Hatma ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar iamuliwe na wananchi

Sep 27, 2023
10
28
Kumekuwa na manung'uniko mengi linapokuja suala la muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar huku kila upande ukionesha kutoridhishwa na muungano huu.

Suala la muungano tangu kuanza kwa kwake mpaka sasa limekuwa likitawaliwa na maamuzi ya watu wachache ( Elites), huku mawazo na mitazamo ya wananchi kutoka pande zote mbili (2) kutochukuliwa kwa uzito.

Wanzanzibar na Watanganyika wapewe nguvu ya kuamua juu ya hatma ya muungano, aidha kuvunja au kuendelea na muungano na aina ipi ya muungano waitakayo.

Kwa mifano Juni 23, 2016 Uingereza iliitisha kura ya maoni ya kitaifa ya kujitoa Umoja wa Ulaya ambapo wananchi 17,410,742 sawa na 51.9% walipiga kura ya Ndio, na 16,141,241 sawa na 48.17% walipiga kura ya hapana na hivyo serikali ya Uingereza ili heshimu mawazo ya wengi (wananchi) na kujitoa Umoja wa Ulaya, Septemba 18, 2014 Scotland iliitisha kura ya maoni, yenye swali.

"Je, Scotland iwe nchi huru?"
Wananchi 2,001,926 sawa na 55.3% walipiga kura ya hapana na 1,617,989 sawa na 44.7% walipiga kura ya Ndio na hivyo Scotland kuendelea na muungano huo.

Maoni yangu ni kwamba, hatma ya muungano isiamuliwe na watu wachache ( Elites) badala yake Iamuliwe na wananchi kwa kura ya maoni.

Ahsante.
 
Zanzibar ina historia yake tofauti kabisa na Tanganyika. Muungano wowote wa Serikali moja utaharibu historia ya watu wa Zanzibar.

Muungano bora ni wa Serikali 3, ya Tanganyika huru, Zanzibar huru na ya Shirikisho. Kama ikifika mahali Muungano haufai au nchi wanachama haziridhiki basi ile ya Shirikisho inakufa bila kuathiri pande zingine kama ilivyotokea USSR na Yugoslavia mwanzoni mwa miaka ya 1990s
 
Zanziba ilikuwa nchi kabla ya 1964 na Muungano tuliokuwa nao ni "marriage of convenience" kwa wakati ule kwenye kipindi cha vita baridi (NATO/ Warsaw Pact).

Ni USA kupitia kachero wao Frank Carlucci aliyekuwa Balozi wao Tanganyika kisha Congo na baadaye akaja kuwa CEO wa CIA. Huyu Carlucci alianza kumshawishi kwanza Jomo Kenyatta kutaka kuiunganisha Zanzibar na Kenya. Jomo Kenyyatta atakataa ndipo akamu approach J K Nyerere ambaye alikubali.

Nyerere aliweka muundo wa Serikali 2 ili kutoimeza Zanzibar kama nchi. Alikataa kabisa kuifanya Zanzibar kuwa Mkoa. Hata hivyo vita baridi ilikwisha mwaka 1989 baada ya kuanguka ukuta wa Berlin. Ushahidi upo kwenye Rasimu ya Katiba ya Warioba uliotaka Serikali 3.

Yeyote anayetaka ridhaaa ya kura za Wazanzibari lazima aongelee "sovereignty ya Zanzibar" as a country.

Zanzibar ilikuwa tajiri sana kuliko Oman kabla ya mwaka 1960 na ndiyo sababu Sultan Seyyid Said alihamisha Makao makuu ya Sultanate of Oman kwenda Zanzibar mmamo 1840. Mwaka 1960 kwa mfano Zanzibar ilikuwa na kilometres 22 za barabara ya lami wakati Oman ilikuwa haina. Leo hii Oman ni nchi tajiri sana baada ya kugundua raslimali za mafuta mpaka imekuwa nchi mfadhili.

Mimi ni Mtanganyika naamini kuwa muda wa kuendelea kuishikilia Zanzibar umekwisha. Tuwaache wapate maendeleo kipitia OIC na waanzishe bandari huru kama ulivyo Singapore au Dubai.
 
Huu muungano ufutwe. Haiwezekani:-

A. Mzanzibari anaruhusiwa kugombea nafasi yoyote huku bara ikiwemo urais, lkn mtanganyika haruhusiwi hata kuwa mjumbe wa mtaa kule Zanzibar .
B. Mzanzibari anaruhusiwa kununua ardhi kiasi chochote huku bara, lkn mtanganyika haruhusiwi kununua na kumiliki ardhi Zanzibar .

Muungano gani huu???!
 
Umevimbiwa nini ktk mfunguo huu wa Ramadhani?
 
Na kura ya maoni ikipigwa isichakachuliwe
 
Na hiyo kura ikipigwa, utayakubali matokeo kama yataonesha Watanzania tulio wengi tunaupenda Muungano? Au mtaloloma kama mnavyololoma kuibiwa kura kwenye Uchaguzi Mkuu wakati hamuendaGI kupiga hizo kura mnazoibiwa?
 
Naunga mkono hoja uvunjwe hauna maana yoyote kwa bara
 
Kuna ukweli tunatotakiwa kuufafanua na kama ni kero irekebishwe kama kweli tunafikiri muungano huu ni wa muhimu.

