Hatutaruhusu kura yetu kuibiwa Igunga - CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatutaruhusu kura yetu kuibiwa Igunga - CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by saliel, Aug 23, 2011.

 1. saliel

  saliel Member

  #1
  Aug 23, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 82
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema kitasimamia na kuhakikisha kuwa hakuna kura yake inayoibiwa katijka uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Igunga, mkoani Tabora hakitaliachia Jimbo la Igunga, mkoani Tabora kufanyika Oktoba 2, mwaka huuu.
  Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini (Chadema), Godbles Lema, alitoa kauli hiyo mjini Singida juzi jioni alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya kituo cha zamani cha mabasi.
  Lema ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, alifafanua kuwa licha ya CCM kutamba kwamba jimbo hilo hawatalipoteza, lakini hawana jipya la kuwaeleza wananchi wa Igunga kutokana na ukali wa maisha unaowakabili watanzania hivi sasa.
  Hata hivyo, Lema aliyefuatana na wabunge wa Viti Maalum wa Chadema, Chiku Abwao Mkoa wa Iringa na Regia Mtema (Morogoro) wakitokea Igunga, aliweka bayana kwamba ni ukweli usiopingika kwamba jimbo hilo ni lazima liende Chadema.
  Alidai kuwa pamoja na mbinu chafu zinazotarajiwa kufanywa na chama tawala, lakini alisema chama chake kina uhakika wa kulichukua Jimbo la Igunga lililoachwa wazi na Rostam Azizi aliyejiuzulu kwa maelezo kuwa amechoshwa na siasa uchwara ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
  “Ndugu zangu wana Singida wabunge wote wa Chadema mara tu baada ya kumalizika kwa kikao cha Bunge la bajeti, tutakwenda majimboni kwanza kusalimia na kisha baadaye wote tutaelekeza nguvu zetu kwenye uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga na hakuna kura itakayoibiwa safari hii mpaka tutatangazwa kulinyakua jimbo hilo,” alisisitiza Lema huku akishangiliwa na wananchi waliokuwa wakimsikiliza.
  Abwao alisema mara baada ya kuingia mkoani Singida wakitokea Igunga alisikitishwa sana baada ya kuwakuta wanawake wa mjini Singida wakiteseka kutafuta maji ambayo ni kazi ya siku nzima.
  “Hivi ni kweli wanasingida mmeridhika muishi maisha haya mnayoishi?” alihoji Abwao na kuongeza: “Wenzenu wa Iringa maji tunamwaga mpaka vyooni maji ni ya kumwaga…kwa sababu Iringa tumeamka hatutaki kudanganywa.”
  Kwa upande wake, Mtema alitumia fursa hiyo kuwataka Watanzania kutodanganyika kutoa kura zao kwa kupewa kanga, fulana, kofia, fedha taslimu na hata vyakula.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #2
  Aug 23, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  strategies za kuhakikisha hawaibiwi ni zipi? maana si kuishia kuzungumza tu majukwaani. au huo ni mkakati wa ndani hautajwi tajwi hovyo! anyway all in all kazi kubwa lazima ifanyike kukabiliana na DED mteule wa rais na manyang'au wengine mawakala wa uchakachuaji
   
 3. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #3
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,248
  Likes Received: 3,836
  Trophy Points: 280
  Kama hilo litafanyiwa kazi basi ushindi mweupee!!
   
 4. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #4
  Aug 23, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  wae makini sana na FF mana nasikia nae kaenda huko kuiba kura
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Aug 23, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />
  mbinu zitakazotumika zitakuwa kama zile zilizotumika Tarime kwenye uchaguzi mdogo, kila kituo cha kupigia kura kunakuwa na mawakala watatu, hakuna anayemjua mwenzake. Hata hivyo kazi itakuwa rahisi kwa chadema, kwani wasimamizi watakuwa waalimu, ambao hawatapenda kumchakachua mwalimu mwenzao
   
 6. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #6
  Aug 24, 2011
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  CCM wizi upo kwenye dam. Wataiba tu, na mi nashauri tujipange sasa kuchukua nchi kanzia Igunga.
   
