Hatma ya UKAWA Juni 27, 2015

Hatma ya UKAWA Juni 27, 2015

Siasa zinabadilika na wakati. Kuna wakati wa kuungana na kuna wakati wa kila chama kufanya mambo yake.

Lengo la ukawa limetimia, katiba mpya imekwama.

Kutokana na mazingira ya sasa kikatiba ni vizuri ukawa wakafanya maridhiano wakaenda katika kampeni za uchaguzi kila chama kikiwa na mgombea wake wa nafasi husika. Halafu baada ya kampeni kwenye sanduku la kura mgombea atakaye onekana kuwa na nguvu aungwe mkono na wenzake wa ukawa kwa maridhiano.

So maridhiano ndani ya ukawa kwa wakati huu ndio muhimu kuliko kusimamisha mgombea mmoja.

Baada ya uchaguzi watangalia walichovuna. Ndiposa watafanya maaumuzi mengine

well said!
 
Akizungumzuia suala hilo ,Mbatia alisema siyo kweli hakuna mwanachama yeyote wa NCCR mwenye fikra za kujitoa ndani UKAWA.Halmashauri KUU haijaitishwa kwa ajili kujadili kujitoa UKAWA.
CCM WANAANDAA KILA MBINU ZA KUIVURUGA UKAWA LAKINI HAWATAFANIKIWA.

Hawa MACHICHIEM ni kama FISI wanasubiria mkono wa binadamu udondoke.............
 
Akizungumzuia suala hilo ,Mbatia alisema siyo kweli hakuna mwanachama yeyote wa NCCR mwenye fikra za kujitoa ndani UKAWA.Halmashauri KUU haijaitishwa kwa ajili kujadili kujitoa UKAWA.
CCM WANAANDAA KILA MBINU ZA KUIVURUGA UKAWA LAKINI HAWATAFANIKIWA.
NCCR siyo Mbatia, chama kina wenyewe hicho wakimamua watajitoa tu. Hata CUF wanasema hivyo hivyo.
 
Hili nimelishuhudia kawe urafiki Wa mashaka haufiki mbali
 
Tatizo ukawa chadema wanajiona wao ndiyo kila kitu na watagawana fito tu kwa mwenendo huo.
 
Sikio la kufa halisikii dawa, UKAWA wanavurugwa na CHADEMA.
 
migogoro iko CCM kati ya mamvi na joka la mdimu,Makongoro na mamvi,Wassira na Makongoro, Mwigulu na Nyalandu ilimradi vurugu tu!
NCCR Mageuzi wameshtuka mnataka muwape majimbo machache tena yale tasa kama Ilala.
 
Kama kila kiongozi wa chama ndani ya ukawa anakanusha habari hizi, kwa nini muandishi wa mada hii asiwe role model wa uzushi Tanzania ili awekwe maabara awe specimen kwa ajili ya wanafunzi?

Shame on you and your big head.
 
Tutafika tu, tunajua CCM kwasasa wanatumia kila tone la jasho na shilingi UKAWA ianguke KAMA walivomtumia ZITO Zuberi Kabwe CHADEMA ianguke, Mungu yupo Upande wetu hawawezi
 
Naona huu umoja wa ukawa unawanyima vibaraka wa ccm usingizi sana ... asubuhi nimemuona mzee mkinga akitokwa na povu channel ten mpaka namuonea huruma ... eti ukawa utavunjika maana hautambuliki kikatiba na pia hawawezi kukubali mmoja agombee uraisi maana hawataweza gawana pesa za ruzuku ... this has been his standing point over and over again ... huku akimshukia lowassa ... sijui nani kamtuma huyu mzee
 
Siyo changamoto ni mgogoro ndani ya Ukawa.

Mkuu tatizo kubwa la ndugu zetu hao linatokana na viongozi wao kugubikwa na ubinasi uliyo kithili, watavurugana wenyewe kwa wenyewe na mwisho wa siku kila chama kitakwenda njia yake, mkuu narudia - si rahisi jamaa hawa wakapendekeza mgombea mmoja - si rahisi!!!
 