1. Wazanzibar wengi sana wanamiliki ardhi na majengo bara, kama raia. ila Wabara wanachukiwa wakienda kule, wanaitwa chogo, na katiba yao inazuia watu wa bara kumiliki ardhi. Juzi nilikuwa Dodoma, kwenda benjamin Mkapa kwenye kona ya Udom, kuna migorofa fulani hivi imejengwa, wanasema karibu na vile vijengo vya majaji, wengine wanamtaja mzanzibari fulani anamiliki hiyo migorofa. tukisema wazanzibar leo hii muungano umevunjika waondoke, wengi wataanza kuuza nyumba nyingi na ardhi kubwa wanayoimiliki. KWANINI BARA HATURUHUSIWI KUMILIKI KULE? faida yao ni nini?

2. kwenye ajira, hii ni kero, wazanzibar maelfu na maelfu wameajiriwa bara, hata kwenye mambo yasiyo ya muungano, wameajiriwa bara ambayo kiukweli ipo bara kwasababu zanzibar kuna utawala wao, lakini wabara hawaruhusiwi kabisa kuajiriwa zanzibaar, hii ni kero, inatakiwa iondolewe, ama la kila mtu abaki kwake.

3. wazanzibar wanakuwa wabunge kule kwao, na huku. akiwa mbunge kule kwao, atakula masurufu ya kule na atakuja kula masurufu ya bara kwa kodi za watu wa bara. tuambieni, yale mipesa wanaku wabunge 50 wa zanzibar wanakiula, zanzibar huwa imechangia bei gani? ni pesa za walipa kodi wa bara. na hao hao wakifika huku wakishiba, wanasenma twende kule kwa passport, kwa msiojua, kile ameongea yule mbunge wa zanzibar kwamba wabara twende kwa passport kwao ndicho kilichopo kwenye mioyo ya wazanzibari wote hata wenye mamlaka huku na hata walioajiriwa huku na hata wanaomiliki ardhi huku, amesema kilichopo kwenye mioyo ya wengi. wala hatakiwi kulaumiwa. kwa waliofika zanzibar wanajua kuwa hicho ndio huwa matamanio yao.

4. mzanzibar anaweza kuwa Mkuu wa wilaya, mkoa, na waziri bara, ila sisi kule marufuku. kwanini?

nimeongea hayo kwa uchache tu, lakini ukweli mwingi hata wanaopinga wanaujua, kama tunataka muungano uwepo, ondoeni kero hizi kwa watu wa bara, ama la, kila mtu achukue hamsini zake kwasababu hakuna kitu wabara wanafaidika nacho as of now. na hawajawahi kufaidika. watu wasioelewa watasema huu ni uchochezi, ila jibuni kwa hoja kama mnazo.
 
Mambo madogo sana haya. Watanzania tuko 61 Million na ardhi yetu ina 945,000 Sqaure kilometres za ukubwa.

Zanzibar wako 1.2 Million na ukubwa wa 2,460 Square kilometres.

Ni aibu leo watu 61 Million kuanza kugombea ki-ardhi kidogo namna hiyo wakati huku kumejaa mapori makubwa ya kutisha.

Hizo fursa za kazi unazozitaka ZNZ ziko wapi? Kama elimu yako na uwezo wako hauwezi kukupatia ajira hapa Bara penye uchumi wa GDP ya USD 85 Billion ndiyo ukabamane na GDP ya ZNZ ambayo USD 3.75??

Tunahitaji kubadilisha mtazamo tu. Tatizo letu kubwa ni umaskini. Zanzibar ingekuwa tajiri kama Qatar, mengi ya yanayosemwa wala isingekuwa issue. Kama sikosei, Area Commissioners from Zanzibar au positions nyingine zimepewa Watu wa upande mwingine wa Mwungano toka enzi za Mwalimu.

Na hizi feelings zikipewa nafasi, zinaweza hata kuleta issues kati ya movements za watu mikoani. Kuna watu, suddenly, watadai wakuu wa mikoa, wilaya, watoke katika mkoa huo huo.

Mikoa kama ya Mbeya, Mwanza, Kilimanjaro, Arusha ina mchango mkubwa kiuchumi kuliko mikoa mingine kama Tabora, Singida, Kigoma, Mtwara. What if hao wenye uchumi mkubwa wakaona wanannyonywa au kutawaliwa na watu wa mikoa maskini?
 
Sipendi muungano, Siwapendi wazanzibar nawachukia kutoka moyoni. Huyo aliyeunganisha sisi na wale watu alikosea sana. Muungano uvunjwe haraka sana
Kama hupendi Muungano, hama nchi au kufa tu, there is nothing you can do dogo!! Muungano is here to stay.

Hata Seif Shariff Hamad, Christopher Mtikila, Aboud Jumbe, Haji Faki, Njelu Kasaka na wengine wengi hawakuupenda muungano na walikuwa na maneno ya shombo kuliko wewe. Wao wamekufa na muungano unaendelea
 
Huu muungano uvunjwe hauna faida yoyote kwa bara
Huko United Kingdom, Scotland inatamani ijiondoe kwenye Muungano lakini wanakataliwa. Wales na Ireland pia wanajiona wanahitaji kuwa sovereign lakini hawajarusiwa kuwa independent.

USA zile states 51 ziliunganishwa kwa civil wars miaka ya 1700. Kwa nini wasiziache ziwe pekee?

Russia leo inapigana na Ukraine kutetea wananachi wa Ukraine wenye asili ya Russia kwenye majimbo ya Luhansk na Donestk, yote ni kujiimarisha.

Akina Tundu Lissu au Jussa ni wachache kuliko wengi wanaopenda Muungano.

Mfumo aliouweka Nyerere ulikuwa na faida zake na hasara zake. Kikubwa ni kuzipima tu whether hasara ni kubwa kuliko faida
 
HOJA NI KWAMBA, kwanini tusifute tu hivi vinnchi viwili, tuwe na moja tu na zanzibar iwe MKoa? tuwe na rais mmoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…