Hatimaye Wadachi wamewarudishia Wachina kampuni ya Nexperia

Hatimaye Wadachi wamewarudishia Wachina kampuni ya Nexperia

Xi Jinping

JF-Expert Member
Joined
Jun 14, 2023
Posts
9,545
Reaction score
28,711
Serikali ya Uholanzi imesitisha uamuzi wake wa kuingilia kampuni ya kutengeneza chipu, Nexperia, inayomilikiwa na China, baada ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili.

Mnamo Septemba, serikali ya Uholanzi ilisitisha kampuni hiyo kutokana na wasiwasi kuhusu usalama wa upatikanaji wa chipu barani Ulaya na madai ya matatizo ya uongozi ndani ya kampuni hiyo. China ilijibu kwa kuzuiwa kwa usafirishaji wa chipu hizo.

Lakini Jumatano, Uholanzi ilisema inasitisha hatua hiyo baada ya mazungumzo mazuri na China. Beijing iliikaribisha hatua hiyo na kusema ni mwanzo mzuri kuelekea suluhisho la tatizo.

Nexperia ni msambazaji muhimu wa chipu zinazotumiwa katika magari na vifaa vingine vya kielektroniki, na upungufu wake unaweza kuathiri uzalishaji duniani.

Awali, Uholanzi ilisema hatua yake ilichukuliwa kutokana na tuhuma dhidi ya aliyekuwa CEO wa Nexperia, kwamba alihamisha mali, fedha na teknolojia kinyume cha sheria kwenda kwa kampuni ya kigeni. Mahakama ya Uholanzi iliamuru kuondolewa kwake kutokana na madai ya usimamizi mbaya.

Wingtech, kampuni mama ya Nexperia, imekuwa kwenye orodha ya tahadhari ya Marekani kwa sababu za usalama, na pia imekumbana na vizuizi nchini Uingereza.

Baada ya Uholanzi kubadili msimamo, China ilisema bado kuna masuala ambayo hayajatatuliwa, hasa uamuzi wa mahakama uliomvua Wingtech udhibiti wa Nexperia. Wingtech imepinga madai yote dhidi yake na inataka serikali ya Uholanzi kuondoa rasmi usaidizi wake kwa kesi hiyo.


=======================================
The Netherlands has suspended its seizure of the Chinese-owned chipmaker at the heart of a six-week dispute between the EU and China that threatened to halt car production at sites around the world.

The Dutch minister of economic affairs, Vincent Karremans, said in a statement on Wednesday that the government would suspend its decision to take supervisory control of Nexperia as a gesture of “goodwill” to Beijing.

“In light of recent developments, I consider it the right moment to take a constructive step by suspending my order under the Goods Availability Act,” he said.

‘I’d do it all again,’ says Dutch minister at heart of car chip standoff with China

The seizure on 30 September had prompted a furious response from China, which in early October banned exports of Nexperia chips from the country, where most of them are packaged and finished.

That threw global carmakers’ supply chains into turmoil, leading to production pauses in Mexico and warnings from EU manufacturers that they were “days away” from stoppages.

Source: The Guardian

Soma Zaidi: Wadachi wameyatimba kwa Wachina, kuwa kibaraka wa Marekani kumeigharimu Ulaya
 

Attachments

  • 20251119_213611.jpg
    20251119_213611.jpg
    237.1 KB · Views: 37
Back
Top Bottom