Hapo kwenye bold umesema kweli ila dah hakuna namna acha tutumie hivyo hivyo tu naona sasa unasoma fresh hapa asubuhi ulikua mzito sanaMtandao sio powa, utajisumbua tu ! Mabando yao pia hayaeleweki, mb zinaisha tu yani bila kujua umetumiaje ? Hawa jamaa ni matapeli..... kitambo sana niliwatemea mbali
Sema walikuja fresh na speed ya kasi mno, nasikia wali pigwa spana watulie kidogo.Hao wajinga wakati wanakuja around 2013/2014 walikuwa wanavimba kwamba wanakuja kuleta mapinduzi ya vifurushi vya mtandao, hasa Internet. Sijui ni mwanasiasa gani aliwaleta hao Vietnamese. 😁
Mara tunaunga mtandao vijiji vyote TZ, Internet itakuwa bei kiduchu. Mara ziii... jero unapewa 200MB. 😁
Hii bongo jau sana aisee.
Sema walikuja fresh na speed ya kasi mno, nasikia wali pigwa spana watulie kidogo.
Hata halopesa yao ni ya kiwaki siku hizi.
Walikuja na ile 1500 unlimited usiku mzima, 500 gb 1 ka sio mbili.Lazima watakuwa walibanwa, voda mtandao wa wakubwa nchi hii. Dizaini ni kama walikuwa wanatishia sana hasa ile sera yao ya huduma bei kiduchu. Wangemharibia voda ambayo kimsingi ni biashara ya wakubwa nchi hii.
Tandao zito kama lami.😠😠Hivi ni mimi tu huku nilipo au na wengine huko mlipo mnakipata hiki kisanga ninachokipitia mimi? Yaan mtandao mzito sio poa. Halotel shida nini Wazee?