Hawa ndio wasaidizi wa Rais

Remote

Remote

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2011
Messages
18,101
Points
2,000
Remote

Remote

JF-Expert Member
Joined May 20, 2011
18,101 2,000
Hawa ndio wasaidizi wa rais

Na Thadei Ole Mushi.

Picha ya Kwanza ni mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh Paul Makonda akili yake na Nguvu zake zote kwa sasa ameziwekeza kwenye kuhakikisha wanaume wa Dar wanasajili ndoa zao. Kwake hili ni kipaumbele kuliko.

1. Kuumiza kichwa ni namna gani atalifanya Jiji la Daresalam Liongoze kwa Usafi Hata East Africa tu.

2. Kupunguza mlundikano wa machinga pembezoni mwa barabara za maeneo kama Mbagala, Tegeta, Gongolamboto nakwingineko. Hivi siku magari yetu yakifeli breki itakuwaje?, lakini kama haitoshi, utakuta vyungu vya chips vinachemka katikati ya dimbwi la watu katika maeneo haya......

3. Kuliko kutengeneza fursa za vijana kujiajiri, jiji la Dar es salaam ni jiji la kimkakati ambalo lina kila kitu katika kuongeza ajira kilichokosekana ni mipango tu.

4. Kuliko kupandisha Ufaulu wa Shule za Mkoa huu na kushika hata nafasi ya kwanza ni nini hakipo Dar cha kuwezesha taaluma kupanda?

5. Kuliko kuendelea kubuni mbinu na mikakati ya kupunguza Msongamano wa magari jiji la Dar.

6. Ni makampuni mangapi ya njee aliyowahi kufanya nayo mazungumzo kuja kuangalia Fursa Dar na kuwekeza?

Matatizo ya Dar ni mengi mno ila Mkuu wa Mkoa kaona hili la Vyeti vya Ndoa ndio la msingi kuliko vyote. Hizi ndizo akili zinazomzunguka Rais wetu John Pombe Magufuli.

Unamwona huyo aliyebeba gunia la kahawa hapo? Huyo ni Waziri wa Viwanda na Biashara. Hii ndio kazi yake ya kwanza anayoitambulisha kwa jamii toka ateuliwe. Anaitwa Innocent Bushungwa.

Nimejiuliza huyu waziri hii ndio kazi aliyotakiwa kuifanya ya kwenda kuwa kibega wa Magunia ya kahawa? Kwa nini hawajifunzi toka kwa watangulizi wao waliotumbuliwa?

Ni mabadiliko gani ameyafanya toka aingie hapo wizarani? Ameshakutana kwa vikao Mara ngapi na wizara ya Kilimo kwa ajili ya kutatua tatizo la Pamba ambayo Ipo kwenye Maghala hadi sasa? Ameshawaza nini kuhusu Korosho itakayovunwa Mwakani? Ameshafanya presentation ya Miradi mingapi kuhusu kujenga viwanda vipya vitakavyomgusa mkulima moja kwa moja? Kwa style hii ya kubeba Magunia Kweli Tutaweza kuwapita Kenya kwa viwanda na biashara? Hii itakuwa ni ndoto ya mchana.

Hawa ndio wasaidizi wa Rais...

Picha ya Tatu ni Juma Aweso akiwa anachochea baiskeli yenye madumu ya maji. Picha hii sitaizungumzia kwa Leo kwa maana kwa kuendesha tu baiskeli maji yanatiririka kila mahali nchini.....

Badala ya kuwaza kuendesha baiskeli yenye madumu KM kibao kufuata maji angeliwaza maji kuwafuata watu majumbani kwao. Anachekelea kuendesha Baiskeli kutafuta maji kwake hii Si Kero na ni kitu cha kuenzi...... Tafiti ya mwisho ya Twaweza kuhusu upatikanaji wa maji umebainisha kuwa asilimia 57 ya wa Tanzania hufuata maji njee ya KM 3 toka anapoishi hadi kwenye Maji. Na Tanzania ndio inayoongoza kwa kuwa na vyanzo Vingi vya maji East Africa......

Hawa wote ni vijana, si Hawa tu wapo wengi wa style hii plus hao wanaotaka kudunga watu sindano za Ukichaa. Najiuliza hivi kwa nini hatuwazi vitu vikubwa? Unajaribu mambo makubwa ukishindwa unasaidiwa? Hakuna ubunifu wowote unaonyeshwa na Hawa vijana.

Wakati watu wakiendelea Kumshangaa Makonda hebu chunguzeni na hao wengine nini wanakifanya? Wana mipango, wana mikakati, wanajua shida za Wanaowaongoza?

Naamini Bado kuna akili nyingi za Rais zipo mtaani zinapaswa kusogezwa kwenye timu yake....
Ole Mushi
0712702602
fb_img_1565702348518-jpeg.1180431
fb_img_1565702355433-jpeg.1180433
fb_img_1565702364082-jpeg.1180434
 
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2013
Messages
4,883
Points
2,000
Gullam

Gullam

JF-Expert Member
Joined Dec 1, 2013
4,883 2,000
Duh, kweli tuna kazi sana vijana. Sana huyo Aweso yeye kazi kugombana na wakandarasi wa maji. Wakati matatizo ya kuchelewesha miradi ni ya wizara yenyewe. Ole Mushi nimekuelewa kongore!
 
