Hatutarudi nyuma – Sheikh Farid | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatutarudi nyuma – Sheikh Farid

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kakke, May 30, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  May 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on May 30, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Kiongozi wa Maimamu Zanzibar, Farid Hadi Ahmed akiongea na waumini katika msikiti wa Mbuyuni Zanzibar jana baada ya sala ya alaasiri

  JUMUIYA ya Mihadhara ya kiislamu (Uamsho) imetoa msimamo mkali shidi ya Serikali ikisema kuwa haitarudi nyuma katika kudai uhuru wa Zanzibar.

  Wakizungumza katika msikiti wa Mbuyuni uliopo eneo la Darajani mjini Zanzibar, viongozi wa Uamsho wamewataka Wazanzibari kutolegezamsimamo wao hata kama jeshi la polisi limezingira mji wao.

  “Umoja wetu ndiyo utakaotukombolea nchi yetu, msikubali kuyumbishwa na kitu chochoe ili kulegeza msimamo wetu. Jambo moja tu, ni mpaka kieleweke.

  Bila hivyo hakuna jeshi, hakuna polisi atakaye tuyumbisha” alisema Sheikh Mussa Juma wa msikiti huo na kuitikiwa na wafuasi waliokuwa wamefurika katika msikiti huo “ndiyooooo!”

  Wafuasi hao walikuwa wameshikilia karatasi zilizoandikwa “hatuutaki muungano, tunaitaka Zanzibar yetu”.

  Naye Sheikh Mussa Juma aliyekuwa amekamatwa na jeshi la polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana aliwapongeza wanachi waliotokana kuandaana akisema kuwa hawatarudi nyuma, Tunawashukuru Wazanzibari kwa sababu mmeonyeshwa kutotaka kutawaliwa” alisema na kuwauliza wafuasi hao “mko tayari” nao wakijibu “Tuko tayariii”

  Naye Sheikh Farid Hadi Ahmed alisema kuwa kundi hilo linafuata taratibu hivyo halipaswi kulaumiwa kwa kufanya vurugu. Aliwataka pia Wazanzibari kutogawanyika kwa vyama vya siasa,“Muone katika silaha kubwa wanayotumia maadui ni kutugawa kivyama na kikabila au kirangu, inasikitisha sana.”

  Huku akinukuu Katiba ya Zanzibar ibara ya 23 Farid alisema kuwa kila Mzanzibari anapaswa kuhifadhi mamlaka na uhuru ya Zanzibar.

  Aliwahamasisha wafuasi hao kuonyesha mabango waliyokuwa wameshikilia na kumtaka mkuu wa jeshi la polisi kutambua hitaji kubwa la Wazanzibari.

  “Hebu mwonyesheni IGP mlichonacho….. mnautaka muungano hamuutaki? (wote wakajibu) “hatuutaki!).

  Huku akitoa mifano, Farid aliendelea kusema kuwa kilichopo ni wimbi la Wazanzibari kudai nchi yao.

  Alisema kuwa kama vile maji ambayo yakizibwa katika njia yake husambaa mitaani, hivyo ndivyo Wazanzibari wanavyosambaa mitaani kudai nchi yao.

  Alitetea kitendo cha jumuiyta hiyo kuandamana akisema kuwa si kosa kisheria kutembea barabara.

  “Kwani mtu akitembea kwenye nchi yake anatembea kwa kibali? Sisi tumeamua kutembea… waliokuja na wake zao wametemebea na Mwenyezi Mungu kajalia tumetembea kwa furaha yote. Mbona timu zinafanya mazoezi, zinachukua vibali, watu wanakwenda hitimani wanapewa vibali?” alihoji.

  Faridi alitangaza siku ya Mei 26 kuwa ni ya maandamano kwa Wazanzibari na kuwataka wanajeshi wa Kizanzibari kujiandaa kuwaunga mkono katika maandamano hayo.

  Huku akikwepa lawama kwa kundi hilo kwamba limekuwa likichoma na kuharibu makanisa, Sheikh Farid aliwalaani watu wanaounganisha kundi hilo na tuhuma hizo, “Tunamwambia IGP kamishina hana uwezo hana uwezo. Wanajeshi tunao…. Vikosi vina watu 8000 waambie wajindae wasibebe silaha ni ndugu zetu… waje wakae barabarani wala sisi hatuhitaji ulinzi” alisema na kuongeza,

  “Lakini tuna wasi wasi na hawa wanaolipua makanisa na sisi tunawalaani vibaya, hawa tunaamini ndiyo wale wale waliokuwa wakisimama na kutukana matusi, tena wana visu, wana nondo, wana pesa Mheshimiwa IGP waambie wakupe rekodi.”alisema Farid.

  Licha ya Waziri katika Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Mohammed Aboud kukemea mihadhara hiyo, jeshi la polisi halikuthubutu kuingilia mkutano huo.

  Magari yaliyosheheni askari polisi yalionekana yakipita mbali na eneo hilo bila kuwabughudhi.

