Hatuko pokee yetu katika Ulimwengu Huu

Venus Star

JF-Expert Member
Dec 6, 2018
19,230
58,180
Nawasalimia ndungu zangu. Ni mambo mengi nimeyaona kutokana na Tafiti zangu. Kuna msemo unasema penye nia pana njia.

Ninapenda kuongelea mambo mawili ambayo nimekumbana nayo katika pita pita na Tafiti za hapa na pale.
  1. Kuna viumbe vipo na tunaweza kuwsiliana navyo
  2. Majini yapo katika ulimwengu tofauti na wetu
Mwaka jana mwenzi wa sita tukiwa tumeenda kufanya utafiti kwenye kijiji cha Matamba kilichopo karibu na Hifadhi ya Kitulo. Nilikuwa na wenzangu kwenye msitu fulani ulio karibu na kijiji hicho. Tulifunga mahema yetu tayari kwa kuweka kambi.

Usiku ulipoingia tuliwasha moto na tukawa nje ya mahema. Wenzangu walianza kupitiwa na usingizi. Nilisikia sauti ya ajabu ambayo sijawahi kuiona ikitokea umbali kama wa mita 50. Huku mwanga mdogo mdogo ukitokea kwenye sauti hiyo. Kwakuwa maisha yangu nimeyaweka kwenye utafiti, nilichukua tochi na kuanza kunyata kuelekea kwenye sauti.

Nilipokaribia kama mita kumi hivi niliona viumbe wawili wakiwa wamesimama na miguu miwili, macho yao yalikuwa makubwa kiasi na masikio yao ni marefu kidogo kama ya punda. Kwenye mikono yao walikuwa wamishikilia vifaa vifananavyo na simu ya mkononi. Nilijificha kwenye kichaka ili niweze kujua wanafanya nini. Walikuwa wakitoa sauti fulani ambayo kwa kweli sikuielewa.

Walianza kubonyeza bonyeza vifaa walivyonavyo kwenye mikono. Ghafla walitoweka kwenye upeo wa macho yangu. Nilianza kurudi nyuma kwa kunyata nikielekea kwenye hema. Nilipo ondoka kidogo niliona mwanga wablu na kijana ukiwa katika umbo la duara kutokea kwenye eneo walipokuwa wamesimaa hao viumbe ukielekea juu. Niliutazama kwa muda na kisha ulipotelea angani.

Niliporudi tulipokuwa tumekaa kwenye moto. Niliwakuta wenzangu wakiwa wamepiga usingizi. Nikawaamsha ili tuingie ndani ya hema na tulale. Kesho yake niliwasimulia na tukaelekea maeneo walipokuwa wamesimama. Tulikuta mawe madogo madogo yametandazwa chini, maumbo kadhaa niliyatambua maana yalikuwa ni pembe tatu, duara na mengine sikujua maumbo yaKe.

Hii ilinipa kuwaza sana kuwa katika ulimwengu huu kuna viumbe wapo tunaishi nao kutokana na uwezo wa macho yetu hatuwezi kuwaona. Vilevile hatuwezi hata kuona UV light mpaka tutumie vifaa maalumu.

KARIBUNI
 
mkuu mimi naamini unachosema, niliwah kuona lichombo kubwa sana angani ila nilipowaambia wenzangu wakasema Ganja niliyovuta siku hiyo ilikuwa ni ya malawi hivyo niko too high lakini binafsi bado naamini niliona chombo hicho na viumbe viwili mfano wa unavyosema na kile chombo kilikuwa juu yao..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siri nyingi nitazidi kuwaambia wenye kuunganisha dots watanielewa.
 
Tulikuta mawe madogo madogo yametandazwa chini, maumbo kadhaa niliyatambua maana yalikuwa ni pembe tatu, duara na mengine sikujua maumbo yaKe.
Wewe MTAFITI andiko lako linakosa hata picha ya hayo mawe? sitaki kuku-judge ila yawezekana ulikuwa unaota.
 
Naamini yanawezekana lakini tafadhari weka hizo picha za maumbo na mawe ni hakiki yale niliowahi kuyaona.
 
Nawasalimia ndungu zangu. Ni mambo mengi nimeyaona kutokana na Tafiti zangu. Kuna msemo unasema penye nia pana njia.

Ninapenda kuongelea mambo mawili ambayo nimekumbana nayo katika pita pita na Tafiti za hapa na pale.
  1. Kuna viumbe vipo na tunaweza kuwsiliana navyo
  2. Majini yapo katika ulimwengu tofauti na wetu
Mwaka jana mwenzi wa sita tukiwa tumeenda kufanya utafiti kwenye kijiji cha Matamba kilichopo karibu na Hifadhi ya Kitulo. Nilikuwa na wenzangu kwenye msitu fulani ulio karibu na kijiji hicho. Tulifunga mahema yetu tayari kwa kuweka kambi.

Usiku ulipoingia tuliwasha moto na tukawa nje ya mahema. Wenzangu walianza kupitiwa na usingizi. Nilisikia sauti ya ajabu ambayo sijawahi kuiona ikitokea umbali kama wa mita 50. Huku mwanga mdogo mdogo ukitokea kwenye sauti hiyo. Kwakuwa maisha yangu nimeyaweka kwenye utafiti, nilichukua tochi na kuanza kunyata kuelekea kwenye sauti.

Nilipokaribia kama mita kumi hivi niliona viumbe wawili wakiwa wamesimama na miguu miwili, macho yao yalikuwa makubwa kiasi na masikio yao ni marefu kidogo kama ya punda. Kwenye mikono yao walikuwa wamishikilia vifaa vifananavyo na simu ya mkononi. Nilijificha kwenye kichaka ili niweze kujua wanafanya nini. Walikuwa wakitoa sauti fulani ambayo kwa kweli sikuielewa.

Walianza kubonyeza bonyeza vifaa walivyonavyo kwenye mikono. Ghafla walitoweka kwenye upeo wa macho yangu. Nilianza kurudi nyuma kwa kunyata nikielekea kwenye hema. Nilipo ondoka kidogo niliona mwanga wablu na kijana ukiwa katika umbo la duara kutokea kwenye eneo walipokuwa wamesimaa hao viumbe ukielekea juu. Niliutazama kwa muda na kisha ulipotelea angani.

Niliporudi tulipokuwa tumekaa kwenye moto. Niliwakuta wenzangu wakiwa wamepiga usingizi. Nikawaamsha ili tuingie ndani ya hema na tulale. Kesho yake niliwasimulia na tukaelekea maeneo walipokuwa wamesimama. Tulikuta mawe madogo madogo yametandazwa chini, maumbo kadhaa niliyatambua maana yalikuwa ni pembe tatu, duara na mengine sikujua maumbo yaKe.

Hii ilinipa kuwaza sana kuwa katika ulimwengu huu kuna viumbe wapo tunaishi nao kutokana na uwezo wa macho yetu hatuwezi kuwaona. Vilevile hatuwezi hata kuona UV light mpaka tutumie vifaa maalumu.

KARIBUNI
Hahahahah! Hii ni bangi! Kwanza ujue binadamu unaweza kujikuta unaona vitu kama maruweruwe tu kumbe hakuna, unahalucinate.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom