Hatimaye wabunge wa Uingereza waungana kuhimiza wahusika kashfa ya rada kuwajibishwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye wabunge wa Uingereza waungana kuhimiza wahusika kashfa ya rada kuwajibishwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Amakando, Nov 30, 2011.

 1. Amakando

  Amakando Senior Member

  #1
  Nov 30, 2011
  Joined: May 9, 2011
  Messages: 158
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Serikali ya Uingereza iko tayari kusaidiana na serikali ya Tanzania kuhakikisha kuwa mtu mmoja mmoja walioshiriki katika wizi wa Rada wanafikishwa mahakamani hii ni kwa mujibu wa Bunge la Uingereza.
  Je Mzee wa Vijisenti atapona?
  Source Amka na BBC.
   
 2. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #2
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa ktk bunge la Uingereza wameungana kuhimiza wahusika wote wa kashfa ya rada inayohusiha kampuni ya BAE system kuiuzia Tanzania rada iliyogubikwa na harufu ya rushwa. Taarifa zinasema wabunge hao wanahoji sababu ya kampuni hiyo kuchelewa kurejesha kiasi cha hela iliyoahidi kuirudishia Tanzania.

  Kampuni hiyo imaesema hivi sasa inafanya mwasiliano na mashirika mabalimbali ya nchini humo yanayoshughulika na kutoa misaada Afrika ili kuona namna gani watasaidiana kuruidisha pesa hiyo Tanzania.

  Wabunge hao wamesema wako tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania ili wahusika woke wafikiswhe mahakamani.

  Source: BBC Swahili- Amka na BBC
   
 3. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #3
  Nov 30, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,675
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Nadhani wahusika wa kadhia hii wote wapo Uingereza si Tanzania. Mbona Waingereza ndio wanaumia zaidi kuliko sisi?
  Vipi wabunge wetu wana nafasi gani ktk hili, au wao ni kujadili posho na CHADEMA tu? Na seikali yetu je, basi iwaombe waingereza waisaidie kujua wahusika maana yenyewe haiwajui, na kama sheria zetu hazitambui kosa hili, basi hata sheria za Uingereza zitumike.
   
 4. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #4
  Nov 30, 2011
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapo inaonekana kuna mkono mrefu. Tumsubiri Hosea na felesh kujitokeza tena kumsafisha.
   
 5. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #5
  Nov 30, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Habari yenyewe ni hii:

  Tanzania urged to take action over BAE bribery claim


  A cross-party parliamentary group is urging the Tanzanian government to prosecute those guilty of corruption or bribery over the sale of a BAE Systems air traffic control package.

  The company, despite not being found guilty of corruption, has agreed to pay nearly £30m compensation to Tanzania.

  The International Development Committee also wants any others involved in the deal to face prosecution.

  Tanzania's government has pledged to pursue bribery allegations in court.

  The sale of a complex military air traffic control system by BAE Systems to Tanzania - one of the poorest countries in Africa - prompted an investigation by the Serious Fraud Office.


  BAE Systems agreed to pay compensation for failing to keep full accounting records of the deal. The money was meant to go towards education, paying for school books and equipment.

  But the Commons committee says it was appalled to find that the compensation has still not been paid.

  BAE Systems says it is now working with the Department for International Development as to how the money should be spent.
   
 6. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #6
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Serikali ya JMT ilishawasafisha watuhumiwa wote wakitanzania kupitia takukuru ispokuwa mhindi mmoja tu aliyekuwa dalali. Umesahau chenge alipogombea uspika. Wabunge "wetu" wa upinzani walipiga kelele since day one lakini wakaishia kuambiwa wana wivu wa kike! Kwa serikali hii ya ccm, tutaendelea kusubiri misaada tu hata tukilazimishwa kuwa mashoga maana vijana tumelala! Very sorry!!?
   
 7. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #7
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,696
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Jamani CHENGE IS UNTOUCHABLE, njia pekee labda KUMWONDOA DUNIANI. Simply because he knows TOO MUCH. He spent more than a decade as the Attorney General.., takataka zote za wakuu anazijua huyu. Nani msafi wa kumnyoshea mkono?
   
 8. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Ingefurahisha iwapo yule Cameroon badala ya kulazimisha mambo ya kipuuzi ya ushoga kwa nchi wanachama wa jumuiya ya madola angefanya la maana na ningempongeza kama atalazimisha serikali ya magamba kuwachukulia hatua zinazostahili wale wote waliohusika katika mpango mzima wa kuuziana rada. Na hapa tunajua sio mzee wa vijisenti pekee bali na vigogo wengine. Na hapa katika waliopewa mgao humkosi pia Mr. Clean.