 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  May 30, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Jamani ndugu zangu Wazanzibar nawatatakia kila la kheri. Ni ukweli kwamba hata sisi Watanganyika tulio wengi hatutaki huu muungano na kwa hakika tunawaunga mkono. Kila la kheri na muwe makini na CCM kwani watafanya juu chini kuwagawa ili msifanikiwe.
   
 3. W

  We know next JF-Expert Member

  #3
  May 30, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Sasa naona JK kalikoroga na Tume yake ya Katiba.
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  May 30, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Is this Sheikh still at large?
   
 5. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #5
  May 30, 2012
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mei 26 ipi tena? watasubiri hadi mwakani au? Aneway, mi naunga mkono, but siwaungi mkono kushambulia makanisa...
   
 6. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #6
  May 30, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=1][/h]Posted on May 30, 2012 by zanzibaryetu
  [​IMG]Kiongozi wa Maimamu Zanzibar, Farid Hadi Ahmed akiongea na waumini katika msikiti wa Mbuyuni Zanzibar jana baada ya sala ya alaasiri

  JUMUIYA ya Mihadhara ya kiislamu (Uamsho) imetoa msimamo mkali shidi ya Serikali ikisema kuwa haitarudi nyuma katika kudai uhuru wa Zanzibar.

  Wakizungumza katika msikiti wa Mbuyuni uliopo eneo la Darajani mjini Zanzibar, viongozi wa Uamsho wamewataka Wazanzibari kutolegezamsimamo wao hata kama jeshi la polisi limezingira mji wao.

  “Umoja wetu ndiyo utakaotukombolea nchi yetu, msikubali kuyumbishwa na kitu chochoe ili kulegeza msimamo wetu. Jambo moja tu, ni mpaka kieleweke.

  Bila hivyo hakuna jeshi, hakuna polisi atakaye tuyumbisha” alisema Sheikh Mussa Juma wa msikiti huo na kuitikiwa na wafuasi waliokuwa wamefurika katika msikiti huo “ndiyooooo!”

  Wafuasi hao walikuwa wameshikilia karatasi zilizoandikwa “hatuutaki muungano, tunaitaka Zanzibar yetu”.

  Naye Sheikh Mussa Juma aliyekuwa amekamatwa na jeshi la polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana aliwapongeza wanachi waliotokana kuandaana akisema kuwa hawatarudi nyuma, Tunawashukuru Wazanzibari kwa sababu mmeonyeshwa kutotaka kutawaliwa” alisema na kuwauliza wafuasi hao “mko tayari” nao wakijibu “Tuko tayariii”

  Naye Sheikh Farid Hadi Ahmed alisema kuwa kundi hilo linafuata taratibu hivyo halipaswi kulaumiwa kwa kufanya vurugu. Aliwataka pia Wazanzibari kutogawanyika kwa vyama vya siasa,“Muone katika silaha kubwa wanayotumia maadui ni kutugawa kivyama na kikabila au kirangu, inasikitisha sana.”

  Huku akinukuu Katiba ya Zanzibar ibara ya 23 Farid alisema kuwa kila Mzanzibari anapaswa kuhifadhi mamlaka na uhuru ya Zanzibar.

  Aliwahamasisha wafuasi hao kuonyesha mabango waliyokuwa wameshikilia na kumtaka mkuu wa jeshi la polisi kutambua hitaji kubwa la Wazanzibari.

  “Hebu mwonyesheni IGP mlichonacho….. mnautaka muungano hamuutaki? (wote wakajibu) “hatuutaki!).

  Huku akitoa mifano, Farid aliendelea kusema kuwa kilichopo ni wimbi la Wazanzibari kudai nchi yao.

  Alisema kuwa kama vile maji ambayo yakizibwa katika njia yake husambaa mitaani, hivyo ndivyo Wazanzibari wanavyosambaa mitaani kudai nchi yao.

  Alitetea kitendo cha jumuiyta hiyo kuandamana akisema kuwa si kosa kisheria kutembea barabara.

  “Kwani mtu akitembea kwenye nchi yake anatembea kwa kibali? Sisi tumeamua kutembea… waliokuja na wake zao wametemebea na Mwenyezi Mungu kajalia tumetembea kwa furaha yote. Mbona timu zinafanya mazoezi, zinachukua vibali, watu wanakwenda hitimani wanapewa vibali?” alihoji.

  Faridi alitangaza siku ya Mei 26 kuwa ni ya maandamano kwa Wazanzibari na kuwataka wanajeshi wa Kizanzibari kujiandaa kuwaunga mkono katika maandamano hayo.

  Huku akikwepa lawama kwa kundi hilo kwamba limekuwa likichoma na kuharibu makanisa, Sheikh Farid aliwalaani watu wanaounganisha kundi hilo na tuhuma hizo, “Tunamwambia IGP kamishina hana uwezo hana uwezo. Wanajeshi tunao…. Vikosi vina watu 8000 waambie wajindae wasibebe silaha ni ndugu zetu… waje wakae barabarani wala sisi hatuhitaji ulinzi” alisema na kuongeza,

  “Lakini tuna wasi wasi na hawa wanaolipua makanisa na sisi tunawalaani vibaya, hawa tunaamini ndiyo wale wale waliokuwa wakisimama na kutukana matusi, tena wana visu, wana nondo, wana pesa Mheshimiwa IGP waambie wakupe rekodi.”alisema Farid.

