Hatua za kupata udhamini ughaibuni (2) - makulilo, jr. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatua za kupata udhamini ughaibuni (2) - makulilo, jr.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by MAKULILO, Jan 30, 2012.

 1. MAKULILO

  MAKULILO Member

  #1
  Jan 30, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  NA: ERNEST BONIFACE MAKULILO (MAKULILO, JR.)
  CALIFORNIA, USA

  View attachment 46332

  Ufuatao ni muendelezo wa hatua za kufuata ili mtu uweze kupata udhamini wa elimu ya juu ughaibuni. Na katika wiki iliyopita tuliona vitu vikubwa viwili navyo ni Barua ya Motisha (Statement of Purpose) na Insha ya Udahili (Admission Essay). Leo hii tutaangalia hatua nyingine ambayo ni Barua ya Mapendekezo (Recommendation Letter).

  Barua ya Mapendekezo (Recommendation Letter) ni nini? Ni nani anatakiwa kuandika? Nini kinatakiwa kuandikwa? Ni barua ngapi zinahitajika? Njia zipi za kufanikisha kutuma barua hizi? Haya ni maswali muhimu ambayo mtu ukiyajua na kuyafanyia kazi itakuwezesha kuwa mwamboji mshindani na si msindikizaji.

  Barua ya mapendekezo ni barua ambayo ni muhimu sana ambayo wanaodahili huitumia kama kigezo kikubwa cha nani achukuliwe na kupewa udhamini na nani aachwe. Mtu unaweza kuwa na matokeo mazuri sana, ila ukawa na barua ya mapendekezo mbovu inayoonesha kuwa huna uwezo nk hivyo utashindwa kudahiliwa na kupata udhamini sababu ya barua hiyo.
  Kila chuo utakachoomba unatakiwa utume barua za mapendekezo. Barua hizi zinatakiwa ziandikwe na aidha mwalimu wako aliyekufundisha au mwajiri/mkuu wako katika fani unayofanyia kazi. Kama ni mwalimu wako anayeandika barua hii ni lazima aoneshe uwezo wako wa kuandika insha makini zenye utafiti ulioshiba, uwezo wako darasani kwa ujumla, matarajio yake kama wewe ukipata nafasi hiyo utafanya nini nk. Na kama ni mwajiri au msimamizi wako kazini akiandika barua hii ni vyema aoneshe uwezo wako kikazi upo vipi, mchango wako kazini na ni nini matarajio yao endapo wewe utapata nafasi ya kusoma chuo uombacho ni mabadiliko gani unaweza kuyaleta katika ofisi hiyo na/au jamii yako husika.

  Mara nyingi unapoombwa kupeleka barua za mapendekezo hupendelea barua tatu kutumwa. Ushauri wangu ni vyema upeleke barua si chini ya nne, yaani barua mbili toka kwa mwajiri au msamizi wako kazini, na barua mbili toka kwa mwalimu wako aliyekufundisha. Hii itaonesha kuwa una watu wanaoamini uwezo wako.

  Si kila mtu kwakua alikua mwalimu wako basi ana sifa za kukuandikia barua za mapendekezo au kwakua mtu ni mwajiri wako au msimamizi wako kazini basi ndio akuandikie barua hizi. Kuna waajiri wengine hawapendi wafanyakazi wao waende kujiendeleza kielimu, au kuna wasimamizi wengine wanakuwa na chuki binafsi au kutopenda maendeleo ya mwingine, sasa ukimpa nafasi ya kukuandikia barua ya mapendekezo anaweza kutumia fursa hiyo kukuangamiza kwa kuandika kuwa una uwezo mdogo, hufai na huwezi kuleta mafanikio yoyote kwa jamii yako. Barua ya namna hiyo itakufanya uondolewe kwenye kinyangÂ’anyiro cha watu wanaweza kupata udhamini. Hivyo uchaguzi wa mwalimu gani au msimamizi gani kazini akuandikie barua ni muhimu sana.

  Kuna njia kuu mbili ambazo hutumiwa mwandikaji wa barua za mapendekezo kuwasilisha barua hizo. Njia hizo ni njia ya kwenye mtandao (online recommendation) na njia ya barua kwa njia ya posta (snail mail). Itategemea chuo na chuo, kuna vyuo ambavyo wao wanampa mwandikaji barua chaguo yeye angependa atumie njia gani kati ya hizo, ila kuna vyuo wanakuchagulia utumie njia gani kuwasilisha barua hiyo kama ni kwa njia ya mtandao au barua kwa njia ya posta.

