CCM kwa uchaguzi wa Nov 11, 2012

Hawa ndio washindi kuingia NEC ya CCM kwa uchaguzi wa Nov 11, 2012

Kazi kwao.waacheni wapigane vijembe na kuchafuana kama Bashe vs Membe sisi tunawasikilizia tu.
 
Nikiangalia hii orodha naona karibia wote ni wa upande mmoja.

Ndio Ritz, wote ni CCM hakuna mpinzani hata mmoja! Pole sana mkuu, jaribu kufuta mawazo hayo mgando.
 
Last edited by a moderator:
Ana ile kitu tunaita UTHUBUTU. Sisi wengine hata kuweka jina halisi humu JF tumeshindwa! Kinachonishangaza mimi ni kwa nini familia ya Mzee wetu Malecela haikubaliki ndani ya CCM pamoja na kazi kubwa sana aloofanya mzee huyu ndani ya CCM na serikali yake. Mkewe kaanguka kule UWT. William naye kwenye NEC nayo hayumo wakati familia za Makamba, Kikwete, Nnauye,...., wanapeta tu!

jina la Malecela lina lahana ya Nyerere...
 
Wasira ameibuka kuwa maarufu sana ndani ya CCM. Kuna waziri mmoja nilizungumza nae akasema watu hawampi nafasi katika hali ya kawaida ila jamaa ni mwanasiasa mwenye mbinu za chinichini na imedhihirika kwa idadi ya kura alizopata NEC. Wakati Lowassa na membe wanapigana, yeye anajijenga na atanufaika kwa vita vya makundi. Tusubiri tuone
Hapa nachokiona,wanachama wamechoka na wale wanaosikika kila siku,kuwania urais.
Sasa kwa vile hata waliosahaulika na kufanyiwa fitina wanapewa nafasi;itabidi wote wanaotajwa kama Sitta,membe na Lowasa wasipewe nafasi ya kuwania urais ili kuondoa makundi.

YAAANI,kumrudisha Mangula kama makamu mwenyekiti,inafanana na jinsi navyosema hapo juu;kama chama kinataka kionekane kipo seriuosly,watafutwe wengine kabisaaaaa wasiosikika katika tamaa ya kutaka uraisi(kwani Ikulu kuna biashara gani?!!!!)

Hebu,tufukirie mmojawapo kati ya MEMBE,SITTA au LOWASA amepata nafasi ya Rais wa nchi,hali itakuwaje kwa yale makundi yaliyojitengeneza ndani ya chama?,itakuwa ni moto utakaokuwa unakiumiza chama katika mgawanyiko na kuporoka kawa namna ambayo itakuwa ngumu kuidhibiti.!!!!!

Mambo mengi wameshindwa kuyakabili na kuyamaliza kwa njia ya vikao,sasa itabidi kuwapiga chini wote wenye harakati za wazi za kuutaka urais,kwani athari za makundi,chama kimeshindwa kushughulikia kwa muda wote wa utawala wa JK.

unaona NEC katika nafasi hizo 10 wapo hao tunaowaona, lakini,wenye mikakati yao walienda kuomba kupitia wilaya zao.
 
Juzi mwanasiasa chipukizi na machachari Hussein Bashe aliibua madai mazito dhidi ya Waziri wa Mambo ya Nje na aliyekuwa mgombea wa ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa. Miongoni mwa tuhuma hizo ni kwamba Membe ni mwanasiasa asiye na uwezo wa kisiasa na ambaye amekuwa akipanda ngazi za siasa kwa kubebwa. Kimsingi alikuwa anasema kwamba Membe 'hachaguliki' huku akiapa kwamba atahakikisha kwamba hapati kura na kushinda kinyang'anyiro cha NEC.

Kwa kuangalia muegemeo wa kisiasa hapa nchini ni wazi kwamba Bashe ni mfuasi wa Lowassa na yeye mwenyewe ameshakiri mara kadhaa na hata juzi kwamba yeye ana nasaba za kiitikadi na Lowassa. Majibu ya Bashe yalikuwa yanahusiana na tuhuma ambazo kundi lao walielekezewa, wakidaiwa kwamba wanapita mikoani kueneza 'injili' ya kutenganisha kofia mbili anazoshikilia Mwenyekiti wa CCM Taifa ili abaki na urais na hivyo 'kukiimarisha chama'. Katika harakati zao hizo pia walidaiwa kupitisha orodha ya wanaotaka wachaguliwe NEC, msisitizo ukiwekwa kwamba jina namba 14 kwenye orodha ya wagombea ambalo ni la Membe lisichaguliwe. Hali hiyo ilijirudia na kujitokeza jana hapa Dodoma ukumbini, baada ya kutangazwa kwamba uchaguzi ungefanyika jana ile ile.

Kufika alfajiri ya leo ikawa ni bayana kwamba harakati za kumnyima kura Membe zilikuwa zimegonga mwamba kwani wajumbe waliojigamba kuwamiliki walikuwa wameamua kumpa kura za heshima kubwa Membe na hivyo kukiuka imani na dhamira ya genge (siyo kundi) hilo la Lowassa. Membe akawa amemjibu Bashe na Lowassa kupitia kwa wajumbe kwamba njama za wanasiasa uchwara wenye visasi na matumizi makubwa ya fedha na propaganda za vyombo vya habari walivyovinunua na kuvimiliki, haviwezi kuwatia upofu watanzania na kujua ipi ni lulu na ipi ni kokoto. HAYO YAKAWA Ni MAJIBU MARIDHAWA YA MEMBE KWA BASHE!
 
Bashe ni adolescent wasiasa na anadhani kwamba kuke kukaliwa kimya ni kwa kiasi kikubwa kukomaa na hata kudiriki kujitoa mhanga kwa ajili ya waliomtuma. Anadhani kule kubebwa kwake na Masha katika sakata ya uraia basi ndivyo ilivyo kwa kila mtu. Wasubiri surprise nyingine ziko njiani mpaka atakumbuka Somaliland.
 
Miongoni mwa watu wailoumia sana na Chenge na Mke wake kwa sababu mke wake amesikika akilalama kwamba kuna usaliti umefanyika kwa sababu haiwezekani kwa fedha zote walizozitumia halafu mambo yageuke vile. Bashe amegeuzwa condom na hivi karibuni atatupwa maana hatakuwa na thamani. Maskini mamilioni yao!
 
Membe ananikumbusha wimbo wa kisiki cha mpingo wa Mchinga Sound (RIP). Bashe anakuja na panga wakati wenye shoka wameshindwa.

Wakati kwa Bashe na waliomtuma siasa ni mchezo wa kubahatisha, Membe amedhihirisha kwamba siasa ni sayansi inayojengwa kwa mikakati na taaluma siyo kukurupuka na kutumia hazina ya fedha. Membe amedhihirisha kwamba uchaguzi bila fedha unawezekana.

Hakika Bashe alikuwa na kiu ya jibu lakini baada ya matokeo haya, kiu yake imeisha mpaka anatapika sasa. Membe bana!
 
Ningeshauri huyu jamaa ahangaike na kwao Somalia badala ya kujitiatia kwenye mambo yetu. Bashe lazima atumike kwa vile Rostam aliyemfuga kwenye kampuni yake ni mshirika wa Lowassa. Bashe si kijana machachari bali kijana anayeweza kutumika kama nepi na yeyote mwenye nazo. Ni aibu.
 
membe ni mnafiki,muongo,hana uwezo wa kuongoza,kigeugeu,mtupu kichwani,hatutaki kiongozi anayetishia watu kuwa 2016 watakimbilia kenya,,wenzie mwakyembe na sitta kimya,lowasa go,edo nenda,lwaiganan jembe mwanaume wa kuchukua maamuzi magumu,nenda lowasa kiboko ya wanafiki wakubwa kama membe
 
Mkuu Shyrose Banji na Ruth Msafiri ni bidhaa zinazolipa mbaya, mtaji walionao unauzika vizuri kwa wazee!!

Wakiwezeshwa wanaweza na mkono mtu haulambwi.....
Sio wachoyo!!

Mkuu hao wanajua kutoa huduma ya VIP level!!



Lakini SHYROSE BHANJI hajawahi kuchaguliwa na CCM; UBUNGE wa EA alioupata ni kwasababu ya CHADEMA bila CHADEMA asingekuwa MBUNGE na ANAJUA FIKA

Sasa kwanini SHY anajiabisha ndani ya CCM na Wanajua fika hawatamchagua YEYE...

RUTH MSAFIRI alikuwa MKALI kweli BUNGENI kaangushwa kwenye kura za awali za CCM sidhani wana chochote tena
 
ccm wana mambo!siasa zao zinafurahisha sana bt nampongeza membe kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa na kwakweli kukaa kwake kimya kumemwongezea credit.
 
CCM ni chama kinachobagua bado wanawake
na wapiga kura wao wakuu ni wanawake
kwao gender balance sio tija
tutasemaje ni chama chenye usawa?
kwanini wanahubiri sera za usawa wakati usawa kwao ni ndoto?
Si kwamba CCM inabagua wanawake ila huwezi kuchaguliwa bila kiwango cha kutosha cha rushwa sasa wnawake wamezoea kuhongwa si kuhonga hivyo mchezounawawia vigumu. Nawashangaa sana wanasema sijui furani jembe sijui huyu kashindwa hiyo ingekuwa vema kama ingeandikwa hivi WAFUATAO NDIO WALIOONGOZA KWA VIWANGO VYA RUSHWA NEC
1 Wasira Stephen (waziri aliyewahi kupatikana na hatia ya rushwa)
2 Makamba Januari
3 Nchemba Mwigulu
..
..
..
Mkama alitoa rushwa kidogo kuliko vijana wake kina Shigela, Makamba nk ndiyo maana wakamzidi kura, si suala la kukubalika na kutokubalika ni RUSHWA tu ndiyo inayoshinda uchaguzi CCM
 
membe ni mnafiki,muongo,hana uwezo wa kuongoza,kigeugeu,mtupu kichwani,hatutaki kiongozi anayetishia watu kuwa 2016 watakimbilia kenya,,wenzie mwakyembe na sitta kimya,lowasa go,edo nenda,lwaiganan jembe mwanaume wa kuchukua maamuzi magumu,nenda lowasa kiboko ya wanafiki wakubwa kama membe

Je,mmekubali kutumika?kiasi cha kujitoa ufaham?ktk siasa zenye tija ni kujenga hoja na kwakweli hutawaliwa na fikra huru,bt kwa mwelekeo huu wa siasa za majitaka hamtofika mbali na mtaishia kuangukia pua.
 
membe ni mnafiki,muongo,hana uwezo wa kuongoza,kigeugeu,mtupu kichwani,hatutaki kiongozi anayetishia watu kuwa 2016 watakimbilia kenya,,wenzie mwakyembe na sitta kimya,lowasa go,edo nenda,lwaiganan jembe mwanaume wa kuchukua maamuzi magumu,nenda lowasa kiboko ya wanafiki wakubwa kama membe

Hakika Lowassa ni mwanaume wa kuchukua maamuzi magumu na mifano iko wazi. Michache kati ya hiyo ni hii:

1. Aliingiza nchi gizani kwa tamaa ya utajiri binafsi na familia yake. Mkataba ule wa Richmond mpaka leo umeiweka nchi kitanzini.
2. Bila aibu wala kupepesa jicho alidai rushwa ya dola milioni 2 kwa muwekezaji aliyetaka kununua NIC.
3. Alichukua maamuzi ya kukatiza makataba wa Dawasa na Bywater na baadae kuliingiza taifa katika hasara ya dola 11 milioni za legal fees walizogawana na Mkono.
3. Alipora viwanja na kuzua migogoro ya double allocation wakati ule akiwa waziri wa Ardhi.
4. Aliiba fedha za maafa kwa waathirka wa mafuriko ya Lindi na Mtwara mwaka 1990 wakati ule akiwa waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu akihusika na majanga.
5. Kwa kukosa upeo na kwa maslahi madogo ya kiimani aliingiza nchi katika makubaliano na dhehebu moja la dini huku akijua kwamba kufanya hivyo kulikuwa kunatishia umoja na mshikamano wa nchi yetu na kukiuka ukweli kwamba serikali yetu haina muegemeo wa kidini.
6. Alipita nchi nzima na husuasani mikoa ya kusini akimwaga ahadi ya kugawa ng'ombe kwa vikundi vya akina mama na kuwahimiza kujenga mabanda ambayo yamegeuka kuwa sehemu za kulaza mbwa.
7. Amechukua maamuzi magumu ya kuwashuhudia wamasai wenzie na hasa wale wa jimbo aliloliongoza kwa miaka 20 wakigeuka kuwa walinzi wa nyumba za watu na sehemu za maegesho ya magari, na wengine wakiwa wasusi wa nywele za wanawake badala ya kuwaendeleza kielimu na kuwawezesha ili kuwaondolea umaskini na kuondoa jinamizi la ukosefu wa ajira analolipigia kelele.
8. Amechukua maamuzi magumu ya kuhakikisha kwamba wilaya ya Monduli anayoyiongoza kama mbunge kwa miongo zaidi ya miwili inageuka kuwa inayotegemea msaada wa chakula kila mwaka na huku bila aibu akipuuza kauli mbiu ya kilimo kwanza.
9. Maamuzi magumu ya kutumia fedha za walipa kodi kwa kuzua safari za Kamati yake ya ulinzi na mambo ya jje kwa ziara zisizo na tija, huku akisafiri kwa daraja la kwanza na mkewe.
10. Maamuzi magumu ya kuwamaliza wabaya wake kwa kuwashambulia kwa sumu na tindikali ili asiwe na ukosoaji au asiwe na ushindani katika medani ya ksiasa, huku akiwa hajui kwamba Mungu naye atampa udhoofu wa afya ambao unatishia ndoto zake za kuelekea magogoni.

Maskini jasiri Lowassa. Mzee kipenzi cha watu kwa maamuzi magumu.
 
Wajumbe wa NEC:

  1. Wassira Stephen - 2,135
  2. January Makamba - 2,093
  3. Mwigulu Nchemba - 1,967
  4. Shigela Martin - 1,824
  5. Lukuvi William - 1,805
  6. Membe Bernard - 1,455
  7. Mathayo David - 1,414
  8. Msome Jackson - 1,207
  9. Mukama Wilson - 1,174
  10. Mukangara Fenella - 984

Hesabu za kura hapo zimekaaje hapo wadau maana wajumbe waliohudhuria ni 2300 hivi sasa sijui kura ilikuaje maana nikijumlisha hapo inakuja jumla ya wapiga kura ni 16058 (walipiga kura kwa style gani hapa
 
Nafikiri tiangalie tunamtaka kiongozi wa aina gani na atatumika kwa Faida ya nani.
 
ccm wana mambo!siasa zao zinafurahisha sana bt nampongeza membe kwa kuonesha ukomavu wa kisiasa na kwakweli kukaa kwake kimya kumemwongezea credit.

Leo katika pita pita yangu maeneo ya Dodoma Hotel, St. Gaspar na maeneo ya Club 84 hali ya unyonge imetawala katika kambi ya mafisadi. Nilimsikia mjumbe mmoja wa Nec toka mkoa mpya wa Simiyu akisema kwamba walikosea kumuacha Mwenyekiti akiacha wagombea kujieleza maana hilo ndilo lililomjenga Membe. Akasema wasipokuwa makini mwaka 2015 wataachwa wanashangaa hivi hivi.
 
Back
Top Bottom