Hawa kweli Wanazuoni walio huru. Je, wanazuoni hawa si wahafidhina wa itikadi ngumu

Mkunazi Njiwa

JF-Expert Member
Apr 22, 2023
5,510
4,818
Wamejitokeza WENGINE kuipinga serikali ya awamu ya 6 kwa kuchukua uamuzi wa kukaa mezani na DP WORLD wa Dubai.

Imekuwa ni "bandika bandua"....wakitoka hawa ,wanaingia wengine.

Tujiandae kuwaona wengi sana wakijitokeza.

WANAZUONI
Wameandika mengi sana katika kuupinga mkataba huu....

Yako yanayofikirisha na kushtua mathalani :

Kuitaja MAREKANI na pia kuitaja CHINA.....

Katika kukosoa kwao wanaonesha kutowaamini taifa la marekani ambao ni miongoni mwa wadau wetu wa maendeleo.

Wanaonesha kuwa inawezekana hawa DP WORLD wa Dubai ni mikono tu....nyuma yao wako wamarekani....hizi ni fikra za ajabu sana.

NCHI YETU HAIFUNGAMANI NA UPANDE WOWOTE

Sera yetu ya nje inabaki kuwa wazi kuwa sisi ni marafiki wa mataifa yote huru na hatufungamani na falsafa za kibeberu wala kikomunisti.

Hili la hawa wanazuoni kuwa na fikra za kihafidhina ni za kutilia mashaka sana.

CHINA
Sisi ni marafiki wa nchi ya China ,sikutegemea kuwaona hawa WANAZUONI wakijaribu kuonesha kuwa China ni bora kiuwekezaji zaidi ya nchi ya Marekani..hapa pananipa mashaka sana juu ya hawa wajiitao wanazuoni kwani mwekezaji aliyekuja ni kutoka Dubai na wala si Marekani wala China.

DUBAI
Wanazuoni "wanaidogosha" "kampuni ya kimataifa ya DP WORLD kuwa inatoka katika jiji la Dubai ambalo ni umoja wa falme za kiarabu kwa kusema kuwa umoja huo uko chini ya "KOO" za familia ya wachache...wakimaanisha kuwa hizo falme si za kidemokrasia....hapa wanajichanganya kwa kutuonesha kuwa wanapenda DEMOKRASIA na si tawala si kiimla.

Nilitegemea kwa kuonesha kwao kupenda demokrasia wasingeupinga utawala wa awamu ya 6 chini ya Rais mh.DrSSH....wako kinyume na kuonesha sura zao kuwa WANAJICHANGANYA kwa wanayosimamia.

Misri
Misri ni marafiki zetu ,chini ya utawala wa awamu ya 5 kampuni ya nchini kwao (Arab contractors) ilipata zabuni ya kujenga bwawa la ufuaji umeme la mwalimu Nyerere.
Misri ni rafiki wa nchi ya Marekani ambayo hawa wanazuoni wameonesha "kuikosoa" sana katika hotuba yao.

Kuna maneno yanasemwa nchi ya Misri pamoja na kuwa na Rais aliyechaguliwa ila inaendeshwa "kijeshi"..hapa panaleta tafakuri ya kukosekana UTOFAUTI wowote ule kati ya nchi INAYOONGOZWA "KIJESHI"(MISRI) NA NCHI ILIYO CHINI YA UTAWALA WA UKOO MMOJA(UAE).
Kwa hili ,hoja yao dhidi ya wawekezaji hawa DP WORLD inakosa mashiko ya kukamatia!!.

MSAMBWENI
Wanazuoni hawa wako msambweni kihoja. Binafsi ninawakumbusha wanazuoni hawa kuwa ,taifa letu si la KIBEBERU ,KIBEPARI wala KIKOMUNISTI.....usalama wa Tanzania ni kwanza "awali kulii"....hatufungamani na upande wowote. Tanzania ni TAIFA LA KIJAMAA(UJAMAA WA KIAFRIKA).

Ninaamini watajitokeza wengi...makundi mengi kuupinga uamuzi wa serikali yetu adhimu kukaa mezani na kuingia mkataba na DP WORLD katika kuendesha bandari zetu.

Serikali yetu adhimu isikate tamaa ,huku mitaani wako watanzania wengi ambao wameanza kuuelewa ukweli dhidi ya upotoshwaji ambao ni kama vile unaratibiwa vyema(systematically) na si tu wanapinga uwekezaji huu bali kuupinga utawala wa awamu ya 6 ndani ya CCM na nje ya CCM huku kwetu bara na kule visiwani kwa kutafuta visingizo kila wanapoona "fursa" ya kufanya hivyo.

