Hatma ya mradi Stiegler’s Gorge: Hatakama hatukubaliana kiitikadi, tukubaliane katika Ushauri wa kitaalam

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Mimi sio nabii, lakini angalau nikisema jambo nakuwa nimeona kijacho mbeleni, Naomba nikukumbushe jambo muhimu ambalo niliandika 13 March 2019 katika makala hii chini.

Katika makala hii nilianza kwakusema, "Vita vya Kiuchumi Tanzania chini ya mradi mtambuka wa maporomoko ya Rufiji, siasa ya Mazingira duniani na muundo na mienendo ya Shirika la Elimu, Sayansi na Udhibiti wa Mazingira duniani (UNESCO), vinanipa sababu ya kuiponeza TISS katika ulimbe huu wa vita vya kiuchumi.

Bonde la Rufiji liko kwenye urithi wa dunia kwamjibu wa Shirika la Uhifadhi wa Mazingira (UNESCO), Na hivyo ulinzi wa bonde hili ni kwa sheria za kidunia sio kwa sheria za Tanzania, hapa ndipo ambapo nataka kusifu idara za ujasusi na kumsifu Rais Magufuli kwa kuishinda dunia dhidi ya misimano na sera za mashirika haya ya kidunia ambayo Mwalimu yalimshinda, Mwinyi yalimshinda, Mkapa yakamshinda, Kikwete yakamshinda.

Kwa wiki kadhaa nimekuwa nikipitia nyaraka za kijasusi za mashirika na taasisi mbalimbali ulimwenguni (Realiised docs), nimejiridhisha kuwa vita nikubwa kuliko wengi wanavyofikiri, na ikiwa mradi wa umeme bonde la Rufiji utafanikiwa, basi TISS itaingia kwenye historia ya mashirika bora kabisa ulimwenguni kwa counter intelligence hii. Palipo na uthubutu lazima tupongeze.

Awali mradi huu wa Umeme wa Stiegler's Gorge Ethiopia walikubali kujenga, lakini hakuna maelezo kama waliishia wapi ama walishindwa tenda. Zikawepo taarifa za Waturuki kuwa watajenga, nazo zikaishia hewani. Kisha tukashuhudia Arabb Contractors wa Misri wakisaini mikataba ya ujenzi. Bado ujenzi rasmi haijaanza, lakini hatua tu ya kuthubutu kusaini mkataba ni hatua kubwa inayostahili kupongezwa.

Bunge la Ujerumani liliweka azimo kuitaka serikali ya nchi hiyo kuzuia ujenzi wa mradi huo wa Rufiji na badala yake serikali ya Ujerumani isaidie kujenga vinu vya gesi kwaajili ya nishati ya umeme. Kwakuangazia jambo hili watu wengi wanaweza kujiuliza, itakuwaje nchi ya Ujerumani iingilie masuala ya ndani ya Tanzania? Mifumo ya kijasusi iko hivi, kwamjibu wa Nyaraka za idara ya ujasusi ya nchini Lithium (Anual report 2016) inaonyesha kuwa Ujerumani pekee ina majasusi 11 wa ngazi za juu ndani ya UNESCO, na kwa nadharia hiyo, Ujerumani ikitaka kuzuia miradi yoyote yenye uharibifu wa mazingira inatumia msukumo wa UNESCO.

Kinachoweza kutokea ni kuwa UNESCO inaweza kuiandikia barua ya katazo nchi husika kwamba pale ni sehemu ya Urithi wa Dunia (World Heritage site.) na hairuhuriwi kupajenga. Na wanaonya kuwa ukiwa mbishi na ukaendelea kujenga utakuwa black listed. Na kampuni inayopata tenda ya kujenga nayo inapewa barua na kuonywa kuwa itakuwa black listed na Bank Account zako zitakamatwa. Kwakufanya hivyo wanashinikiza kampuni zijitoe katika mradi husika.

Majasusi hawa wamefanya hivyo kuidhibiti Iran, enzi za Reza Khan kwakutumia mashirika haya ya kidunia , ambayo mengi ni mashirika ya kijasusi. Pia nchi za Panama zimewahi kukumbana na nguvu ya mashirika haya.

Kwa namna yoyote naipongeza Serikali kwa ujasiri huu wa kufunga masikio na kelele za kidunia na kuamua kuanzisha mradi huu uliokwamba tangu miaka ya 60+. Hii ni hatua kubwa sana na ninaamini itaacha legacy kubwa sana kwa rais Magufuli na kwa vyombo vya ujasusi nchini ikiwa utafanikiwa, ingawa hakuna nchi au kikundi kilichowahi kushindana na mashirika haya ya kidunia na kikashinda, zaidi ya hapo labda ziwe ni siasa za kura. Bado naamini tumethubutu pakubwa sana, na katika ndoto tutashinda". Makala iliishia hapo.

Sasa mwaka mmoja na baadaa ya makala hii, Kampuni iliyokuwa ikijenga mradi huo imeandika taarifa hii ambayo inajumuisha ndani yake katazo la UNESCO. Isome hapa kwa lugha ya kitumwa....>>> ElSewedy Electric Co - Council on Ethics

Unaweza kujipa nafasi ya kusoma kwa undani zaidi kitabu cha Ujasusi kujua nama Ujasusi dhidi ya Ujasusi unavyofanya kazi na mifano hai toka katika viunga vya dunia ya ujasusi.

Nunua Kitabu kwa Ofa ya Mwezi Mtukufu na #Corona kwa 25,000 tu popote ulipo. Badala ya bei halisi ya 80,000/=

Nunua kwa Mpesa na Tigopesa 0715865544/ 0755865544 (Yericko Nyerere) kisha tuma majina yako na mahali ulipo.

Kwa Dar kitabu kitaletwa ulipo bure. Nje ya Dar nauli ni 8,000/=
 
Huwezi kushinda kwenye soko la dunia kama competitive advantage yako iko chini.

Hichi kisingizio cha mazingira mbona kwao wao wanajenga?

Tatizo letu tuna midomo sana . Ethiopia walipokuwa wanajenga walikaa kimya. Wananchi wao walichanga kupitia government bonds.

Sisi tuliitangazia dunia vita. Hilo ndo kosa letu.

Wazo zuri la maendeleo kwa taifa ila ulimi umetujengea maadui!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wasitubababishe wao.mazingira yao walifyeka yote wakajenga viwanda ulaya na marekani mbuga zao zote wanyama wakawamaliza Sasa wanakomalia wa kwetu waende zao huko.

Ohh urithi wa dunia!! Huo ni urithi wetu Watanzania tuna Uhuru wa kufanya chochote na urithi wetu.

Tuna Uhuru wa kuwafanya chochote wanyama wetu tukawala au tukawapiga kibiriti ni wa kwetu sio wao na miti Ni yetu sio yao watukome.

Hakuna cha utaalamu Hapo ni ukoloni tu.mamboleo wanataka tuwe tunakodi mitambo yao ya kufua umeme maruhuni wakubwa Hilo litabu ni takataka.
 
Wasitubababishe wao.mazingira yao walifyeka yote wakajenga viwanda ulaya na marekani mbuga zao zote wanyama wakawamaliza Sasa wanakomalia wa kwetu waende zao huko

Ohh urithi wa dunia! Huo ni urithi wetu watanzania tuna Uhuru wa kufanya chochote na urithi wetu.

Tuna Uhuru wa kuwafanya chochote wanyama wetu tukawala au tukawapiga kibiriti Ni wa kwetu sio wao na miti ni yetu sio yao watukome

Hakuna Cha utaalamu Happ no ukoloni tu.mamboleo wanataka tuwe tunakodi mitambo yao ya kufua umeme.
Kama ule ukoloni wa watu weusi dhidi ya weusi wenzao unaondelea hivi sasa katika nchi fulani ya giza.
 
Mbwa kweli wewe, una urithi gani ilhali hata unapopaita petu mzungu kakuchorea ramani hadi ukajijua uko wapi? Una urithi gani kunguni wewe bila mzungu kukuzungushia duara ungekua na nchi?

Pambafu
Wasitubababishe wao.mazingira yao walifyeka yote wakajenga viwanda ulaya na marekani mbuga zao zote wanyama wakawamaliza Sasa wanakomalia wa kwetu waende zao huko

Ohh urithi wa dunia!! Huo ni urithi wetu watanzania tuna Uhuru wa kufanya chochote na urithi wetu

Tuna Uhuru wa kuwafanya chochote wanyama wetu tukawala au tukawapiga kibiriti Ni wa kwetu sio wao na miti Ni yetu sio yao watukome

Hakuna Cha utaalamu Hapo ni ukoloni tu.mamboleo wanataka tuwe tunakodi mitambo yao ya kufua umeme maruhuni wakubwa Hilo litabu ni takataka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ewe jasusi uchwara Ethiopia wanajengewa bwawa lao na Waitaliano halafu wangekuja kutujengea sisi?!

Ewe jasusi uchwara unayelima bamia Mbutu unawezaje kujua sehemu Ujerumani walipoweka majasusi wake duniani?

Ewe jasusi uchwara intelegensia yako inasemaje kuhusu kushindwa kwa bomba la gesi kutuletea umeme wa kutosha kama tulivyoahidiwa?
 
Ukiwa unalalamikiwa na watu,ni wazi utakuwa mtu wa mikosi tu.
Hahaha mtu mwenye mikosi anawezaje kufika mbali hivyo kwenye career yake? Amepitaje huko koote mpaka kuwa Top Boss? I mean from zero to hero? Mimi nafikiri wewe ndiyo mikosi imekuandama na kukukwamisha kufika popote katika maisha yako na umebakiza chuki na wivu tu kama Wamarangu wenzako.
 
Huwezi kushinda kwenye soko la dunia kama competitive advantage yako iko chini.
Hichi kisingizio cha mazingira mbona kwao wao wanajenga?
Tatizo letu tuna midomo sana . Ethiopia walipokuwa wanajenga walikaa kimya. Wananchi wao walichanga kupitia government bonds.
Sisi tuliitangazia dunia vita. Hilo ndo kosa letu.
Wazo zuri la maendeleo kwa taifa ila ulimi umetujengea maadui!!

Sent using Jamii Forums mobile app

Hivi hata tusingetangaza hao maadui wasingeona huo ujenzi?
 
Back
Top Bottom