  Endapo barua itakuwa inaandikwa na kutumwa kwa njia ya posta, ni lazima barua hiyo iwe kwenye bahasha ya kiofisi yenye nembo ya ofisi au chuo husika. Na pia barua iandikwe kwenye karatasi la kiofisi lenye nembo ya chuo au ofisi husika (official letter head). Pia muhuri wa ofisi au chuo husika ni vyema uwepo ili kuthibisha. Na endapo barua itawasilishwa kwa njia ya mtandao ni vyema anuani ya barua pepe ya mwandishi wa barua hiyo iwe ya kiofisi na si anuani binafsi. Mfano wa barua pepe binafsi ni zile kama za yahoo.com, gmail, hotmail nk, na zile za kiofisi huwa zinakuwa na tovuti ya kiofisi mwishoni mwake, mfano Makulilo@makulilofoundation.org. Endapo hutofuata masharti hayo kuna walakini wanaodahili kuanza kuhisi kuwa barua iliyowasilishwa ni ya kugushi na si halali, kupewa walakini. Inabidi uondoe huo walakini kwa kuwa makini katika kila hatua. Na kama pia barua hiyo itaandikwa kwa kutumwa kwa njia ya posta ni vyema barua hiyo iandikwe mapema na kutumwa mapema ili iwasili kabla ya tarehe ya mwisho ya kupokea maombi.

  Napenda kukupa anuani hizi mbili za tovuti ambazo zitakusaidia kujua zaidi kuhusu barua za mapendekezo na utaweza pia kupata sampuli baadhi. Anuani hizi ni www.recommendationletters.org na www.lettersofrecommendation.net

  Pia nimeandaa video ambayo inatoa maelezo mazuri kuhusu barua hizi na ninaamini itakuwa ya msaada sana kwako. Tovuti yangu ya www.makulilofoundation.org ina video hiyo. Na kwa video nyinginezo za msaada wa kupata udhamini ughaibuni zinapatikana katika Makulilo Scholarship Show inayoongozwa nami www.youtube.com/makulilofoundation
  Kwa wenye maswali au maoni, niandikie hapa Makulilo@makulilofoundation.org. Fuatalia mfululizo wa hatua za kupata udhamini ughaibuni katika makala inayofuata.

  MAKULILO, Jr.
  CALIFORNIA, USA
   
 2. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #2
  Jan 30, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Asante sana kwa maelezo. Endelea kutoa maelekezo ya njia nzuri ya kuapply kwa ajili ya scholarship. Ipo siku watanzania wengi watafunguaka na kuona yote inawezekana. Suala ni kujipanga. Keep it up Makulilo Jr
   
 3. MAKULILO

  MAKULILO Member

  #3
  Jan 30, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Asante mdau Chona,

  Naamini kabisa mbeleni watu watazidi kuchangamkia fursa hizi

  MAKULILO
   
 4. +255

  +255 JF-Expert Member

  #4
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 1,909
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 180
  Thanx mkuu, hili ni darasa tosha. Minimum GPA ya kuwa na possibility kupata scholarship ni kama ngapi ukiacha hz issue nyngn ka recommendation letter etc
   
 5. MAKULILO

  MAKULILO Member

  #5
  Jan 30, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Ndugu +255,

  Kawaida hakuna minimum GPA, ila kutokana na ushindani uliopo, ni vyema uwe na GPA ya kuanzia Upper Second Class yaani 3.5 na kuendelea. Hii itakuwezesha kuwa mshindani mkubwa.

  Kuna baadhi ya scholarships mfano zile za Quota Scheme huko Norway wao wanaandika kabisa kuwa kama huna 3.5 na kupanda juu basi huruhusiwi hata kuomba. Hivyo zipo scholarships ambazo zinasema uwe na GPA ya ngapi, na zipo zingine haziosemi huacha ushindani uamue inakuaje.

  Pia, ktk admission na scholarship decision, sio kila wakati wanachukua mtu kwa kuangalia GPA pekee kama kigezo. Kuna vitu vingi sana wanavyoangalia. Mfano ni kama huu. Ndugu Sumaye alikua Waziri Mkuu wa Tanzania kwa miaka 10. Na aliomba kusoma MA Public Administration huko Havard University na alikuwa admitted..sijui kama alijilipia au alipewa scholarship na chuo au serikali ya Tanzania. Hayo tuyaache, lakini kubwa ni kwamba kwa kuwa alikuwa Waziri Mkuu wa nchi kwa miaka 10, hata kama angelikuwa na GPA ya Lower Second Class, au just Pass angeweza kuchaguliwa kujiunga na Havard kwa uwaziri mkuu ni uzoefu mkubwa sana kwa kupewa udahili.

  Hivyo unapofanya application usijiamini tu kwakuwa una 1st class, au upper second kuwa lazima upewe scholarship. Mfano ukipewa recommendation mbaya inakula kwako, au umkaandika statement of purpose mbovu hata kama umefaulu vizuri hutopewa scholarship. Kila kitu kwenye application kinapewa higher consideration hivyo ni kuandaa winning application.

  MAKULILO
   
 6. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #6
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 861
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu,me najiulzaga,unakuta scholarship wanasema lazima ulipie application fee, sa sijui wanakua hawajui kwamba mpaka mtu anaamua kuomba scholarship ni kwamba ye ni choka mbaya,unadhan hyo application fee let say $ 120,mtanzania wa kawaida utaitolea wapi?
   
