Hatma ya ubunge wa mbunge wa Meatu (CHADEMA) kujulikana kesho Jijini Dar es Salaam

Scolari Ndenga

JF-Expert Member
Aug 4, 2008
271
43
Wadau,

Kesi ilifunguliwa na wanachama wa CCM kupinga matokeo ya ubunge wa Meashaki Opulukwa wa jimbo la Meatu kupitia CHADEMA iliamuliwa na kumpa ushindi Meashaki Opulukwa kati kati ya mwaka jana.

Kama ilivyo kawaida, wanachama wa CCM wa huko Meatu walikata rufaa na rufaa hiyo inatarajiwa kuamuliwa kesho saa mbili asubuhi kwenye mahakama ya rufaa jijini Dar es salaam kama ilivyokuwa kesi ya lema.

Nini kitajiri hiyo kesho, yetu masikio na macho kwani kuna hofu kubwa CHADEMA inaweza ikapata pigo la kuporwa ubunge
 
Chadema ishinde,isishinde hii,bado jimbo ni la chadema tu hatuna hofu wakitaka uchaguzi hawa magamba mi tapenda zaidi ili tukayavue vizuri sumbawanga,igunga na meatu ngoma inogile.
 
Kesho mahakama inawazika rasmi hao wanaccm waliokubali kutumiwa kama ndomu. Aibu iliyowakuta waganga njaa wa Arusha dhidi ya Lema ndiyo inakwenda kuwapata hao wa meatu.
 
Kesho mahakama
inawazika rasmi hao wanaccm waliokubali kutumiwa kama ndomu. Aibu
iliyowakuta waganga njaa wa Arusha dhidi ya Lema ndiyo inakwenda
kuwapata hao wa meatu.

kwahiyo hutaki wananchi watumie haki yao ya kikatiba? kama hawakuridhika wanayo haki ya kukata rufaa na wameitumia kama walivyoitumia wale wa jimbo la segerea. tumia busara kaka
 
Back
Top Bottom