<br />vizuri mkuu, kwanza hongera kwa kunywa maji mengi kiasi hicho!!!, bali hutakiwi uzidishe lita 3 na nusu kwa siku. kumbuka pombe ni kikojoshi (diuretic) huyalazimisha maji kukimbia nje ya mwili kwa haraka, yaani unapokunywa pombe kikombe kimoja, utaenda kukojowa vikombe viwili, kwahiyo unapungukiwa maji mara 2. utaona mwenyewe ukinywa tu maji, haukawii kwenda kukojowa. kitendo hiki cha kukojowa muda mfupi tu baada ya kunywa kimiminika hupelekea madini na vitamini za mhimu kutoka nje ya mwili na kuandaa ngazi ya ugonjwa fulani huko mbeleni. kumbuka; usizidishe lita tatu na nusu kwa siku na pombe ni kikojoshi(diuretic). tembelea: <u>maajabuyamaji2.artisteer.net</u>
<br />
<br />
Mimi hunywa lita 1.5 ya maji asubuhi nikiamka kabla hats sijapiga mswaki. Hunywa taratibu huku nikiendelea na shughuli zingine kama vile kunyosha nguo, kufagia uwanja n.k. Nikienda ofisini huendelea kunywa maji taratibu kiasi cha lita 1.5 tena. Pamoja na ratiba hiyo, haja kubwa huenda mara moja tu kwa siku yaani asubuhi. Hata hivyo, magonjwa yananisumbua sana hasa kichwa. Je, ratiba hiyo inaweza kuwa ndiyo sababu ya kuuguaugua hata magonjwa ya tumbo?