 7. JAPUONY

  JAPUONY JF-Expert Member

  #7
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 374
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ushauri wangu ni kwamba, ukiona scholarships zenye fee (yaani za kulipia fee) usiombe. maranyingi zinakuwa za matapeli. Scholarships nyingi hakuna fee.
   
 8. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #8
  Jan 30, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 861
  Trophy Points: 280
  asante kwa ufafanuzi wako mkuu.
   
 9. Mpatanishi

  Mpatanishi JF-Expert Member

  #9
  Jan 30, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 1,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Big up Makulilo.
  Tunachangamkia fursa hizi.
   
 10. Adharusi

  Adharusi JF-Expert Member

  #10
  Jan 30, 2012
  Joined: Jan 22, 2012
  Messages: 10,635
  Likes Received: 3,017
  Trophy Points: 280
  Safi sana
  Mr Makulilo jr
   
 11. MAKULILO

  MAKULILO Member

  #11
  Jan 31, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Kuhusu suala la Application Fee, si kwamba ni wezi wanaposema hivyo. Nina article nimeandika kuhusu Application Fee, inakuaje na nini ufanye. Ila kwa ufupi ni kwamba, kwa vyuo vya Marekani na Canada...application fee ni lazima ulipe...ila kwa Ulaya, Australia, New Zealand nk wao hawana application fee. Huo ni utaratibu wao. Ni mara chache sana kukuta scholarships za Marekani na Canada hazina application fee...nitaeleza kwenye makala yangu kwa kina

  Pia nina makala nimeandika, nitaibandika hapa punde ambapo inaelezea utofauti uliopo ktk utaratibu wa uombaji vyuo Ulaya vs Marekani nk. Na ushauri wangu wa kitaalam ufanyaje. Maana sehemu ya kutaka kwenda kusoma tu, itakufanya ujue utaratibu na ujipange vipi kwenye mchakato mzima.

  MAKULILO
   
 12. Chona

  Chona JF-Expert Member

  #12
  Jan 31, 2012
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 514
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Nadhani ukieleza kwa kina juu ya suala la application fee litasaidia sana. Binafsi nimekuwa nikitatizwa sana na suala la application fee mfano Sweeden na nchi zingine ulizo zitaja. Ukifanya conversion ya hela wanayohitaji utakuta ni kubwa. Kiasi kwamba kwa mtu wa kawaida huwezi si kuipata tu bali kuitoa kwa kitu ambacho pia akikugarantee kupata hiyo scholarship baada ya admission. Ni suala ambalo linahitaji umakini na ufumbuzi hasa kwa watu wanaotaka kusoma huku kipato chao kikiwa kidogo. Inasumbua kidogo ingawa wanasema elimu ni gharama, lakini wakati mwingine wale wanaohihitaji si tu kuwa wanaogopa gharama ila hawana uwezo wa kugharamikia gharama hizo, maisha magumu.
   
 13. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #13
  Jan 31, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,029
  Likes Received: 861
  Trophy Points: 280
  Kuna mtu wangu wa karibu amejaribu kuaapply for swedish scholarship,wamesisitza kama ni non-EU citizen lazima ulipe application fee,bt cha kushangaza amefanikiwa kuaply na wamemuambia wako kwenye selection process.hyo imekaaje mkuu,watamchagua kweli hapo?
   
 14. MAKULILO

  MAKULILO Member

  #14
  Jan 31, 2012
  Joined: May 30, 2010
  Messages: 84
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Kwa ufahamu wangu Swedish Scholarship Application haina Application Fee. Nina mashaka kama amelipa anaweza kuwa amelipa matapeli. Mfano ukifungua link hii Search Results - sweden - SCHOLARSHIP FORUM itakuonesha baadhi ya Swedis Scholarships na hakuna application fee. Na huo ni utaratibu wa vyuo vya Ulaya.

  Sasahivi nipo naandika kitabu kiitwacho SCHOLARSHIP OPPORTUNITIES IN AMERICA AND EUROPE: The Secret From Makulilo. Na moja ya Chapters ni AMERICA vs EUROPE: Comparative Analysis. Chapter hiyo inaeleza kwa kina hatua za uombaji scholarships kwa ujumla, utofauti uliopo kati ya Ulaya na Amerika...na ushauri wangu wa kitaalam ni upi...yaani wapi mtu uweze kufanya maombi yako kwa wingi.Moja ya tools of analysis niliyotumia ni Application Fee...utofauti uliopo kati ya Ulaya na Amerika.

  Ndugu Senetor, naandika kwa kina uchambuzi wa application fee na nitauweka hapa punde tu.

  MAKULILO
   
 15. Z

  Zabron Erasto Member

  #15
  Feb 1, 2012
  Joined: May 29, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ahsante mkuu kwa kututahadhalisha
   
Loading...