B

bababikko

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Messages
2,271
Points
2,000
B

bababikko

JF-Expert Member
Joined Apr 2, 2012
2,271 2,000
Hatutakaa tupate majibu ya matatizo hayo kutoka hao wteuliwa kwa kua ushamba bado unawasumbua licha ya wengine kusomea nje, tunayo majibu ya matatizo yote tena yanatatuliwa kwa gharama nafuu sana ila jiwe anapenda kuimbiwa nyimbo za mapambio
 
Nemo Judex

Nemo Judex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2014
Messages
2,998
Points
2,000
Nemo Judex

Nemo Judex

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2014
2,998 2,000
Hii point namba mbili ni ya kuiangalia kwa makini sana, Kuanzia Tegeta hadi kwenda Bunju kuna s
Msongamano sana wa watu wanaofanya biashara hasa nyakati za usiku pembezoni mwa barabara hasa katika vituo
 
VAPS

VAPS

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2012
Messages
2,729
Points
2,000
VAPS

VAPS

JF-Expert Member
Joined Jul 10, 2012
2,729 2,000
Duh, kweli tuna kazi sana vijana. Sana huyo Aweso yeye kazi kugombana na wakandarasi wa maji. Wakati matatizo ya kuchelewesha miradi ni ya wizara yenyewe. Ole Mushi nimekuelewa kongore!
Hivi sasa kuna urasimu na kudai comm kwa nguvu, usipoeleweka, kasoro ndogo ya maelekezo na kujadiliana inakuwa kesi na usumbufu wa ajabu malipo. Wakandarasi wengi wa serikali wanalia kucheleweshewa malipo.
 
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2015
Messages
26,788
Points
2,000
MKWEPA KODI

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2015
26,788 2,000
Eti makonda anataka kupambana na malaya, malaya wanafanya kazi kubwa sana ambazo hata Serikali haiziwezi kwa mfano
1. Kuzuia wanafunzi kupewa mimba
2. Kuzuia migogoro katika jamii kutokana na ugoni
3. Kuzuia magonjwa yatokanayo na ngono kwenda kwenye familia
N.k.
Hiyo biashara ipo miaka na miaka hata Mungu alishindwa kuizuia itakuwa yeye
 
N

needeseela

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2014
Messages
1,602
Points
1,500
N

needeseela

JF-Expert Member
Joined Feb 13, 2014
1,602 1,500
Duh, kweli tuna kazi sana vijana. Sana huyo Aweso yeye kazi kugombana na wakandarasi wa maji. Wakati matatizo ya kuchelewesha miradi ni ya wizara yenyewe. Ole Mushi nimekuelewa kongore!
Tatizo la kuacha akili iliyosababisha matatizo kutatua matatizo yatakanayo na hizo akili
 
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Messages
5,016
Points
2,000
Kurunzi

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2009
5,016 2,000
Eti makonda anataka kupambana na malaya, malaya wanafanya kazi kubwa sana ambazo hata Serikali haiziwezi kwa mfano
1. Kuzuia wanafunzi kupewa mimba
2. Kuzuia migogoro katika jamii kutokana na ugoni
3. Kuzuia magonjwa yatokanayo na ngono kwenda kwenye familia
N.k.
Hiyo biashara ipo miaka na miaka hata Mungu alishindwa kuizuia itakuwa yeye
Hapa umewaza sana
 
P

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2015
Messages
10,235
Points
2,000
P

Phillipo Bukililo

JF-Expert Member
Joined Dec 29, 2015
10,235 2,000
Mkuu, unatafuta picha za hao waheshimiwa halafu unaandika uzi!. Kazi nyepesi sana hiyo.

Unajuaje kama hayo unayotaka wayafikirie kama kwa sasa hayapo katika mikakati yao ya kikazi?.

Au labda ulitaka kila wakifanya jambo fulani wakutafute na kukueleza?. Kuandika uzi humu jukwaani ni kazi nyepesi, kuvaa viatu vya hao viongozi sio kazi nyepesi.
 
M

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2018
Messages
3,584
Points
2,000
M

Mfiaukweli

JF-Expert Member
Joined Aug 30, 2018
3,584 2,000
Mkuu, unatafuta picha za hao waheshimiwa halafu unaandika uzi!. Kazi nyepesi sana hiyo.

Unajuaje kama hayo unayotaka wayafikirie kama kwa sasa hayapo katika mikakati yao ya kikazi?.

Au labda ulitaka kila wakifanya jambo fulani wakutafute na kukueleza?. Kuandika uzi humu jukwaani ni kazi nyepesi, kuvaa viatu vya hao viongozi sio kazi nyepesi.
Tutolee uzwazwa wako hapa. Kuna mtu gani mwenye akili ya kufanya mipango madhubuti na akaona kubeba gunia ndio kuonyesha umahiri wa kazi za uwaziri?
 

Forum statistics

Threads 1,326,261
Members 509,458
Posts 32,216,041
Top