Watanzania wanaelewa haya yafuatayo:

Bandari zetu zinakwenda kuondoa kudorora na kusuasua kupakia na kushusha mizigo.

Haiwezekani bandari yetu iweze kuchukua siku mpaka 20 kupakia/kupakua mizigo katika meli ilihali bandari ya nchi jirani ,Mombasa inachukua hadi siku 3 tu.

Watanzania wamechoshwa na STATUS QUO" isiyotupeleka mbele tutakako na ndio maana ninapowaona hawa " wanazuoni " ninapata hisia hasi kuwa huwenda WANATUMIKIA MASLAHI YA WAFAIDIKAJI WANAOSABABISHA BANDARI ISIPIGE HATUA AMA HATA NA MAKUNDI HASI YA NJE YA NCHI.

Binafsi nimefarijika kusikia kuwa DP WORLD watafanya haya:-

- Hawatowafukuza wafanyakazi waliopo bandarini

- Watawaendeleza kielimu

- Hawatoajiri raia wa kigeni

Nimesikia pia hawatojihusisha na USALAMA wa bandari zetu na MAMLAKA YA BANDARI (TPA) itabaki na "berth 8-11"...hapa ni kuwa WANAZUONI wajue kuwa TPA ipo.

Mkunazi Njiwa,

Matema Kyela

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Kwajinsi unavyoikampeni na namna ulivyoandika hakika wewe ni mnufaika na ni miungona mwa mliepelekwa Dubai kuhongwa uuzwaji wa bandari yetu.
Kwa taarifa yenu sauti ya wengi na saiti za sirini mioyoni mwenu ni sauti ya Mungu, sasa endelea kushindana na Mungu utaepata matokeo yake
 
Usinitishie Mwenyezi Mungu mimi...

Ninamuamini ,ninamuishi kupitia imani yangu "jiwe" juu yake...imani inayohusisha AMANI ,USALAMA NA USTAWI WA NCHI NIISHIYO...

Mimi si mnufaika wa chochote cha mkataba....ila nitanufaika kama mtanzania kuona taifa langu kupitia bandari kupitia hawa DP WORLD linapata pato nusu ya bajeti ya taifa kila "fiscal year"...

Chengine mimi ni mnufaika wa kuiona Tanzania inabaki ikiwa moja na yenye mshikamano kwani nje ya hayo kuna:-
-Uzanzibari na uzanzibara

-UGAIDI WA KIDINI(wanaweza kutumia dini yoyote uijuayo)
-UGAIDI WA KIKOMUNISTI

-UKABILA ,UKANDA NA UDINI...

Usipoelewa haya wewe baba Jayaron utakuwa ni "MBUBU"

#SiempreJMT
#MamaAnaupigaMwingi

Hakuna mwizi anajitaja hata siku moja... hata wezi wa awamu zilizopita hawakukiri wanauza nchi ila mwishoni walikiri so siku shangai ni mmoja wao
 
Argumentum ad hominem....

Unaongea usichokuwa na uthibitisho nacho...

Vijana tunaanza kuziishi "mentalities za hovyo"?!!

Yaani mtu haongelei jambo kwa UZURI NA WEMA mpaka awe pale amelamba fedha kama dalali vile na kupata maslahi binafsi ?!!!duuh

Yaani hatuna tena ALTRUISTIC BEHAVIOR?!!!Gooosh

#DoNotDoHarm
#SiempreJMT

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Argumentum ad hominem....

Unaongea usichokuwa na uthibitisho nacho...

Vijana tunaanza kuziishi "mentalities za hovyo"?!!

Yaani mtu haongelei jambo kwa UZURI NA WEMA mpaka awe pale amelamba fedha kama dalali vile na kupata maslahi binafsi ?!!!duuh

Yaani hatuna tena ALTRUISTIC BEHAVIOR?!!!Gooosh

#DoNotDoHarm
#SiempreJMT

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
Wezi haoooooooo
 
Hamna mtanzania anapinga uwekezaji wenye tija kwa TAIFA!

Hofu ya watanzania inatokana na vipengele vya kimkataba ikiwemo ukomo wa mkataba wenyewe, na kama nia ni njema kwanini bandari za Zanzibar zipo excluded!

Uliyoyaeleza sidhani kama ni maoni ya wananchi
 
Back
Top Bottom