Hatuijengi Tz Kwa Kupiga Kelele! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatuijengi Tz Kwa Kupiga Kelele!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumaku, Jun 2, 2009.

 1. S

  Sumaku Member

  #1
  Jun 2, 2009
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na Andrew Mushi

  MAKALA haya ni mwendelezo wa makala ya wiki iliyopita. Wiki jana nilijaribu kuonyesha kila mmoja wetu alivyo na nafasi kubwa ya kuwa chachu ya maendeleo. Ujumbe muhimu niliojaribu kuujengea hoja ni kuwa, katika sehemu mbali mbali tunamoishi, kuabudu au kufanyia kazi au biashara, kuna mianya na nafasi nyingi zinajitokeza na tukiamua kufungua macho yetu na kuthubutu kuzitumia , basi, mara tutaona mambo yanaanza kujipa. Nikajaribu kutoa mifano michache ya watu waliofanya vitu ambavyo jamii ilifaidi na kustawi kwa vile tu waliamua kujaribu.

  Leo nitajaribu kuongelea nafasi tulio nayo tunapojumuika katika makundi mbali tunayoyaanzisha au tumeanzisha. Lakini, kabla sijasonga mbele niseme kwa nini nimesema hivi. Mara nyingi nimesika watu wakisema nitagombea ubunge na mara chache wanasema watagombea udiwani ili waende bungeni’ wakapige kelele’ ili maendeleo yaje.

  Ni jambo la kusikitisha kuwa tumefikia pahala kuona ili serikali ifanye kitu au maendeleo yaje, ni lazima kupiga kelele. Nafikiri kama jamii huo ni udhaifu.

  Inatakiwa tuelekeze muda mwingi na nguvu zaidi kupangilia mipango thabiti na inayofanana na mahitaji na matatizo yetu, na sio kupigiziana kelele.

  Nimesoma katika barua pepe mtandaoni pale Mtanzania mmoja anaposema ameona jimboni kwake kuna matatizo makubwa sana ya usafiri na anajiandaa kugombea ubunge mwakani ili ‘akawakomboe’ wananchi wa jimboni kwake. Ila nimecheka pale Mtanzania mwingine alipomjibu; “ Wewe kama unataka ubunge, usihangaike kuandaa sera wala habari za madaraja maana hazikupeleki popote.”

  Mtanzania huyo anamshauri mwenzake aandae pilau, kanga, t-shirts na kofia. Hapo ubunge utakuwa wake, ila eti aanze mapema maana mbunge aliyeko sasa kaanza maandalizi toka Krismas ya mwaka jana.

  Mara nyingi tumeshuhudia watu waliojiunga katka makundi mbalimbali na kufanikiwa kuleta mabadiliko makubwa ndani ya jamii. Kikubwa hawakupitia milango ya siasa. Ili nisiongelee mambo ya kusadikika nitatumia mifano hai.

  Mpaka kufikia miaka 15 iliyopita, tatizo la usawa wa kijinsia lilikuwa kubwa sana nchini mwetu. Wanawake walikuwa wana nafasi duni sana. Hali ilikuwa mbaya zaidi pale serikali ilipoanza kutekeleza mpango wa kurekebisha uchumi kwa kufuata masharti waliyoopewa na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), na Benki ya Dunia (WB) kunako mwishoni mwa miaka ya 1980. Kwa kifupi, kina mama waliteseka sana na walikuwa na hali duni maana huduma kama elimu, afya, maji na nyinginezo vilipopewa bajeti ndogo, wao ndio walikuwa waathirika wakuu

  Mwaka 1994 Wakajitokeza Watanzania 12 (wanawake 10 na kina baba 2) wakasema hatuwezi kuacha hali iendelee kuwa mbaya. Wakajiunga wakaanzisha kikundi kilichojiita Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP). Wakasema wanataka kufanya kitu kimoja kitakacholeta mabadiliko makubwa ya kijamii. Wakachagua suala la Upangaji wa Bajeti kwa kuzingatia mahitaji ya makundi mbali mbali ya kijamii.

  Walichomaanisha ni kuwa serikali imezoea kupanga bajeti bila kuzingatia makundi mbalimbali ya kijamii kama vile, kina mama, watoto, walemavu, wazee na vikongwe. Sana sana bajeti inazingatia mahitaji ya kina baba wenye nguvu ambao wakati huo huo hawana mahitaji mengi na majukumu mengi. Kama unabisha niambie kwa nini kila kikicha vilabu vya pombe vinaota kama uyoga na havikosi wateja, ni kina kina nani hao? Jibu unalo!

  Waliona huu ni mlango nzuri wa kuingilia ili kujenga hoja yao na serikali na jamii ikawasikiliza. Wakaweka mikakati yao. Wakaona pa kuanzia ni wizara ya fedha maana wao ndio wanapanga bajeti. Hapa ndio jikoni eti! Hawakukimbilia kuanza na kila wizara au kuinyooshea mkono serikali. Unajua siku zote ili jambo lifanikiwe ni vizuri kuwa na mikakati mizuri na ambayo haiwezi kushindwa kirahisi.

  Taratibu wakaanza kujenga urafiki na mahusiano na watendaji wa wizara ya fedha . Mara ya kwanza wizara ya fedha walipoona hawa kina mama, maana ndio walikuwa wengi na kina baba wachache wanaongelea upangaji bajeti kwa kwa macho ya kijinsia wakawashangaa, kwanza wao sio wataalamu wa bajeti wala fedha, na zaidi wala sio wachumi.

  TGNP hawakukata tama, wakaaza kuwaeleza wanamaanisha nini wanaposema kuna uwezekano wa kupanga bajeti kwa kuzingatia mahitaji ya makundi mbalimbali . Kwa vile walikuwa wanajua wanachokisema na pia kuwaonyesha kwa mifano ni jinsi gani unaweza kuwa na bajeti ya kijinsia serikali ilianza kuwasikiliza.

  Walipopewa mwanya wakautumia vizuri na baadhi ya maafisa wa bajeti wakaonyesha mwitikio chanya. Taratibu bajeti kuu ikaanza kuwa na mwelekeo wa kijinsia. Wizara nyingi tu zikaanza taratibu kuingiza masuala ya kijinsia katika mipango yao. Na kwa mikakati mizuri waliokuwa nayo na mbinu, wakapewa nafasi hata ya kuwapatia mafunzo watendaji serikalini jinsi ya kupanga bajeti na mipango yote ya maendeleo kwa kuzingatia jinsia.

  Baada ya kuona wameanza kusikilizwa na serikali wakawa wanapanua wigo taratibu. Wakawa wanaenda bungeni Dodoma kuwaelimisha wabunge juu ya hoja yao. Pia wakaanza kuwaingizia hii hoja makundi mengine yanayotetea haki za kijamii. Wakaenda mbali zaidi kwa kushawishi uanzishwaji wa mitandao ya kijinsia katika baadhi ya wilaya hapa nchini. Kwa kifupi kila TGNP walichokifanya wamekuwa na mafanikio mazuri sana. Ila kumbuka bango walilolibeba ni bajeti ya kijinsia, basi, hawakubeba kila kitu!

  Kwa wafuatiliaji wa mambo ya maendeleo Tanzania, leo hii kila utakapoenda utasikia watu wanasema jamani tuzingatie jinsia. Kwa kiasi kikubwa ni makundi kama TGNP na wengineo kama TAMWA, WLAC, TAWLA n.k waliopenyeza na kuzengea haya mambo ya jinsia yakawa ajenda ya taifa. Leo kwa kulinganisha na nchi nyingi duniani, Tanzania ni nchi inayojitahidi kupanga mipango yake kwa kuzingatia jinsia. Japo hatujafika lakini dhamira ya dhati toka kwa wanaume na wanawake wa nchi ipo.

  Nataka nirudi kwako ndugu msomaji. Nasema badala ya wote kutaka kukimbilia katika siasa, ambako muda mwingi unatumika katika malumbano , tunaweza tukajiunga katika vikundi pale tunaapoona kuna jambo linatukera mtaani kwetu, kijijini kwetu, wilayani kwetu. Tunaweza tukaanza kuliwekea mikakati ya kulitatua. Sisemi mkimbilie kuanzisha NGOs, maana NGOs nyingi tu hazifanyi chochote mpaka wapate hela ya wafadhili. Hii nchi haiwezi kujengwa na hela zaa wafadhili.

