Natafuta Pampu ya umwagiliaji

chayowa

JF-Expert Member
Aug 15, 2011
413
109
Habari Wadau wa jukwaa la ujasiriamali.
Nina shamba la hekari 20 nataka kulilima kwa kilimo cha umwagiliaji ambao tayari nimeshachimba kisima. Sasa natafuta pampu nzuri yenye ubora mzuri wa kufanya kazi. Nitashukuru mkinisaidia aina tofauti, uwezo wa kazi, na makadirio ya bei.
Nategemea kufanya umwagiliaji wa kumwaga maji kwenye mifereji kwa sasa kabla sijajaribu kuweka tenki na mabomba.
Nawashukuru sana

Update...
Baada ya kuwa na shamba na kijipamp changu na kufanya utafiti kipindi cha kulima zao nilitamanilo sana la kitunguu nikaamua ni test na ekari 3 hivi kwa zao la nyanya.
Kiukweli zao hili lina changamoto kubwa sana hasa kipindi hiki cha mvua. Dawa zitumikazo ni nyingi sana sana kiasi kwamba kwa mahesabu hadi ya leo siku ya 93 imeshakata 4.7M.
Nasoma ' think and grow rich cha napoleon Hill napata nguvu na faraja hasa katika charter ya desire na faith'... na kutokana na ukweli kwamba kwasasa nyanya iko juu sokoni... jana kariakoo ilikuwa juu ya 50000 kwa box hope I will make the dream in to reality..
Pamp hii inajitahidi. .. nimeifanyia service mara moja tu hadi sasa kwa shilingi 19000 pamoja na pesa ya fundi na usafiri. Ila nimegundua inafanya kazi kubwa sana kwani inanyonya maji kutoka kisimani ambapo ni mbali sana kama 13m hivi steep slope.. hii inasababisha kutumia nguvu nyingi hivyo mafuta pia. Nawaza mbinu ya kuiwekea kitanda ili kuisaidia kidogo. Huwa inatumia litre 15 hadi 20 kumwagilia hekari tatu vizuri.. kumbuka natumia umwagiliaji wa mifereji kwahiyo kuna upotevu mkubwa sana wa maji. Nawaza kufanya utaalamu zaidi baadae wa drip pesa ikifikia.
 
Maada nzuri hata mie nasubiria watalam waje hapa ili tufaidi wengi Halooooo popote mlipo watuwa kilimo kwanza na wataalam wa irrigation tasavali mkuje huku
 
Nakushauri uwasiliane na jamaa wa SN-TECH waliopo Nkrumah street jijini Dar es Salaam karibu na New Continental Hotel. Namba zao za simu ni 2 128 007. Mimi nilielekezwa na injinia mmoja wa maji aliyekuwa anawafahamu. Nilipokwenda pale niliwaelezea mahitaji yangu ya maji kwa kina na wao kwa kuzingatia mahitaji yangu walinichagulia pump ambayo kiukweli tangu nimeifunga February 2007 haijawahi kuharibika hadi hivi leo. Kwa wiki uwa naiwasha siku tatu kwa ajili ya kusukuma maji. Sana sana ni service tu ambayo uwa nafanya kila baada ya miezi sita. Hawa jamaa kwa ubora wa pump zao niliwakubali na hata bei zao hazikuwa kubwa. Labda hivi karibuni wawe tu wamebadilika. Wengine wanaouza pump imara za maji ni Davis and Shirtliff walio maeneo ya KAMATA (Dar) japo hawa kwa wakati huo niliona bei zao ziko juu. Pia kuna Merry Water Ltd na Balton Ltd wanauza pump nzuri.
 
Dah asante sana Mkuu.. Inatumia mafuta gani? naona kama namba umeikosea mkuu.
 
Mkuu pia unaweza kucheki na jamaa wa Rift Valley Machinery Ltd walio karibu na Kibodya Hotel pale Nkurumah street (Dar).
 
Nimefanikiwa kuipata moja maeneo ya kariakoo... Nashukuru kwa wote mliokuwa na nia ya kunisaidia... nimeona nianze na hii kwa muda kabla sijachukua mashine kubwa zaidi.. nimechukua 7.5hp, 3 inch, petrol
 
Mkuu chayowa, tuambie na bei zake umepata kwa bei gani?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu chayowa, tuambie na bei zake umepata kwa bei gani?

Mkuu nimeinunua pump yenyewe laki 3, vishikio vya bomba elfu 40, bomba la kuvutia maji mita Moja elfu 20, na kidude cha kuzuia kunyonya takataka elfu 60.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu nimeinunua pump yenyewe laki 3, vishikio vya bomba elfu 40, bomba la kuvutia maji mita Moja elfu 20, na kidude cha kuzuia kunyonya takataka elfu 60.

Mkuu kwa bei hizi wamekuliza kiaina! yaani chujio la takataka kwenye inlet pipe sh60k? je, delivery pipe bei gani? na isitoshe hiyo pump ni mchina!!
 
Mkuu kwa bei hizi wamekuliza kiaina! yaani chujio la takataka kwenye inlet pipe sh60k? je, delivery pipe bei gani? na isitoshe hiyo pump ni mchina!!

