Hawa hapa maadui wa Taifa la Tanzania

MzeeKipusa

JF-Expert Member
Feb 10, 2023
2,706
4,923
Enzi zetu wakati nakuwa mambo hayakuwa kama ilivyo sasa.

Nakumbuka, nilikuwa nikishuhudia viongozi wengi sana wakistaafu huku wakiwa hawana miliki ya vitu vingi.

Nionavyo Mimi, naona tayari MEZA imeishapinduliwa.

Maadui wakubwa wa Tanzania ni:

1. UJINGA (Enzi zetu hii ilikua kwà WANANCHI/ RAIA)
2. MARADHI (yalikuwa kwà Watumishi na Wafanyakazi)
3. UMASIKINI (ulikuwa kwà Viongozi)

Nasema meza imepinduliwa kwasababu, hivi sasa. UJINGA umewatawala viongozi walio wengi. Na wengi wao wanajidanganya kuhamasisha ujenzi wa mashule kwà ajili ya Wananchi wakati kiukweli kwasasa Wananchi hawana shida kabisa ni hizo shule zao (Kwani wameishagundua haziwasaidii watoto wao zaidi ya kuwatia UMASIKINI/wanaona bora wakae na watoto wao wasiwapeleke shule kupoteza muda na mwisho kuambulia Kukosa Kazi/ajira)

VIONGOZI wengi wamejirundikia mali za wizi na kuwafanya Wananchi/ Raia kuwa na UMASIKINI uliokithiri.

USHAURI: Ndugu zangu, hatuwezi kamwe kuwaondoa hawa maadui kwà kuipindua meza tutakua tunajidanga sisi wenyewe tu.

Ni vyema tukajitafakari sana kwà dhati ya mioyo yetu na kwà kukubaliana na ukweli. Tusiyakwepe matatizo tuliyonayo kwà kuyapaka rangi ya lips.

Tujitahidi sana kuzitumia experiences zetu, lessons zetu, study zetu na wisdoms zetu vizuri.

Mimi Mzee Kipusa, kwà dhati ya moyo wangu nina amini ya kwamba taifa letu haliwezi kamwe kuendelea na kuwa lenye Mafanikio kama tukiruhusu Milango na Madirisha yetu kuwa yamefungwa muda wote. Ni lazima tukubaliane kuifungua either Milango au Madirisha (kimojawapo). Hapa ndipo tutaweza kupiga hatua za kweli na zenye uhakika.
 
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
😁
🤯
 
Maadui wa taifa ni.
Mwigulu
Makamba
Nape
Hawa jamaa walianzia mbali kabla ya kuwa WAJINGA.

walianza kufanya mambo ya kipuuzi , wakagraduate , kisha wakaanza kufanya mambo ya kinafki,...napo wakagraduate tena wote wakawa mabest students...then wakaendelea kufanya mambo ya kishenzi...Mwigulu akawa best student , na sasa wapo katika kufanya mambo ya kijinga na kipumbavu.

Kupitisha/ kusign mikataba kama vichaa ( Unaambiwa jamaa kwenye mikataba hawanaga muda hata wa kusoma yaliyomo ndani...wanaangalia kichwa cha habari tu na Kiasi cha hela walichoandaliwa kupewa kama hongo basi...Wana sign shaaashaaaa...Imeisha hiyo dadekii )


Note: Siku hizi mtu akifanya mambo ya kipuuzi kwenye Taifa letu...lazima atrend. Nafikiri makosa yetu pia ni kukubaliana na mawazo au entertainments/vituko vya watu wapuuzi.
 
6982430F-83C8-4805-BF1F-845CCE723A7D.jpeg
 
DAH KUMAMAK* INATIA HASIRA KINOMA
Wakati mwingine nikifikiria sana ...naona sisi vijana (sio wote) tukawa na makosa pia.

1. Baadhi ya Viongozi ni wazazi wetu ; Huenda sisi ndio tuliwashawishi wawe majizi / majangili ....baada ya wao kutupeleka Nchi za nje kusoma / kupata exposure. Tukawaletea habari za namna ya kuihujumu Serikali ( kujilimbikizia mali ili tuishi kifahari) #familia bora #mboga saba

2. Vijana ni walinzi na waongozaji wa Taifa. Tumekua kama mazezeta , tunaona mambo hayako Sawa..lakini tumekalia tu kulalamika. Hivi kwanini tusiingie barabarani tukawatia hasara hawa viongozi ili wajifunze...halafu tukaanza kujenga UPYA kwà Umoja? Tunafeli wapi?
 
Back
Top Bottom