  Sio vizuri kuanza kwa kupiga kelele. Kama ni suala la elimu, mazingira, ajira, afya, usalama mnaweza kuwa na mikakati mizuri sana, na ikaleta mabadiliko makubwa sana. Najua unaweza kusema mipango mingi inakwamishwa na mafisadi waliojichimbia kila mahali, ni kweli, lakini pia hawa mafisadi papa na nyangumi walipata nafasi ya kuota mizizi kwa sababu tulikuwa tumelala usingizi mzito wakati wao wanafanya mipango ya kutuangamiza. Ila tukijipanga vizuri na kujiwekea mikakati mizuri, hakuna cha mapapa wala nyangumi watakaotukwamisha, tutafanikiwa tu!


  amushi1@yahoo.com

  Andrew Mushi anasomea shahada ya PhD katika masuala ya Uchumi na Utawala

  CHANZO:
  kwanzajamii.com
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Inawezekana kweli "Hatuijengi TZ kwa kupiga kelele" tu, mengi zaidi yanahitajika.

  Lakini for sure kwenye ufisadi na uozo kama huo "Kukaa kimya ni kuibomoa TZ" kwa hakika.
   
 3. M

  Mkandara Verified User

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sumaku,
  nampongeza huyu jamaa yetu Andrew Mushi lakini kitu kimoja anakosea sana. Anaposema watu hatuwezi kuijenga Tanzania kwa kupiga Makelele!.. Hili neno makelele kalitumia sehemu nyeti sana kiasi kwamba nashindwa kuelewa anachozungumza...Hivi hayo mashirika au NGOs anazozitolea mfano huwa hazipigi makelele wanapoweka hoja zao mbele iwe bungeni au wizarani? Ni wakati gani madai ya haki ya wananchi au maslahi ya taifa hugeuka kuwa Makelele!..
  Kila mtu anayetaka kuingia Ubunge au Udiwani ni moja ya mjumuiko anaozungumzia sii lazima kila mtu ajiunge na NGO inayowakilisha kundi moja..kwani kujiunga Bungeni kuna tofauti gani na hizo NGOs anazozungumzia

  Haya makelele yanazungumzia hata hizo Jinsia kwa mapana zaidi na kama sii makelele haya hao wanaosifiwa wasingeweza kusimamisha hoja na maombi yao kwani wananchi wasingefahamu umuhimu wa NGO hizo kwa sababu haya yanayoitwa makelele huambatana na dataz zinazotoa ushahidi mkubwa wa waathirika..
  Mtu unaposhindwa kuelewa nguvu ya dola inavyptakiwa kuhimizwa mara nyingi hii lugha ya makelele hutumika. Weusi wa Marekani walipotaka haki zao walizipeleka ktk migomo, makelele kote magazetini, TV na ndipo mwamko mkubwa wa kuunda vyama vinavyopigania haki hizo lakini sii kila mweusi alifungua NGo inayohusiana na haki hizo.
  Tulipopigania Uhuru wetu tulipiga hayo makelele hadi Muingereza akainua mikono kutuwezesha kufungua chama cha siasa nchini..Ideas zote hutokana na hayo makelele kama vile soko la bidhaa hutokana na mazungumzo ya watu. Ubunifu hutokana na mahitaji ya watu na sii kufikiria kitu kichokuwepo..hakuna NGO yoyote iliyofunguliwa kabla ya hayo Makelele isipokuwa zimetokana na makelele..unapokanyagwa ni bora upige uyowe kumtahadharisha aliye kukanyaga kabla hujarusha konde!..
  Hivyo ktk uwakilishi wa makelele hayo ndipo tunapokuta fotauti anazozungumzia..Leo hii siwezi kufungua tena NGO ya jinsia wala hatuihitaji kuwa na mbili au Tatu, to make our voice heard! lakini haina maana sikufikiria swala hilo hata kidogo... makelele yangu ni ishara tosha kwamba maswala ya Jinsia yalikuwa tatizo kubwa nchini..lakini kukutanisha watu mkajipanga na kufungua NGO inahitaji maelewano baina ya wahusika ktk hoja moja, na hata hao waliofungua TGNP hawawezi kupokea sifa zote ama kufikiria wao ni mitume wakati inawezekana kabisa kuwa hiyo Idea wameichukua toka kwa mtu ambaye hakuhusishwa kabisa..Ama Idea nzima imejengwa kama kawa kufunika lengo kubwa la kujinufaisha wao..Tunajua sana kinachofanyika ktk NGOs hizi, mara zote huujilipa wao mishahara mikubwa kutokana na fedha za sadaka au wahisani..Huwezi kukuta wanatoa mitaji au fedha zao wenyewe toka mifukoni mwao bali hutegemea mfuko wa serikali na ajabu kubwa wao kujipa ajira ndani ya NGOs hizi.
  kama kweli hawa watu huwa na nia nzuri kwa nini wao waibakie na kazi zao za zamani (kabla ya kuzaliwa kwa NGO) kisha wakaajiri watu wengine kabisa kuendesha hizo NGOs..Hawa wote walikuwa hawana magari wala nyumba za maana nenda leo katazame maisha yao wao binafsi, yamebadilika ghafla kuliko hata waathirka kwa kutumia jina la Jinsia..
  Haya yangu pia myaite makelele..lakini huwezi kutumia janvi hili kupinga maamuzi ya watu ktk mbinu za kulijenga taifa letu iwe kupiga makelele au kuomba misaada serikalini ili kukidhi maisha yako na kusaidia kidogo waaathirika kwa aslimia 20 ya pato zima...
  Kitu muhimu ni kutambua kwamba Ujenzi wa taifa lolote lile ni mkusanyiko wa mambo mengi..Kuhoji utekelezaji mbaya haiwezekani kuwa ni kupiga makelele..Na siku zote mtu yeyote anayejitokeza na kusema - he will fight to make a change! huwezi mchagulia uwanja.... wakati Mohammed Ally anapigana masumbwi jukwaani, Martin Luther King alikuwa mpiga makelele.. wote hawa walileta mabadiliko ktk maisha ya watu weusi Marekani.
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,420
  Likes Received: 81,471
  Trophy Points: 280
  Bluray na Mkandara ahsanteni sana kwa majibu mazuri. Hatuweze tena kuendelea kukaa kimya wakati tunaona wazungua wanaingia Tanzia maskini na kuondoka mabilionea tunawaona akina Manji, Rostam, Chavda, Subhash Patel, Jeet wakiiba mabilioni ya pesa kwa njia za kifisadi na kuachwa kuendelea kupeta uraiani huku wakifaidi matunda ya wafanyakazi na wakulima walalahoi ambao hawayafaidi matunda ya jasho lao. Hatuwezi kukaa kimya huku rasilimali zetu zikiwemo dhahabu, Tanzanet, almasi zikiwanufaisha Wazungu, wahindi na makampuni ya nje huku Watanzania tukiachiwa mashimo bila kuona manufaa yoyote ya rasilimalizetu hizo. Hatuwezi kukaa kimya huku viongozi waroho wa utajiri wa haraka haraka akina Mkapa, Chenge, Mramba, Yona, Karamagi na wengineo wengi wakituibia mchana kweupe ili kukidhi uroho wao wa utajiri huku Tanzania ikiendelea kutokuwa na maendeleo yoyote ya kutia moyo.

