Hatua muhimu za kuanza kufanya meditation

Emc2

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2011
Posts
16,808
Reaction score
16,961
Ninawasalimia wana JF wote.
Natumaini ni waziwa wa afya njema. Leo napenda kuanza na somo hili la kuanza hatua kwa hatua kufikia Enlightenment. Nina maanisha kuwa kuweza kufanya meditation na kufikia hatuwa ya kuwa aware. Bila kupoteza mda nitaanza kuelezea kitu kimoja kwa utangulizi.

UTANGULIZI
Asili yetu ni roho zetu, tumekuja kuingia kwenye mwili huu tulionao kwaajili ya kuweza kuishi hapa duniani. Na asili yetu ni universe ambayo ni halisi sio illusion. Basi tunapo zaliwa hapa duniani tunaanza kuwa attached na mambo mengi sana kwa kupitia milango yetu ya fahamu. Kila sekunde inayoupita tunapiga picha na kuweka kwenye database yetu ya akili zetu.

Kadri siku zinavyozidi kwenda tunatengenza ulimwengu ndani ya akili zetu. Ulimwengu huo ninaweza nikauita virtual World. Ni ulimwengu ambao umejengwa kutokana na picha mbali mbali zilizoingizwa kupitia milango ya fahamu.

Wazazi wanapo mzaa mtoto wanaanza kumjenga na kumpa picha tofauti tofauti na huyo mtoto kuwa attached na mazingira ya wazazi. Kadri ya wazazi wanavyotaka watamjenga mtoto wao awe hivyo. Basi ulimwengu huu ambao umejengwa kwenye akili uanawafanya watu wawe hawana furaha, kuchukiana, kupenda utawala, kupenda pesa, kuwa wadini na mambo mengine ya fananayo na hayo.

Mara baada ya mtu kufa tu. Ulimwengu alioujenga unapotea unakuwa haupo maana upo kwenye akili zake tu. Anakutana na uhalisia ulimwengu ambao ni halisi.

Sasa ni vyema kuanza kuondoa ulimwengu huu ndani ya akili zetu na kuweza kuufaidisha ulimwengu kwa kutupa huu mwili na akili ili kukamilisha safali yetu ya hapa duniani. Tukijiunganisha na uhalisia (Universe) na kujua kuwa sisi ni nani hakika tutafanya dunia kuwa sehemu nzuri sana.

1. HATUA YA KWANZA (KUONDOA NA KUANZA KUFUTA ULIMWENGU ULIO KWENYE AKILI)
Ili uweze kufanya meditation vizuri mimi nadhani hii hatua ndio ya kwanza kabisa. Sasa nitaelekeza namna ya kufanya.
a. Kaa sehemu tulivu kwa mda wa kama dakika kumi huku umefumba macho. Anza kujiuliza maswali ndani ya moyo wako (Mimi ni kitu gani, Mimi ni nani, Kwanini nipo duniani, je nimetoka wapi)
b. Baada ya dakika hizo kumi napendekeza hatua ifuatayo inaweza ikakusaidia sana.
i. Fumbua macho anza kutafakari Maisha yako (miaka 0 - 10) kisha (11 - 20) (21 -30) nakuendelea. Fanya mwaka kwa mwaka. (hii inaweza kuchuka kama lisa limoja au zaidi)
ii. Anza kutafakari kuhusu uhusiano kutoka utototni hadi leo(Wazazi, Dini, Shuleni, wapenzi nk)

Tengeneza jedwari lenye namba kuanzia 1 mpaka 50. Kila ukimaliza mzunguko wa kuanzia ulipo zaliwa mpaka sasa zungusha kwenye namba moja wapo mpaka utakapo zimaliza zote hizo hamsini. Kwa wastani unaweza kuchuka masaa 90-100 kwa hatua hii.

Hii hatua ni maandalizi ya kuandaa akili ili iweze kuanza kuziondoa picha zilizopo ndani yake.
Ninapendekeza kuwa ni vyema wakati unatafakari hivyo kuwa umefumbua macho.

Ngoja naomba niishie hapo. Kwa wale ambao watakuwa wapo tayari watakuja walete mlejesho baada ya hatua hiyo ya kwanza na ndipo nitaanzisha hatua nyingine mpaka tutakapo fika enlightenment.

