Farudume unakiri kuwa mapinduzi yalifanywa na watanganyika?. Unakubali kuwa mauwaji ya wazanzibari yalifanywa na watanganyika?. Tukienda "the Hague", upo tayari kutoa ushahidi?.
Hivo katika ndoto yako ipo nafasi kuwa Sultani atarudi kuitawala Zanzibar?. Jee, wazanzibari wanataka Sultani arudi?. Na kama wanamtaka kuna makosa gani?. Acha ulimbukeni. Sultani alikuwa mzanzibari kama mzanzibari yeyote yule. Hapo Tanganyika hakuna watu wenye asili ya kiarabu au kihindi?. Munawaua?. Au ndio wenye kuwapa ajira asilimia kubwa ya watanganyika. Nakushangaaa sana.
Ndugu yangu Mapinduzi yoyote yanayohusisha Silaha lazima yawe na Umwagikaji Damu.Mara nyingi Damu ikimwagika huwa inaleta Ukombozi.Hata Vitabu vya Dini vinaeleza hivyo.
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar nayo yalimwaga Damu lakini tulimwondoa Sultani ambaye alikuwa anawadhulumu ndugu zetu wa Zanzibar.Hivi sasa Zanzibar chini ya Himaya ya Tanganyika(Tanzania) ni Salama sana kuliko Enzi ya Mwarabu.
Waarabu waliopo Tanganyika hawana Ubavu wa Kutesa Watu kama alivyokuwa akifanya Sultani.
Kwa kuwa Zanzibar bado haijiwezi Kijeshi LAZIMA iendelee kuwa Chini ya Usimamizi wa Tanganyika ili kuzuia Tishio la Waarabu kurudi kwenye Utawala Zanzibar.