Hatufanyi jaribio kuingia kwenye ndoa

Hatufanyi jaribio kuingia kwenye ndoa

12STONE

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2013
Posts
1,190
Reaction score
409
Wanajamvi.

Ni vizuri hili suala lieleweke wazi kwa wote hasa wale ambao bado kuoa au kuolewa.Ndoa ni makubaliano ya hiari kwa wawili,ni mapatano na agano la kuanza kujenga himaya yenu mpya.

Inapendeza wana ndoa wakiifurahia ndoa yao ni vema wale wasio na wenzi kujiandaa kuishi na mwenza wao.
Maandalizi hayo yalenge mambo yafuatao:-

1.Kupendana.
2.Kuthaminiana.
3.Kustahi.
4.Kusameheana.
5.Utii.
Kutunzana.

Pia lazima mume ajitambue mapema yeye ndiye mhusika mkuu wa mrembo wake.Ukioa huyo mke sio mke wa kijiji wala ukoo kwa maana nzuri tu.

Linda mkeo usiache shemeji mtu na mawifi wanaropokea mkeo kama wapendavyo.

Wanandoa wakitambua wao ni akina nani na kuweka mipaka kwa mambo yasiyoya lazima,mtaifurahia ndoa yenu mwanzo mwisho.Masikio na midomo ya majungu ikae mbali nanyi.

Mwisho kwa wale ambao bado hawajaoa msiwe wepesi wa kutoa ahadi zisizotimilika kwa kuwaambia Wasichana hasa walioiva kuolewa,Ilove you, nataka nikuoe baada ya hapo wanapiga corner.

Tatizo wanaume walio wengi huvutiwa na maumbile ya nje tu hawafuatilii tabia kwanza huku mioyoni mwao wanaume hao kuoa kwao sio kipaumbele chao.

Tukitaka kuwa na familia bora zilizo imara lazima tujenge misingi bora na imara kwa kuanza na mahusiano ya kuingia kwenye ndoa.

Chunguza,jiridhishe,tosheka,sema ukweli kisha amua kuingia kwenye ndoa badala ya kuishi kwenye ndoa kwa kuvumiliana mtaishi kwa kuifurahia ndoa yenu.

Nawasilisha kwenu.

Unakaa Sayari ya ngapi weye? Dunia hii hii yenye Wanaume na Wanawake! Ama Mwenzetu yuko Sayari ya Pluto/Utaridi!!!
 
Mie bado siamini kama ndoa ni jambo muhimu sana

unaona si jambo la muhimu sana sababu vitu vingi vimerahisihwa katika upatikanaji wake.....mfano unyumba unaweza kupata....tena muda wowote.......watoto unaweza kuzaa bila ndoa na kadhalika......ndiyo maana unaona siyo jambo muhimu sana......
 
Siku hizi nikisha toa ushauri namalizia hivi, yakukishinda ondoka mapema...usisubiri hadi hali iwe mbaya.
 
Unaona si jambo la muhimu sana sababu vitu vingi vimerahisihwa katika upatikanaji wake,mfano unyumba unaweza kupata.tena muda wowote watoto unaweza kuzaa bila ndoa na kadhalika,ndiyo maana unaona siyo jambo muhimu sana.

Huo uhuru wa ovyo huleta ongezeko la watoto wa mitaani,Ni aibu kwa wanaume wafurahiapo mahaba na mabinti /wanawake kisha wakipatikana viumbe wanaikataa damu yao yenyewe na kuwachia machungu wapenzin wao
 
ndiyo hivyo wanafurahia uzinzi.....
 
Maumbile ya nje ni muhimu nayo pia

Kabisaaa ni muhimu mno tena usije ukakosea kama wewe Mwanamume/Mwanamke unataka Mkeo/Mumeo awe wa rangi fulani,mrefu au mfupi,mnene ama mwembamba.

Japo baadhi ya vigezo vyaweza kubadilika mf.wembamba hadi unene.

Basi zingatia vigezo hivyo Lakini lazima ujue hizo sio SIFA PEKEE zenye kukidhi viwango na Sifa za Mwenzi umtakaye ama Umpendaye.
 
Mkuu, asante kwa maneno yako yenye hekma, ntayafanyia kazi
 
Back
Top Bottom