Hatuwezi kukimbia JF

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kuna wanapropaganda kutoka sijui kwa mafisadi au CCM yenyewe ambao wameingia humu kwa kazi au minajili wanayoijua wenyewe, wanaeneza Uongo unaopaswa kukataliwa na kila mwana JF

kwanza walianza na kudai kuwa kuna baadhi ya member wanao uwezo wa kumwamrisha Moderator ahamishe Thread au afute post ya mtu kwa maelekezo ya wenye blog jambo ambalo limethibitishwa siyo kweli!

wakaja na nyingine kwamba JF ni mtandao unaomilikiwa na chama cha siasa cha CHADEMA. Kwa bahati mbaya kwao imethibitika siyo kweli,ingawa inawezekana kabisa wanaoiendesha JF wana mahusiano na baadhi ya viongozi wa CHADEMA

Sasa kwa hili wanalotamba nalo na kujigamba kwamba wamewatimua wapinzani ndani JF halipaswi kuachwa lipite bila ya kuwaeleza ukweli. Kwanza JF siyo kilinge cha wapinzani au CCM bali ni jukwaa la jamii kujadili mambo yao

Ndani ya JF hakujadiliwi siasa peke yake bali kila kitu, hadi watafuta wachumba wamo humu,waswalihina na walokole huwakosi. Tatizo liliopo inawezekana wanaodhani kwamba JF ni kilinge cha upinzani ni wale ambao wakifungua main board ya JF wanaingia kwenye jukwaa la siasa moja kwa moja, wakati kuna majukwaa mengine mengi yanayojadili mambo mbalimbali ya kijamii.

Kwa taarifa yao hapa ni jukwaa la jamii ambalo hakuna mipaka ya kutoa mawazo au maoni (siyo ujinga) bila ya mipaka ya kirasimu ya watawala wetu.kwa hiyo hapa ndiyo jukwaa pekee wananchi wanao uwezo wa kuikosoa serikali yao bila ya kuhofu kushughulikiwa na serikali. kwa maana hiyo hatukimbii wala kuhama JF. Tutabanana hapahapa!
 
Kwa maana hiyo hatukimbii wala kuhama JF. [COLOR="Red" said:
Tutabanana hapahapa![/COLOR]


Utaweza? Kubanana kwataka ubavu yakhe !!!!! Pili itabidi uvae koti la mvua na mask. Wengine huwa hawakogi
 
Utaweza? Kubanana kwataka ubavu yakhe !!!!! Pili itabidi uvae koti la mvua na mask. Wengine huwa hawakogi


Mtaka cha uvunguni sharti ainame yakhe,nitavumilia bora jahazi lifike Pwani!
 
Back
Top Bottom