masubo tapta
Member
- May 17, 2014
- 7
- 5
Ni takribani miaka miwili sasa na ushehe tangia shirika la pride Tanzania kusitisha huduma zake za mikopo kwa kilichoelezwa awali kufirisika lakini chanzo kikubwa kikiwa ubadhirifu wa fedha uliofanywa na aliyekuwa mkurugenzi wa wake ndugu Malima ambaye mpaka sasa anatafutwa.
Shirika lina wafanyakazi wasiopungua 700 wakiwa njia panda wasijue nini kinachoendelea kuhusu ajira zao mishahara na stahiki nyingine huku tegemeo lao kubwa likiwa serikali ambayo ilisemekana imelitwaa tena shirika hilo kisheria,ikimbukwe pride ilitolewa serikalini kiujanja ujanja na watu ambao hawajawekwa wazi mpaka sasa.
Wafanyakazi hao wanaiomba serikali kutoa tamko kwa umma kuhusu hatma yao kwani kila kitu kimesimama kwa sasa hata wakiwasiliana na makao makuu yao wanambiwa wasubiri tamko la serikali.