Mashaxizo
JF-Expert Member
- Jun 13, 2013
- 6,707
- 3,360
Inaeleweka raisi Kikwete ndie aliependekeza mabadiliko ya katiba, na kwa mawazo yake alidhani ingekuwa issue ndogo licha ya kukutana na baadhi ya vikwazo! But kwa mtazamo wangu nahisi amefanya kitu ambacho anaweza/ameanza kukichukia! Hii ni kutokana na yale aliyoyakusudia kwenda kinyume!
kikwazo namba 1 ni pale Wazanzibari walipokataa kutokujadiliwa kwa mambo ya Muungano na muungano wenyewe! (kumbukeni pale mswada ulipochanwa ndani ya baraza la wawakilishi kule visiwani Zanzibar)
hule msemo 'maji ukishayavulia ni lazima uyaoge' ulifanya kazi na kuruhusu kujadiliwa kwa mambo ya muungano na muungano wenyewe!
...
Ktk bunge la katiba kumezuka issue moja ngumu na kusababisha mambo mengine yawe magumu vilevile.
Hapa naongelea muundo wa muungano/serikali umeleta mzozo kwa upigaji kura, either ya siri or ya dhahiri, CCM wamekua hawaaminiani kiasi kwamba wanataka kuvunja misingi ya kidekrasia ili tu yapite yale yaliomo ktk sera zao, na kwa uwengi wao walidhani wangefanikiwa vizuri!
Hata hivyo wamekwama kutokana na sheria ya mabadiliko ya katiba inataka 2/3 itumike ktk kupitisha vipengele vya katiba hiyo!
2/3 imekuwa ni kigezo kigumu kupitisha wanayoyataka kutokana na upinzani na usaliti wa wenyewe kwa wenyewe (CCM)! Na pia 2/3 ipite kwa wabunge na wajumbe wa Tz bara na Z'bar!
Hii imedhihirika kule Dodoma ambapo wanaotaka serikali mbili na wanaotaka serikali tatu wameshindwa kufikia 2/3!
Ni nini hatma ya utata huo?
Hatma yake ni mbaya kutoka na upinzani na hakuna upande unaotaka kukubali kushindwa na ukizingatia Wazanzibari hawatakubali serikali mbili! Hapa naweza kusema hata bungeni wakikubaliana serikali mbili haiwezekani Wazanzibari kupitisha hili (ikumbukwe mwisho wa siku ni wananchi ndio wanapitisha!)
Na kwa mujibu wa sheria ya mabadiliko ya katiba, inasema: katiba itapigiwa kura na wananchi, ikifeli, itarudi tena bungeni kwa marekebisho na baadae ipigiwe tena kura na wananchi, ikifeli tena, tutaendelea kutumia katiba iliyopo! na ni hapa ndipo kwenye utata huku CCM wakiamini itakuwa ni afueni kwao kitu ambacho sio kweli!
Jee wananchi wa Tz bara na visiwani watakubali kuendelea na katiba iliyopo?
Ukizingatia Z'bar wameshafanya mabadiliko ya katiba yao ya mwaka 2010 ambayo inapingana na katiba ya Jamuhuri ya Muungano?
...
My take:
CCM msitake kuifanya Tz kama uwanja wa mapambano na kuwapa faida mabepari!
Kwa hali ilivyo, ni kukubaliana tu na matakwa ya wapinzani, kama haiwezekani Muungano uvunjwe!