Bora NCCR Mageuzi wajiondoe tu.

Inawatesa dah hadi huruma maana kwa hakika mnajua mwaka huu, kazi iko

Kuna facts ambazo lazima ziwape presha.

Kwasasa Upinzani una nguvu- Lowasa, kikwete wamekiri hili hadharani mara nyingi

CCM inakabiriwa na Matatizo ya Ndani- hii haina Siri hata wewe unajua

CCM huku uraiani sasa wengi wananchi hawaiamini kama miaka ya 95

CCM ina misuguano na makundi ya kijamii mengi- madereva, machinga, walimu, wananchi, wachimba madini wadogo nk nk

Alafu VYAMA hivi vimeunga, - hii ni nguvu nyingine KuBWa ya kui defeat CCM

Tukiacha Propaganda UKWELI msiotaka usemwe mwaka huu ni mbaya na mgumu sana katika siasa kwa chama cha mapinduzi tangu uhuru
 
Kila kitu kipo vizuri ndani ya UKAWA, wala msiwe na wasi wasi Makamanda.

Mkuu tuache mahaba huo japo tunapenda ukawa ,Lakin
Mim naona huo muungano wanaishi kwa kuvumiliana tu ,ni swala tu la muda ,baada ya wk mbili turudi hapa
 
hivi wapinzani wapo tiyari kushinda utawala wa nchi hii?
 
NCCR siyo Mbatia, chama kina wenyewe hicho wakimamua watajitoa tu. Hata CUF wanasema hivyo hivyo.
Mwenyekiti wa NCCR taifa ni nani wewe gamba utakuwa chizi bure UKAWA haiwezi kuvunjika ccm ndo inakaribia kufa Lowasa ndo ameshikilia roho ya ccm kwa sasa
 
Pesa ya kumnunua hata Mbowe, Limpumba na Mbatia kuisambaratisha Ukawa CCM wanayo, sio ajabu ukawa ikatoweka ghafla. Hata hivyo, vyama vinavyounda UKAWA visitarajie muujiza kutoka UKAWA huwezi wewe kuwa na diwani mmoja ghafla uwe na madiwani 100 eti kwasababu ya kujiunga na UKAWA, hii haiwezekani kabisa, nguvu za asili za vyama vyenu katika maeneo husika lazima iwe ndio dira yenu na muongozo wenu katika kuachiana majimbo ya uchaguzi mwaka huu ndani ya ukawa. Watu siku hisi huwa wanachagua mtu na chama pamoja na sio chama pekee. Mgawane majimbo kwa usawa na isiwe sawa. Maana kuna tofauti ya usawa na sawa (equitably and equally, equity and equality). Equitably ni kugawana kutokana na jasho, rasilimali na kukubalika kwa mgombea na chama kulikowekezwa kwenye jimbo husika.
 
Hii habari nimeisoma mapema sana kunako gazeti la mwananchi ukweli kwa jinsi nilivyo na imani na huu muungano (UKAWA)nimeumia sana kusikia kuna mvutano, lkn nafurahishwa pia na hekima za hawa viongozi, hasa Kamanda Mbatia....jamaa ni mnyeyekevu na busara humtawala muda wote.
Ombi langu kwa UKAWA hasa Chama changu CDM kidogo sie ndio tunalalamikiwa kuwa tumechukua majimbo mengi, kama sio shida basi hayo 13 yaliyobaki tuwape wengine maana kwa utazamaji wa karibu ni wazi CDM ndio itatoa mgombea urais, tupo chini ya miguu yenu makamanda, Watanzania wanawahitaji wakati huu kuliko wakati wowote katika historia ya Nchi hii.
Mungu awabariki munapozidi kufanya tafakuri kuelekea October.
 
Back
Top Bottom