Jadason Monga
JF-Expert Member
- Aug 5, 2019
- 366
- 347
Bongo bila Kiki hutoki chezea press wewe
Kila mtu anao upeo wake wa kuelewa maana ya matukio kama hayo.Kwani haya mauupuzi wanayofanya si wanatupa taarifa kabla. Na kama walikuwa mipango watupe taarifa ila sio hizi drama za kibashite.
Huwezi kuwaponda wasaidizi wa rais kwa kigezo cha picha na maoni ambayo hujui kama na wao wanayo au hawana.Nadhani umesahau usemi mmoja muhimu sana, kuwa....;
".......yaonekanayo kwa macho na kusikika kwa masikio na kushikika kwa mikono, ndiyo yanayodhihiri yaliyojificha kwenye vungu za mioyo ya mtu/muhusika/wahusika.....ukipenda sema.... kwenye paper plans zao.......!!"
Ndo kusema, huwa hatutolei maoni yaliyojificha kwenye vungu za mioyo ya watu bali yale yaliyowazi na yanayoyatendeka na kuonekana pamoja na kusikika na yale yanayoshikika!!
Kweli unataka asubiri ambayo hayaonekani, kusikika ama kushikika ndiyo aseme/aandike?..
You are not serious wewe, umekosa hoja kabisa ukaamua utetee kivyovyote tu,......right?
Well; suppose, wawe hawana/hayapo maana wewe umeandika kana kwamba yapo ila hawayatoi tu na badala yake wanayatoa yaliyo ya hovyo na dhaifu hata kusababisha watu wahoji ubunifu na umakini wao hawa viongozi.....!!
Sasa na wewe, ukiulizwa....kama hayapo je......utajibuje?
Acha utoto mkuu. Jenga hoja kabla ya kukimbilia matusi ya mitaani.Na wewe ni msengerema kama wao
Lini kunguru kucheza na njiwa? Haitatokea! Birds of the same feather fly together. Hao wanaruka! Waziri siku tatu analala analala wanakojenga daraja. Labda mnyapara! Hata site engineer halali huko. Asubuhi akikuta makosa, ukuta unapigwa chini bila kinyongo. Kiroho safi! Kama ni rahisi rais kupiga pushup mteule wake kabakiwa na nini? Like son like father!hatutakaa tupate majibu ya matatizo hayo kutoka hao wteuliwa kwa kua ushamba bado unawasumbua licha ya wengine kusomea nje, tunayo majibu ya matatizo yote tena yanatatuliwa kwa gharama nafuu sana ila jiwe anapenda kuimbiwa nyimbo za mapambio
Yule chiziUmemsahau Yule Walu Walu RC wa Mbeya
Hiyo namba mbili penye sana,hata zile kesi za wanaume kushitaki kwa wakwe wamenyimwa unyumba kwishney!siku hz wife akizingua una act umenuna tu ila moyoni uo saafi maana unapata fursa za kwenda kugegeda michepuko na machangu hadi akikaa sawa wewe umeshampita kwa magoli mengi tu!Eti makonda anataka kupambana na malaya, malaya wanafanya kazi kubwa sana ambazo hata Serikali haiziwezi kwa mfano
1. Kuzuia wanafunzi kupewa mimba
2. Kuzuia migogoro katika jamii kutokana na ugoni
3. Kuzuia magonjwa yatokanayo na ngono kwenda kwenye familia
N.k.
Hiyo biashara ipo miaka na miaka hata Mungu alishindwa kuizuia itakuwa yeye
I wish ungeongea hayo huko Bweranyange (Karagwe) kubeza waziri kubeba gunia ndo ungejua wanyambo wakoje. Huyo ni mtoto wao amefanya kile amekuwa akifanya, huo uwaziri ni majaaliwa tuu.Hawa ndio wasaidizi wa rais
Na Thadei Ole Mushi.
Picha ya Kwanza ni mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda akili yake na Nguvu zake zote kwa sasa ameziwekeza kwenye kuhakikisha wanaume wa Dar wanasajili ndoa zao. Kwake hili ni kipaumbele kuliko.
1. Kuumiza kichwa ni namna gani atalifanya Jiji la Daresalam Liongoze kwa Usafi Hata East Africa tu.
2. Kupunguza mlundikano wa machinga pembezoni mwa barabara za maeneo kama Mbagala, Tegeta, Gongolamboto nakwingineko. Hivi siku magari yetu yakifeli breki itakuwaje?, lakini kama haitoshi, utakuta vyungu vya chips vinachemka katikati ya dimbwi la watu katika maeneo haya......
3. Kuliko kutengeneza fursa za vijana kujiajiri, jiji la Dar es salaam ni jiji la kimkakati ambalo lina kila kitu katika kuongeza ajira kilichokosekana ni mipango tu.
4. Kuliko kupandisha Ufaulu wa Shule za Mkoa huu na kushika hata nafasi ya kwanza ni nini hakipo Dar cha kuwezesha taaluma kupanda?
