Hatimaye Waziri Kapuya Afunguka Mwenyewe Live!!

Hatimaye Waziri Kapuya Afunguka Mwenyewe Live!!

Joined
Apr 27, 2006
Posts
26,584
Reaction score
10,464
-
The Biggest IQ, Ijumaa Wikienda, lilimsakanya Kapuya mpaka kijijini kwake Kaliua, Urambo, Tabora na kwa juhudi hizo, sasa linakuwa la kwanza kuzungumza na kiongozi huyo ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.
Akifunguka kikamilifu kuhusiana na ‘saga’ hilo, kwa sauti imara bila wasiwasi, Kapuya alisema kuwa anamjua mwanafunzi husika, kisha akasema:
“Kuna watu wanamtumia. Hili suala limetengenezwa ili kuniharibia malengo yangu.”
ACHAMBUA UTAPELI WA MWANAFUNZI
KESI A; Mwanafunzi aliyedai kubakwa, alinukuliwa mitandaoni akisema kuwa yeye ni mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Turiani, Magomeni, Dar es Salaam.
Kapuya anapangua: “Huyo muongo, alinifuata kuniomba ada ya chuo. Aliniambia anasoma Chuo Kikuu cha Tumaini.”
KESI B; Mwanafunzi huyo alisema anasoma kidato cha tatu na alibakwa mara mbili na mheshimiwa huyo.
Kapuya anajibu: “Achilia mbali yeye, mimi sijawahi kubaka katika maisha yangu yote. Kuhusu kidato cha tatu, yeye mwenyewe aliniambia anasoma Tumaini University na aliomba nimlipie ada ya miaka miwili ambayo ni shilingi 3,000,000.
“Kwa mara ya kwanza nilimpa shilingi 2,300,000 na baadaye nilimpa shilingi 700,000. Kipindi hicho nilikuwa sijagundua kama ni tapeli, ila baadaye nilipogundua utapeli wake, nilihakikisha hanisogelei. Hapa nawajua watu wengi aliowatapeli.”
Kuthibitisha anachokisema, Kapuya alitaja jina la mkurugenzi wa benki moja nchini (jina tunalihifadhi) kuwa alishalizwa na mwanafunzi huyo.
KESI C; Denti huyo alidai ana umri wa miaka 16.
Hilo nalo Kapuya analipangua hivi: “Hata mimi mwanzoni aliponifuata nilijua ni binti mdogo, yatima anayehitaji msaada lakini ukweli ni kwamba yule ni mama mzima na ana mtoto. Ameshazaa yule.
“Hasomi popote, Mungu amemsaidia kuwa na umbile dogo ambalo analitumia kuwatapeli watu kwamba ana umri wa miaka 16, ni tapeli mkubwa, tena wa kuogopwa kabisa.”
KESI D; Mwanafunzi mwenyewe alidai kuambukizwa Ukimwi na kiongozi huyo aliyewahi kuongoza wizara mbalimbali nchini.
Kuhusu hilo, Kapuya alicheka kidogo halafu akajibu: “Sina Ukimwi, afya yangu ipo imara sana. Kama yeye ana Ukimwi, basi aseme mahali alipoutoa, siyo kusema uongo na kutaka kunichafua mbele ya jamii ambayo inaniheshimu.”
KESI E; Denti amedai kutumiwa SMS za vitisho kwamba mheshimiwa huyo amedai atamuua.
Hivi ndivyo Kapuya anavyojibu: “Sijawahi kutuma SMS za vitisho. Unajua haya mambo nashangaa sana, nipo huku kijijini Kaliua, kwa hiyo mambo mengi nafanya kuambiwa kwa sababu sipati magazeti kwa wakati.
“Nina laini tatu, Tigo, Airtel na Vodacom, hata siku moja sijawahi kutuma SMS ya kumtishia mtu kumuua. Hao wanaomuamini, waendelee kumuamini huyo tapeli lakini lazima nimfikishe kwenye vyombo vya sheria.”
KESI F; Yapo madai kuwa Kapuya alitishia kujiua baada ya kugundua ameshikwa pabaya na denti huyo.
Hilo nalo Kapuya alilijibu hivi: “Nimesema sijatuma SMS yoyote, wala siwezi kutishia kujiua. Nitishie kujiua kwa lipi?”
KESI H; Miongoni mwa madai yaliyotajwa ni kwamba Kapuya anajindaa kuwa waziri mkuu baada ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Kuhusu hili, Kapuya alicheka akasema: “Nilimwalika Lowassa (Edward) jimboni kwangu. Akiwa huku na maeneo mengine ya Mkoa wa Tabora, wananchi walisema mimi ndiye nitakuwa waziri mkuu wake.

“Yalikuwa ni maneno tu na mimi nilianza kuyasikia kipindi hicho. Kwa hiyo sijawahi kutamka popote kuwa mimi najiandaa kuwa waziri mkuu.”
MTAZAMO WAKE

Pamoja na kupangua madai yote hayo, Kapuya aliongeza kuwa yapo makundi mawili ambayo anayahisi kuwa ndiyo yapo nyuma ya denti huyo ambaye yeye amemwita ni mama mtu mzima.
Alisema: “Kuna majambazi fulani alikuwa anawatumia kunishawishi niwape pesa, baadaye waligombana. Wale majambazi walimwambia watamuua ikiwa yeye ataniendekeza.
“Nahisi hao ndiyo yupo nao kundi moja kuhakikisha wananichafua baada ya mimi kugundua uhuni wao ambao walikuwa wananifanyia. Nitakapoanza kuwashughulikia kisheria, itajulikana tu nani na nani anahusika nyuma yake.”
Aidha, Kapuya alimtaja mwanasiasa mmoja mwandamizi nchini (jina tunalo), mwenye asili ya Mkoa wa Tabora, mwanachama wa CCM kuwa anamhisi yupo ndani ya mkakati huo wa kumchafua.
“Ni hivi, … (anataja jina la mwanasiasa huyo), ameshapandikiza vijana wawili ili waniangushe kwenye Uchaguzi Mkuu 2015. Hao vijana wametengeneza tovuti ambayo imekuwa ikinichafua sana.”
MADAI YA MSINGI
Mwanafunzi huyo ambaye Kapuya amemwita ni mama mwenye mtoto, aliripotiwa na mitandao mbalimbali ya kijamii akidai kubakwa kisha kuambukizwa Ukimwi na kiongozi huyo.
Katika madai yake, mwanafunzi huyo alisema kwamba zahama hiyo ilimpata baada ya kwenda kwa Kapuya kuomba msaada wa ada ya shule ndipo kiongozi huyo alimgeuzia kibao.

chanzo:globalpublishers
 
Mkuu WJ Malecela, naona uko kila kona kila dakika kila mahali vehemently kumtetea huyu Kapuya. Mna uhusiano gani?
You seem to have suddenly became a staunch ally/supporter of mheshimiwa Kapuya.
I'm just curious.
 
Mkuu WJ Malecela, naona uko kila kona kila dakika kila mahali vehemently kumtetea huyu Kapuya. Mna uhusiano gani?
You seem to have suddenly became a staunch ally/supporter of mheshimiwa Kapuya.
I'm just curious.

- Mkuu chambua hoja zake kwanza ndio kazi ya great thinkers sio kutafuatana uchawi, chambua hoja zake kwanza!1

LE Mutuz
 
sasa hivi sijui watakuambiaje sasa langu jicho dole gumba na button zangu..
 
Bulahi Willy,mbona mzee hajajibu.maswali ya msingi??
 
Global ni Kiboko.....

Kapuya4.jpg


KHAA! MHE. KAPUYA - Global Publishers
 
Hiyo mikono si misafi hata kidogo
Kwa kumtazama tu utaliona hilo haihitaji mtu awe na upako kulijua hilo
 
bora mchawi kuliko mnafiki mnazidi kuharibu kapuya amebakaaaaa kweli mnaficha nn kwa huyu mwanafunzi ni mjinga kwanini asimtaje wasira akasema kapuya??
 
Sasa alichofunguka nini hapo ,kipi kwako kipya ..huwa napata shida sana kuamini kama kweli we ni mbegu ya Mzee John si bure mzee aliuziwa mbuzi kwenye gunia.maana akili yako haiendani kabisa na umri wako .lakini si bure mwalimu nyerere aliona mbali like father like son ndiyo maana alizimilia mbali harakati zake za kukimbilia magogoni baada ya kukopa mihela huko ghuba
 
willy, hii dhambi ya kueneza magonjwa itawatafuna mbele za Mungu, fanya muwezavo , badili stori, pindisha ukweli, yoooooote ayo ni kwa kuwa mna serikali na mshasema nyie mwenye nchi yao...hapa sisi wananchi tumechagua kuwapuuza kabisa...sitarudi kuchangia kwenye ushetani wenu huu.......safari njema ktk kuinajisi nchi yetu.....
 
- Mkuu chambua hoja zake kwanza ndio kazi ya great thinkers sio kutafuatana uchawi, chambua hoja zake kwanza!1

LE Mutuz



Sioni hoja hapo mkuu, kama 'alifunguka live' hayo mambo ya 'jina tunalo' ya nin? au mnaogopa kusema 'nimeambiwa, nimeelezwa'
 
le mutuz naona unaonesha jitihada kubwa sana kumtetea huyu mbakaji..hapa anasema anamfahamu vizuri sana huyo binti,lakini kwenye lile tamko lake kwa umma amesema hamfahamu kabisa(kama unabisha rejea kwenye hilo tamko,lipo humu jamvini) sasa tumueleweje huyu professor,cha zaidi hapo anazidi kutuaminisha kwamba njia ya muongo ni fupi,na ufupi wenyewe ndio kama huo wakujikanyaga.
 

From this...



...to this!

attachment.php


the same www.global publisherstz.com?

Kaazi kweli kweli, kwa lugha nyingine hii ni metamorphosis babu kubwa! Au ni evolution of Prof. Kapuya?
This is a typical case of Dr. Jekyll and Mr. Hyde syndrome...yangu macho!

 
Habari kaka William, mimi naomba kujua vitu vifuatavyo kutoka kwako

1. Una umru gani
2. Taaluma yako ni nini?
3. Umesomea wapi?
4. Una familia?
5. Iko wapi?
6. Sasa hivi unaishi wapi na unajishughukisha na nini?
7. Kabla ya kurudi TZ ulikuwa unaishi wapi na ulikuwa ukijishughulisha na nini?
8. Na kwanini uliondoka huko?
9. Mafanikio yako binafsi nini mpaka sasa?

Asante natumai utajibu kaka
 
Back
Top Bottom