Ahsante karibuni mwenye swali aniulize.
@aretasludovick
 
aretasludovick
Annael kwa maisha tuliyo nayo ni vigumu sana kufanya hiyo practice kuna changamoto za ki maisha kipato na kiimani,
Imagine una madeni lukuki kuanzia kodi za nyumba matumizi ya kila siku ada za watoto mahitaji ya ndugu wazazi na jamaa
Changamoto ya kiimani nayo ni tatizo kubwa imagine unarudi nyumbani na kujifungia chumbani tuli utafikiriwa mengi mabaya
Enlightenment through meditation inataka discipline ya akili ya kiwango cha juu...nimeshauri siku zote kuwa ukiingia kwenye hii practice anza na vitu rahisi, misingi ambayo ndio itakupa mwanga wa nini maana hasa ya concentration na meditation
Nimeshauri kuwa kwa kuanzia mtu ajifunze kuwa na ratiba iliyopangika na kufanya kitu kile kile kwa muda ule ule kila siku mfano..muda wa kuamka muda wa kwenda kazini muda wa kulala nk nk
Pili kuwa na kipimo kile kile cha chakula kwa muda ule ule kila siku usipunguze wala usizidishe
Hapa unai displine mind ni kitu kigumu sana mwanzoni lakini ukifanikiwa utakuwa umepiga hatua moja kubwa sanaView attachment 307899hii ni hatua ya pili kukata hizo u mimi angalia zipo self ngapi
 
Last edited by a moderator:

Uko sahihi kabisa mkuu ndio maana nikahisi huenda hiyo njia inaweza ikasaidia. Maana mtu anaweza akafanya hivyo mahali popote kwa hatua hiyo ya kwanza.
Nipendekezo tu. Labda tunaweza kutafuta njia nyingine rahisi zaidi kwa kipindi hiki cha changamoto ili kusaidiana.
 
Kuna mabandiko mengi mazuri sana humu kuhusu meditation lakini watu wanaishia kusoma na kukosa muda wa kupractice
Kuna kipindi nilishawahi kutoa rai ya kuwa na meditation retreats mara moja au mbili kwa mwezi lakini hatukuweza kufanya hivyo may this time we can try again
 
Mimi nadhani mda utafika tu watu watakapo amua kuamka. Kipindi hiki dalili zinaonekana.
 
Nakubaliana kabisa na somo hili, lakini changamoto ni nyingi mno. Mf mimi kipindi cha miezi mitatu iliyopita nilijitahidi sana. lakini kwasasa imekuwa ngumu kweli baada ya chuo kufunguliwa kila siku test, assgnment mara darasa mpaka jumapili nimejikuta nakwama kabisa.
 
Kama mtu ataweza kumaliza kipindi hicho tajwa hapo. Ninauhakika ataanza kubadili namna ya kuishi. Hii hatua kusema kweli unaweza ukafanya hata ukiwa nyumbani uko kwenye kitanda chako. Tatizo watu wengi kabla ya kuanza kufanya wanatanguliza matatizo kwanza.

Lakini mtu atakaye thubutu na kuanza, Hakika utaanza kutoka kwenye utumwa wa ulimwengu uliopo kwenye akili.

Anza hatua acha, ondoa sababu ambazo kwa uhakika ukiamua unaweza ukazikabili.
 
napenda sana kufanya meditation...nimejaribu kwa miezi miwili mfululizo,tatizo ni kwamba pale ninapofumba macho na kuanza kujiondoa kwenye ulimwengu halisi huwa najikuta kama nimelala flani au nimelala kabisa..je ni kawaida na naizuiaje hii hali?
 
Fuatilia Steps hizi ninazokuelekza hakika utafikia kiu yako.
 
Kuna mabandiko mengi mazuri sana humu kuhusu meditation lakini watu wanaishia kusoma na kukosa muda wa kupractice
Kuna kipindi nilishawahi kutoa rai ya kuwa na meditation retreats mara moja au mbili kwa mwezi lakini hatukuweza kufanya hivyo may this time we can try again

Huu ni ukweli kabisa.
Mimi nilikuwa na bidii lakini sasa naona nimelemaa.
 
napenda sana kufanya meditation...nimejaribu kwa miezi miwili mfululizo,tatizo ni kwamba pale ninapofumba macho na kuanza kujiondoa kwenye ulimwengu halisi huwa najikuta kama nimelala flani au nimelala kabisa..je ni kawaida na naizuiaje hii hali?

Wewe bila shaka utakuwa unafanya meditation usiku/wakati wa kulala tu.
Fanya mchana alafu ulete feedback
 
Sijaelewa hapo kwenye masaa 90-100..Yani masaa yote hayo unakuwa umefumba macho?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom