Hatupingi kipengele cha maadili-Nnauye

Hatupingi kipengele cha maadili-Nnauye

bulama

JF-Expert Member
Joined
Dec 13, 2012
Posts
568
Reaction score
138
Dar es Salaam. Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema hakipingi kuwepo kwa kipengele cha maadili ya viongozi ndani ya Katiba Mpya na kwamba kinapendekeza itungwe sheria itakayosimamia kifungu hicho.

Kauli hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Katibu Mwenezi wa CCM, Nape Nnauye, alipokuwa akizungumza katika Baraza la Kitaasisi la Katiba la UVCCM kuhusu masuala kadhaa yaliyoibuka kwenye mapendekezo ya rasimu mpya ya Katiba.

Nnauye alisema tangu mwanzo, CCM ilipendekeza kuwepo kwa kifungu kitakachoshughulikia maadili ya viongozi. Wanajanvi na wansheria, nataka kuuliza hivi sharia huwa zinatungwa kutokana na nini? Hasa za nchi.
 
Utetezi mwingine inabidi ujitoe ufahamu kidogo , hivi mapendekezo ya Rasimu ya katiba si maoni ya wananchi kwa ujumla?
 
---- huyu .... Anataka kutubambikia mawazo ya ki CCM siku hizi hapendwi mtu.... lengo ondoa CCM miaka hamsini hamna kitu weka chama nyingine ... na wengine wafaidi.... sio kila wakati CCM tuu
 
Yeye anafikiri ni ya wale aliowatukana kuwa wanakaribia kufa. Ninacho shangaa wakati maoni yanakusanywa je, ccm walibaguliwa? maana naona wanapinga kila kitukilichom kwenye rasimu hiyo. Kumbe ccm siyo wananchi wa nchi hii
Utetezi mwingine inabidi ujitoe ufahamu kidogo , hivi mapendekezo ya Rasimu ya katiba si maoni ya wananchi kwa ujumla?
 
sheria zinatugwa ili kutuongoza,kutukinga na kutoa haki...kwa maana hii kipengele cha maadili ni muhimu na kwenye kipengele hicho kiseme wazi mtu anayekwapua wake za watu hafai kuwa kiongozi.
 
Nape sema wananchi wataamua,sii kusema hatupingi hii sii katiba ya ccm!
 
Jibu ni kuwa sheria Inatungwa kutokana na Katiba.
Sasa wao hawataki Madili ndani ya Katiba, Ila wanataka sheria zake, haya si mazingaombwe.
 
sheria zinatugwa ili kutuongoza,kutukinga na kutoa haki...kwa maana hii kipengele cha maadili ni muhimu na kwenye kipengele hicho kiseme wazi mtu anayekwapua wake za watu hafai kuwa kiongozi.

Muhimu wapi?
Wanachobishania watu ni kuwa MACCM hawataki Maadili ndani ya Katiba na wengine wanataka katiba itamke wazi ni nini maadili yta Taifa na Uongozi, Kama huna hayo wewe hufai kuwa kiongozi, MaCCM wanaogopa. Wanajua ikiwekwa kwenye sheria wanauwezo wa kuichakachua na kuichelewesha, na itachukua mika zaidi ya kumi kufanya mchakato, upembuzi yakinifu na mengineneo kuja kutunga hiyo sheria.
 
Kipengere cha maadili kwa Tanzania ya sasa utakuwa ni kama Sheria kivuli kwani hata vipengele vingi vinavyowabana viongozi hakuna sheria wala mtu wa kuwawajibisha, kuna matukio mangapi yametokea ya Ubadhilifu na Mikataba mibovu ya mali ya umma nk lkn hakuna hatua madhubuti ya kukomesha, ipi ile sheria ya Viongozi kutaja Mali zao....Sheria Kipofu
 
Back
Top Bottom