Dah ndio kariakoo ndugu... sikuwa na namna kwani uhitaji ulikuwa umebana sana na pesa ya kuchukua kubwa zaidi ilipungua...
 
uzuri wa nashine za mchina ni bei kuwa rahisi, hivyo kwa kuanzia ni nzuri pia spares zinapatikana sana.
Ebu utakapoanza kuutumia tpe majibu
 
Wewe tusaidie bei halisi ili tusilizwe wengii

Ninayo pump used kutoka Italy. Ni ndogo kwa umbo na iko portable watu wawili wanabeba bila shida. Uwezo wake ni HP 30. Sijawahi kuitumia. Anayehitaji bei 3.0 million. call 0764640244
 
Jinsi ya kuchagua pump kwa ajili ya matumizi yako ya umwagiliaji!

images

prm_pump.jpg

Image source: mtandao.

Kabla ya yote, Kuna huu uzi ambao pia ulikua unaelezea kilimo cha umwagiliajai kwa ujumla Special thread: Kilimo cha umwagiliaji (Irrigation)

Ni ukweli usiopingika katika kilimo cha umwagiliaji, pump ni kama moyo au sehemu ya muhimu ya umwagiliaji! Pia pump inachukua kiasi kikubwa katika bajeti ya kuanza kilimo cha umwagiliaji, hivyo ni vyema tukachagua pump ambayo hatuwezi kujutia baada ya kuinunua!!! Hizi ni njia ambazo unaweza kuzitumia wakati unachagua pump kwa ajili ya kilimo cha umwagiliaji!

1. Price/gharama.

Ni ukweli usio pingika kwamba kwa sasa kutokana na soko huria, bidhaa moja inaweza kuwa na bei tofauti kulingana na duka! Hapa lazima uchague pump ambayo utatumia gharama ndogo ili kubata ubora unahitajika. Lakini pia ni vyema ukajua unapoangalia bei pia zingatia ubora wa pump!!

2. Fuel/Mafuta

Pump nying zinatumia mafuta ya diesel au petrol! Sasa hapa unatakiwa ujue kati ya petrol na diesel ni wapi patakua rahisi kwako hasa katika swala la gharama! Je petrol ni shilingi ngapi kwa lita? Je diesel ni shilingi ngapikwa lita? Ni ukweli kwamba engine inayotumia diesel ina ufanisi/efficiency mkubwa kuliko injini ya petrol!

Kama hiyo haitoshi kuna pump ambazo zinatumia umeme na nyingine zinazotumia solar/umeme wa jua! Hapa unatakiwa uamue moja ambayo itakua rahisi kwako!

3. Operation/matumizi

Kuna pump unatumia manually na nyingine unaziwasha na kuacha ziendelee kufanya kazi! Kuna pump kama money maker pump ambazo nguvu yako inahitajika ili ifanye kazi, ila nyingine mfano za petrol na diesel haziitaji uzi-operate manually!!

4. Matengenzo/service

Je pump unayotaka kuinunua inatengenezeka kwa urahisi? Pump kama mashine nyingine inafika kipingi zinaharibika kwahiyo ni vyema unaponunua uangalie je inatengenezeka kwa urahisi? Je vifaa/spare vyake vinapatikana kwa urahisi??

5. Ukubwa wa eneo!

Shamba likiwa kubwa maana utahitaji pump kubwa zaidi, na shamba likiwa dogo utahitaji pump yenye uwezo wa wastani!

Capture.PNG

Kutoka kwenye manual book ya pump aina ya honda…

Sunction port diameter.

Hiki ni kipenyo cha sehemu ya kuvutia maji. Kama tunavyoona imeandikwa 2 inches, hizi zinatofautiana kulingana na ukubwa wa pump, inaweza kuwa Zaidi ya 2inches!

Delivery port diameter.

Delivery port ni sehemu au tundu la kutolea maji kutoka kwenye pump!

Total head.

Huu ni umbali kwenda juu, ambapo pump ina uwezo kusukuma maji, kwa case yetu ni futi 64 sawa mita 50!

Delivery head.

Huu ni umbali (vertical distance) ambapo pump inauwezo kusukuma maji. Umbali huu unaanzia kwenye delivery port.

Sunction head.

Huu ni umbali ambao pump inaweza kuvuta/kuvyonza maji kutoka kwenye chanzo kama mto, bwawa, mfereji n.k. mara nyingi huwaga mfupi kuliko delivery head!

Discharge capacity!

Hii ni sehemu ya muhimu ya pump. Hapa tunaonyeshwa uwezo kamili wa pump, je pump ina uwezo wa kusukuma maji kiasi gani je ndani ya muda gani?? huwa inaandikwa interms of discharge/flux per time! kwa mfano hapo juu pump yetu imeandikwa discharge capacity equals to 500 litres per minutes! kwa lugha nyingine tunaweza sema pump yetu ina uwezo wa kutoa lita 500 kwa dakika! hii inatofautiana pump na pump pia inaweza wekwa kwa vipimo tofauti yaani ft/min au Miter cubic per hour n.k.

Priming.

Hikini kitendo cha kuondoa hewa ambayo ina madhara makubwa sana ndani ya pump! Kuna pump lazima utoe hewa manually na nyingine ni automatic!! ni vyema ukachagua pump inayotoa hewa yenyewe (automatic priming)!
maxresdefault.jpg

Image source: google
 
Back
Top Bottom