Hatua zipi nizifuate ili kujiridhisha kuwa pikipiki nayotaka kununua kwa mtu si ya wizi?

Ahmet

JF-Expert Member
Oct 15, 2019
1,537
3,404
Habari zenu wanaJF,

Nina mpango wa kununua pikipiki used, nimeona mitandaoni Facebook na Instagram pikipiki nyingi zinauzwa. Ukiachana na hofu ya kununua bidhaa mbovu, hofu yangu kubwa zaidi ni kununua bidhaa ya wizi ambapo bila shaka unaweza kuishia sehemu mbaya.

Sasa Basi wadau naomba mnijuze ni hatua zipi nizifuate ili kujiakikishia kuwa chombo nachotaka kununua si cha wizi?

naombeni muongozo tafadhari.
 
Kupewa kadi original piki piki, pia mwandikishane kisheria wakati wa mauziano itakusaidia kubadilisha kadi jina

Vingine wataongezeaaa wadau
 
Shukran kwa muongozo, na huko kuandikishiana kisheria kunaweza kufanyika wapi
 
Usinunue kutoka kwa mtu ambaye jina lake halisomi kwenye kadi esp endapo hana nyaraka za mauziano zilizo halali kisheria.
 
Asante kwa ushauri, na vip Kama nataka kununua kwa hawa watu ambao kazi yao ni kuzinunua kutoka kwa watu wengine na wao kuziuza tena? Vip wanaweza kuwa na nyaraka zote hizo?
 
Kama hawana nyaraka ina maana si wamiliki halali kisheria. Kumbuka hicho ni chombo cha moto, kuna masuala ya historia ya matumizi ya chombo hicho, ukinunua halafu bahati mbaya kikawa kina historia ya uhalifu, kama huna ushahidi wa mmiliki kabla hujawa nacho wewe utakuwa katika wakati mgumu kujitetea.
 
Asante sana nipekupata mkuu
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Nimenunua na kuuza pkpk used zaidi ya 15 kwa nyakati tofauti.

Kikubwa muone mtendaji wa kata mpe 10 wengine mpaka 20 elfu. Andikishaneni mbele yake na kubadirisha pesa na nyaraka mbele yake.

Karatasi ya kuandikishana lazima liwe na mihuri wa huyo mtendaji.

Mwisho kabisa, ile kadi lazima namba zilizopo kwenye kadi mfano, injini namba iliyopo kwenye kadi iendane na kwenye injin, plate namba inayosoma kwenye kadi pia isome kwenye kibao cha pkpk (plate no.) Na mwisho chases namba viendan.

Hapo hiyo kadi na pkpk vitakua ni halali na kujua kadi si kopi angalia kuna nembo ya kung'aa lazima iwe halisi.

Karibu hata sasa nauza pkpk boxer 125 CHF.
 
Nimenunua na kuuza pkpk used zaidi ya 15 kwa nyakati tofauti.

Kikubwa muone mtendaji wa kata mpe 10 wengine mpaka 20 elfu.
Andikishaneni mbele yake na kubadirisha pesa na nyaraka mbele yake.

Karatasi ya kuandikishana lazima liwe na mihuri wa huyo mtendaji.

Mwisho kabisa, ile kadi lazima namba zilizopo kwenye kadi mfano, injini namba iliyopo kwenye kadi iendane na kwenye injin, plate namba inayosoma kwenye kadi pia isome kwenye kibao cha pkpk (plate no.)
,Na mwisho chases namba viendan.

Asante sana, hakika umeeleza vizuri, vip inapatikana wapi mkuu
 
Njoo nikuuzie honda yangu sijui bei utaiweza m2 haishuki zaidi ya hapo

FB_IMG_16223802538332661.jpg
 
Habari mkuu, ukishakagua ubora wa chombo na mkakubaliana bei fanya yafuatayo:

1. Omba nakala ya kadi kisha fika TRA watakuambia mmiliki halali wa chombo.
2. Baada ya kujua kuwa anayekuuzia ndiye mmiliki, tafuta wakili akusaidie kuandaa mkataba wa mauziano.
3. Hakikisha wakati wa makabidhiano ya fedha husika kuwepo na mashahidi owapo mtakabidhuana cash na wote wahakiki kiasi ulicholipa.
4. Kama malipo yatafanyika benki basi hakikisha akaunti namba na benki vinatajwa kwenye huo mkataba.
5. Baada ya amuziano hakikisha unawasiliana na TRA ili kubadili umiliki na pikipiki iwe kwa jina lako.

Hiyo namba 1 ni muhimu sana maana watu wanatengeneza sana kadi fake siku hizi hivyo kushindwa kutambua mmiliki halisi kisha ukashikishwa mzigo.

Kila la kheri.
 
Hakika naendelea kupata faida, shukran kwa maelezo yaliyonyooka,
 
Nimenunua na kuuza pkpk used zaidi ya 15 kwa nyakati tofauti.

Kikubwa muone mtendaji wa kata mpe 10 wengine mpaka 20 elfu.
Andikishaneni mbele yake na kubadirisha pesa na nyaraka mbele yake.

Karatasi ya kuandikishana lazima liwe na mihuri wa huyo mtendaji.

Mwisho kabisa, ile kadi lazima namba zilizopo kwenye kadi mfano, injini namba iliyopo kwenye kadi iendane na kwenye injin, plate namba inayosoma kwenye kadi pia isome kwenye kibao cha pkpk (plate no.)
,Na mwisho chases namba viendan.

Hapo hiyo kadi na pkpk vitakua ni halali na kujua kadi si kopi angalia kuna nembo ya kung'aa lazima iwe halisi.

Karibu hata sasa nauza pkpk boxer 125 CHF.
Mkuu bado unafanya hii biashara ya pikipiki used
 
Back
Top Bottom