5. Kuliko kuendelea kubuni mbinu na mikakati ya kupunguza Msongamano wa magari jiji la Dar.
6. Ni makampuni mangapi ya njee aliyowahi kufanya nayo mazungumzo kuja kuangalia Fursa Dar na kuwekeza?
Matatizo ya Dar ni mengi mno ila Mkuu wa Mkoa kaona hili la Vyeti vya Ndoa ndio la msingi kuliko vyote. Hizi ndizo akili zinazomzunguka Rais wetu John Pombe Magufuli.
Unamwona huyo aliyebeba gunia la kahawa hapo? Huyo ni Waziri wa Viwanda na Biashara. Hii ndio kazi yake ya kwanza anayoitambulisha kwa jamii toka ateuliwe. Anaitwa Innocent Bushungwa.
Nimejiuliza huyu waziri hii ndio kazi aliyotakiwa kuifanya ya kwenda kuwa kibega wa Magunia ya kahawa? Kwa nini hawajifunzi toka kwa watangulizi wao waliotumbuliwa?
Ni mabadiliko gani ameyafanya toka aingie hapo wizarani? Ameshakutana kwa vikao Mara ngapi na wizara ya Kilimo kwa ajili ya kutatua tatizo la Pamba ambayo Ipo kwenye Maghala hadi sasa? Ameshawaza nini kuhusu Korosho itakayovunwa Mwakani? Ameshafanya presentation ya Miradi mingapi kuhusu kujenga viwanda vipya vitakavyomgusa mkulima moja kwa moja? Kwa style hii ya kubeba Magunia Kweli Tutaweza kuwapita Kenya kwa viwanda na biashara? Hii itakuwa ni ndoto ya mchana.
Hawa ndio wasaidizi wa Rais...
Picha ya Tatu ni Juma Aweso akiwa anachochea baiskeli yenye madumu ya maji. Picha hii sitaizungumzia kwa Leo kwa maana kwa kuendesha tu baiskeli maji yanatiririka kila mahali nchini.....
Badala ya kuwaza kuendesha baiskeli yenye madumu KM kibao kufuata maji angeliwaza maji kuwafuata watu majumbani kwao. Anachekelea kuendesha Baiskeli kutafuta maji kwake hii Si Kero na ni kitu cha kuenzi...... Tafiti ya mwisho ya Twaweza kuhusu upatikanaji wa maji umebainisha kuwa asilimia 57 ya wa Tanzania hufuata maji njee ya KM 3 toka anapoishi hadi kwenye Maji. Na Tanzania ndio inayoongoza kwa kuwa na vyanzo Vingi vya maji East Africa......
Hawa wote ni vijana, si Hawa tu wapo wengi wa style hii plus hao wanaotaka kudunga watu sindano za Ukichaa. Najiuliza hivi kwa nini hatuwazi vitu vikubwa? Unajaribu mambo makubwa ukishindwa unasaidiwa? Hakuna ubunifu wowote unaonyeshwa na Hawa vijana.
Wakati watu wakiendelea Kumshangaa Makonda hebu chunguzeni na hao wengine nini wanakifanya? Wana mipango, wana mikakati, wanajua shida za Wanaowaongoza?
Naamini Bado kuna akili nyingi za Rais zipo mtaani zinapaswa kusogezwa kwenye timu yake....
Ole Mushi
0712702602
View attachment 1180431View attachment 1180433View attachment 1180434
Mkuu, unatafuta picha za hao waheshimiwa halafu unaandika uzi!. Kazi nyepesi sana hiyo.
Unajuaje kama hayo unayotaka wayafikirie kama kwa sasa hayapo katika mikakati yao ya kikazi?.
Au labda ulitaka kila wakifanya jambo fulani wakutafute na kukueleza?. Kuandika uzi humu jukwaani ni kazi nyepesi, kuvaa viatu vya hao viongozi sio kazi nyepesi.
Kila siku mnaibiwa nyinyi tu kura, hamuoni kuwa tatizo lipo kwenu?.Hiyo kazi sio ngumu kama unavyotaka tuamini, iwapo ingekuwa ngumu hivyo tusingeona wizi wa kura ili wakae madarakani. Labda ugumu wa hiyo kazi ni kutenda haki.
Kila siku mnaibiwa nyinyi tu kura, hamuoni kuwa tatizo lipo kwenu?.
Hamuoni kama ni kisingizio cha walioshindwa upande wenu kuwa na hoja ya nyinyi kuwasiliza ili waendelee kubakia na uhalali wa kuwa viongozi wenu?.
Palikuwa na jamaa kazini kwetu ambaye kikazi alikuwa amepangwa sehemu ya majimaji na topetope hivi, sasa yeye akitaka kwenda kumtoa pesa ya chapuchapu tajiri yetu basi anachofanya ni kupaka matope nguo zake na kujimwagia maji nguo zake halafu anachomoka moja kwa moja mpaka ofisini kwa bosi na bila kupepesa yeye hapo anatoa shida yake na haulizwi swali zaidi ya kupewa kiasi alichoomba, huyu mwingine mwenye project zisizoisha na kuwa na mwisho chanya nafikiri yeye ana maono na vision ya mbali kuliko sisi tunavyoona, hebu tujaribu kufikiria kidogo kabla ya kubeza je hapa Dar wapiga kura wengi ni jinsia gani?....kazi kwenu huko Kawe!