 7. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #7
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Wananchi wa Igunga ndio hao siku Rostam alipobwaga manyanga walilia na kusaga meno na kuzirai. Nina imani watachagua magamba tena
   
 8. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #8
  Aug 24, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Nasikia wale walioangua kilio walikuwa wamelipwa.
   
 9. SHERRIF ARPAIO

  SHERRIF ARPAIO JF-Expert Member

  #9
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 25, 2010
  Messages: 7,081
  Likes Received: 1,818
  Trophy Points: 280
  Are u serious mkuu? Mtu alipwe kwaajili ya kulia na kuzirai?? Basi ina maana kwenye misiba mingi siku hizi ukiona waliaji ni wengi kumbe wengine wamelipwa!!! Ha!
   
 10. M

  Malova JF-Expert Member

  #10
  Aug 24, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  kikubwa cha kuangalia ni uhesabuji na ukaguzi wa program zinazotumika na NEC. ninavyohisi kama programmer what greencard does is; if x =greenbalots, and y=cdmbalots, then greenbalots= x + 0.6cdm balots and
  cdm balots=0.4 y. Ndugu zanguni sasa hivi codes ndizo zinazotuua kwa sababu you see what you input but results from the system are different from the manual ones
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  si kila kitu kinapaswa kuanikwa lakini njia moja wapo ya kusimamia ni kuwafanya wana Igunga wajue umhimu wa kura zao, kuwa na wakala kila kituo, kuto kula chochote hovyo ili kupunguza kwenda chooni..
   
 12. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #12
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  pesa kitu kingine kaka cha msingi kila mmoja awe mlizi wa mwenzake...
   
 13. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #13
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  kwa kura za jimbo moja kushi kuzilinda ni upumbavu hata kama watakuwa na program ya aina yoyote...
   
 14. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #14
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  ndiyo maana haonekani sikuhizi kumbe yuko kwenye michakato, safari hii itakula kwake
   
 15. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #15
  Aug 24, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,180
  Likes Received: 1,182
  Trophy Points: 280
  Cdm waamke sasa ccm walishaanza mbinu chafu tangu zamani
   
 16. O

  Omr JF-Expert Member

  #16
  Aug 24, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Lema ametoa uhakika kuwa hakuna kura itakayo ibwa,Ina maana CCM wakishinda mtakubali matokeo? Kama mnasema watu wa igunga walilipwa kulia na kuzirai sasa kutakuwa na ugumu gani kuwalipa wachague CCM? Naona nyie CHADEMA kila siku zinavyo kwenda mnazidi kuwa matahira.
   
 17. h

  hoyce JF-Expert Member

  #17
  Aug 24, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 1,119
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  <br />
  <br />Wewe hujui kwamba kuna vikundi vya kulia na kugalagala misibani? Umechelewa. Kimoja kipo hapo mburahati. Hata waombolezaji wa kawaida wafikapo karibu na msiba ndo hujipanga na kuambizana 'tuanze' hapo ndo kilio cha kusaga meno huanza.
  Unadhani kama hawakukodia mafuso yaliyoletwa na bashe kutola Nzege yakiwa na wafuati kibao yalikuwa ya nini?
   
 18. p

  propagandist Member

  #18
  Aug 24, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 93
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mbona mmeanza kulia lia mapema kabla hata mtanange wa igunga haujaanza mnatafuta huruma ya wapiga kura wa igunga, kuweni kama cuf ngangari, cdm acheni kulalama!
   
 19. G

  Godwine JF-Expert Member

  #19
  Aug 24, 2011
  Joined: Jan 15, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  hivi vyama vimeshakagua daftari la majina ya wapiga kura...........mimi nilipata kuliona hivi karibuni mchezo mchafu umetendeka mule yani majina hayaendani na namba ya shahada za watu na mengine hayapo nadhani chadema,ccm na cuf lazima mmoja atakuwa anahujumu wenzake
   
 20. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #20
  Aug 24, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Komaeni mpaka dakika ya mwisho.
   
Loading...