Hatutaki longolongo za CCM na Rais Samia

Kwa kifupi hao tumeishawachoka maana tokea tunaanza mfumo wa vyama vingi ndo wagombea. Kwa kifupi Upinzani hakuna Tz kwa sasa labda 2030 napo mkijipanga vizuri. Imagine Tundu Lisu, Lema walikimbia walisema serikali ya JPM inawatishia usalama haya JPM hayupo mbona hawarudi wanapigia kelele huko
Hakuna serikali ya jpm wala ya ccm,serikali iliyotaka na inayoangamiza upinzani na viongozi wao ni ya Tanzania.Kisheria serikali zote duniani hulinda watu wake ila hapa kwetu ni tofauti kabisa.
Ndiyo maana tunahitaji Katiba mpya kuirudisha serikali mikononi mwa wananchi.
 
MiCCM inawachezea sharubu viongozi wa Upinzani wakijua connection between them na wanachama wao ni dhaifu haina mashiko ,hadi leo CHADEMA hawajaweza kuprove kama wanachama wao wapo tayari kusikiliza amri zao kama ilivyokuwa kwenye CUF ya Maalim Seif.

Unaita watu waandamane wewe unaenda kujificha kwenye balozi za nchi za nje tiketi mkononi ,hivi mwanachama atakufahamu vipi wewe kiongozi ,ndio pale inaposemwa wanachama wanatumika kama ngazi,

Hata hivyo wapo akina Mbowe huenda wakaweza kuipata connection ya wananchi na kuanza kurindima tena. Lakini kwa hii itikadi ya kijiditali naona kama ni udhaifu.

Tume huru ya uchaguzi ni haki ya wananchi ni lazima iwepo na ipingwe kwa hali na mali kwa watu wake kuchaguliwa na Raisi hivyo kuaminisha kuwa waliokuwemo ndani ya Tume ni watumwa na watumwa hufuata amri na humtumikia bwana wao tu.
 
Kwani kwenye CCM ukimuondoa Samia nani mwingine anaweza kuwa Rais?Kwani wote waliomo kwenye mfumo tunawajua.
2015 ulimtegemea kama JPM angepeperusha bendera ndani ya CCM. CCM ni taasisi hivi vyama vingine ni one man show. ukimtoa ZZK ACT chama kinakufa siku hiyo hiyo. Ukimtoa Mbowe CDM chama kinakufa kinapotea
 
2015 ulimtegemea kama JPM angepeperusha bendera ndani ya CCM. CCM ni taasisi hivi vyama vingine ni one man show. ukimtoa ZZK ACT chama kinakufa siku hiyo hiyo. Ukimtoa Mbowe CDM chama kinakufa kinapotea
Ukimtoa ZZK chama kinakufa ? mi nafikiri ingependeza ungelisema ukileta tume huru CCM inapotea kusikojulikana.
CCM haipo kwenye mioyo ya wananchi walio wengi ,CCM imechomeka wakuu kwenye mihimili ya Nchi tu,ndio ukaiona ipo hai, lakini ukae na kuelewa CCM ni maiti anaekwenda ,ufahamu wabunge wa CCM hawapo kihalali ,hiki Chama hakina mbunge aliechaguliwa kiuhalali na ndio ukaona wabunge wake hawaonekani onekani,wamekuwa watu wa kujifichaficha hawana mahusiano mazuri na raia walio mitaani na vijijini.
 
Back
Top Bottom