  Wakati wa kuendelea kukaa kimya umeshapita. Tutaendelea kupiga kelele mpaka umma wote wa Watanzania uelewe nini kinaendelea katika nchi yetu ili tufanye mabadiliko ya kweli kwa niaba ya Watanzania wote na vizazi vyetu vijavyo.
   
 5. L

  LeoKweli JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2009
  Joined: Apr 23, 2008
  Messages: 335
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hawa kina andrew Mushi ndio wamekuwa wakitumika kama toolbox pale TANGO kupitisha hoja za serikali ki ulaini bila kuhoji maswali magumu kwenye Public Expenditure Review , na sikuhizi Hizo NGO ndio zimewekwa mfukoni than before through utaratibu mpya wa Basket Funds, Ukiangalia Tanzania serikali ina perfomance nzuri kuliko NGOS, na ninaomba huyu mushi kwa miaka yake yote kufanya kazi TANGO kama anabisha aje na perfomance benchmarks against NGOS and government tuone, accountability zerooo.

  NGO za bongo wanandika project ,kabla hata ya kupata pesa, huwa tayari wana result za monitoring and evalution kabisaa , baada ya kupata pesa project g hewa ya siku mbili mainly semina au kama ni jengo la very law quality lakini report wameshamiliza inayowalizisha watoaji , kwahiyo huo mfano wa tisheti unazigusa NGOS za bongo mojakwa moja administration costs kibao kuliko hata implimentation.

  Serikali iki imarika i believe matatizo ya NGO yatakuwa machache
   
 6. Tatu

  Tatu JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2009
  Joined: Oct 6, 2006
  Messages: 1,081
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 145
  amushi:

  What's Kelele? Can you define that for me/us?

  So, do you think JF Members are just blowing hot air?

  Did you find any constructive ideas from JF members which can be educational and critical on the way we see things?
   
Loading...