Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,502
- 911,254
Wamachinga kuondolewa machinga Complex
na Nasra Abdallah
HALMASHAURI ya Jiji la Dar es Salaam imetoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara ndogo ndogo (wamachinga) waliogawiwa vizimba katika jengo la Machinga Compex kuanza biashara la sivyo watanyanganywa.
Msimamo huo ulitolewa jijini Dar es Salaam jana na meya wa jiji hilo, Dk. Didas Masaburi, alipotembelea jengo hilo na kukuta maeneno mengi yakiwa wazi.
Masaburi alisema iwapo wafanyabiashara waliogawiwa vizimba hivyo hawataanza biashara katika kipindi cha mwezi mmoja kutoka jana vizimba hivyo vitagawiwa kwa watu wengine.
Meya huyo alisema sababu ya wamachinga wengi kukimbia katika jengo hilo kutokana na kutokuwapo kwa biashara haina mantiki, kwani kuna takriban wamachinga milioni mbili mitaani hawana mahali pa kufanyia biashara.
Alisema biashara zilizopo hapo kila moja inategemea mwingine, akitolea mfano mama lishe wanategemea uwepo wa wafanyabiashara ili wauze chakula.
Dk. Masaburi ambaye alipata fursa ya kusikiliza kero zinazowakabili wamachinga wachache waliopo kwenye jengo hilo, alikataa ombi alilopewa na wafanyabiashara hao la kuwaondoa wenzao waliopo Soko la Mchikichini.
Alisema kuwa kuwaondoa wafanyabiashara waliopo Mchikichini na Ilala ni sawa na kuibua mzozo mwingine usiokuwa na maana kwani hata wakiondolewa hakuna sehemu ya kuwapeleka.
Kuhusu utozwaji wa kodi inayogharimu kiasi cha shilingi 60,000 kila mwezi, alisema watakaa na watendaji wa jiji waone ni namna gani wanaweza kupunguziwa hadi sh 30,000 kwa mwezi.