  Licha ya Waziri katika Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Mohammed Aboud kukemea mihadhara hiyo, jeshi la polisi halikuthubutu kuingilia mkutano huo.

  Magari yaliyosheheni askari polisi yalionekana yakipita mbali na eneo hilo bila kuwabughudhi.
   
 7. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #7
  May 30, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Kipere kimepata mkunaji!
   
 8. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #8
  May 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Sasa tayari,,watawala wafungue macho!
   
 9. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #9
  May 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  eti nchi yetu..nchi gani ina mikoa miwili tu...fanyeni kazi wazenji nyie acheni kutafuta umaarufu usiokua na mbele wala nyuma
   
 10. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #10
  May 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kila la kheli na ndoto na fikra za uonevu sijui wakipata uhuru itakuwa kwa wabara waliozaliwa huko watakuwaje..
   
 11. h

  harakati83 Member

  #11
  May 30, 2012
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 61
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kila la heri wakuu
   
 12. The Listener

  The Listener JF-Expert Member

  #12
  May 30, 2012
  Joined: Feb 5, 2012
  Messages: 977
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Nahisi kuna haja ya kumuuliza swali moja kubwa huyu Bwana Mkubwa - ANATAKA UHURU UPI AMBAO AMEUKOSA? Wakati mwingine ajue fika kwamba si yeye pekee atakayeathirika na misimamo hii ila jamii kwa ujumla. Kama yeye anadai kuwa hatarudi nyuma kamwe, kwa upande mwingine Polisi na majeshi wao huwa ni mbel kwa mbele sasa asije sema kwamba hakuonywa. Mimi ni Mtanganyika na kinachoniuma ni kwamba huyu Bwana na wafuasi wake anadai kuwa Wabara ndo tunaowanyima uhuru katika Muungano.
   
 13. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #13
  May 30, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,313
  Likes Received: 5,604
  Trophy Points: 280
  Muungano umpasukie yeye na Magamba kimfie yeye!duu atakuwa amevunja rekodi 3 moja dr anazo 5,Muungano na chama chake!!!
   
 14. M

  Makupa JF-Expert Member

  #14
  May 30, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,742
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  huu usemi kuwa mpaka kieleweke wa kulaumiwa ni cdm
   
 15. b

  blue arrow JF-Expert Member

  #15
  May 30, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 271
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siyo kutafuta uhuru ila tu baadhi ya wazanzibari wanafanya uvunjivu wa amani jambo ambalo hatari kwa maisha ya wapenda amani:lock1:
   
 16. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #16
  May 30, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  nyerere alisema awazanzibar wakikataa muungano sita wapiga mabomuuu sasa tanganyika mbona munasahau raisi wenu maneno yaka Karume muungano ni kama kotiiii likikubana unalivuwa
   
 17. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #17
  May 30, 2012
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,520
  Likes Received: 1,691
  Trophy Points: 280
  Inlalilahi........
   
 18. Tetty

  Tetty JF-Expert Member

  #18
  May 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25,559
  Likes Received: 16,530
  Trophy Points: 280
  Hivi jamani muungano unazungumziwa kwenye misikiti? Tuwe watu wakutambua kuwa unapoanzisha cheche ya moto anaglia usiwe wa kwanza kuungua.Kama Zanzibar siwaichukue?Inatusaidia nini Wadanganyika?Siyo tu waongee kuvunja muungano na hao WaZanzibar walioko Huku Danganyika waanze kuondoka si basi kila mtu abaki na chake?Tumewachoka bwana anzeni tu!
   
 19. H

  Hatutaki Muungano Member

  #19
  May 30, 2012
  Joined: May 30, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unanifurahisha sana kutambua kuwa nchi yetu ni ndogo kiasi cha kuidharau, kwanini usiwaambie na wenzako kama JK na wengine wanaoing'ang'ania watuachie sisi tumeridhika na hichi kijinchi chetu tuacheni tubanane wenyewe sasa hatutaki tena kubanwabanwa na watu wenye kutupangia yakufanya......ilhali wao wenyewe hawajui kujipangia - hii akili au matope?
   
 20. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #20
  May 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Ushauri wangu kwa watu wa dini, na kwa hapa Muamsho
  "Ya Ngoswe wamwachie Ngoswe".Si busara kwao kutumia
  majukwaa ya kidini kufanya madai ya kisiasa. Madhara yake
  tunayaona. Ijapokuwa nia yao ni nzuri na madai yao ni halali,
  lakini jukwaa wanalotumia ni baya. Wanaweza kuifikisha
  Zanzibar pabaya. Kama wana madai ya kisiasa, waunde chama
  cha siasa chenyelengo la kuvunja Muunganona watapata wafuasi
  wengi kutoka pande zote, kuliko kutumia dini ambapo matokeo
  yake ni kuzipaka dini matope na kueneza chuki miongoni mwa
  wafuasi wa dini mbali mbali.

  BUSARA INAHITAJIKA ZAIDI KULIKO JAZBA
   
Loading...