  Najua serikali ya uingereza ina uwezo wa kulazimisha hili na ninavyoifahamu serikali ya magamba wanaweza kuchukua hatua za kuigiza lakini angalao watakuwa wameonyesha hayo maigizo.
   
 9. G

  Godsonmo New Member

  #9
  Nov 30, 2011
  Joined: Sep 29, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Habari BBC zinasema kutokana na makosa yaliyofanyika wakati wa ununuzi wa Rada ya Tanzania kampun iliyouza rada hiyo haikuweka kumbukumbu zozote za kimaandishi kwa ajili ya mauzo hayo hivyo imeamuriwa kurudisha kwa serikali ya tz kiasi cha dolla million 46 na pia bunge la uingereza limesema liko tayari kuisaidia mahakama ya tz kuwafikisha wale waliohusika na utapeli akiwemo yule jamaa wa vijisent je serikali ya ccm itathubutu kuwapeleka mahakaman au wapelekwe ICC ?
   
 10. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  ICC inahusika vipi na makosa ya kibiashara?
   
 11. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Junior member.... junior mind

  Godsonmo
  [​IMG] Junior Member
   
 12. M

  Malova JF-Expert Member

  #12
  Nov 30, 2011
  Joined: Apr 21, 2011
  Messages: 777
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Uingereza inawezakuwa na nia thabiti lakini mambo yatapindishwa hapahapa bongoni kwetu
   
 13. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #13
  Nov 30, 2011
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Lakini sheria za Bongo mwizi akisharudisha pesa aliyoiba, basi kesi si kwisa kazi yake? Au mmesahau ile ya EPA?
   
 14. WA-UKENYENGE

  WA-UKENYENGE JF-Expert Member

  #14
  Nov 30, 2011
  Joined: Oct 1, 2011
  Messages: 2,904
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hapo Uingereza wanatafuta namna ya kutuhadaa ili waweke mtu wao 2015 aingie magogoni kuendelea kutuvuna. Walishaona karata hazichezeki inabidi ramani ichorwe vizuri ili mambo yaende kama wanavyotaka. Subiri mtaona.
   
 15. M

  Msanya Member

  #15
  Nov 30, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 86
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  True. Mtoto wa shule akipewa mimba na mhusika akasidia kuitoa, basi kesi kwisha!
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Imeandikwa na LONDON, Uingereza; Tarehe: 30th November 2011 @ 14:30

  WABUNGE wa Uingereza, wameitaka Serikali ya Tanzania kumfungulia mashitaka mtu yeyote aliyehusika katika kashfa ya ufisadi wakati wa mauzo ya rada yaliyofanywa na kampuni ya vifaa vya ulinzi ya BAE Systems ya Uingereza.

  Kampuni ya BAE Systems tayari imekubali kulipa takribani pauni milioni 30 kama fidia kwa Tanzania kwa kukosa kuweka kumbukumbu zake za hesabu kuhusu mauzo hayo yenye utata.

  Kamati ya Maendeleo ya Kimataifa ya Bunge la Uingereza pia wametaka watuhumiwa wote wa
  Tanzania waliohusika na sakata hilo wachukuliwe hatua za kisheria haraka.

  Kamati hiyo pia imeishutumu kampuni hiyo kwa kuchukua muda mrefu kurejesha kiasi cha fedha ilichozidisha katika mauzo ya rada hiyo.

  Wakati Wabunge wa Uingereza wakisisitiza watuhumiwa wa Kitanzania washitakiwe, Serikali ya Tanzania imekuwa ikidai haina ushahidi wa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa ufisadi wa Rada.

  Waziri katika Ofisi ya Rais anayehusika na Utawala Bora, Mathias Chikawe aliwahi kutoa msimamo huo wa Serikali bungeni na kutaka wale wote wenye ushahidi waupeleke ili Serikali ichukue hatua.

  Jana waziri huyo alipopigiwa simu na kuulizwa suala hilo alisema yuko kwenye kikao na kuomba apigiwe baada ya nusu saa.

  Alipopigiwa baada ya muda huo simu yake iliita bila majibu. Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hoseah naye hakupatikana kuzungumzia suala hilo kuhusu msimamo huo wa wabunge wa Uingereza.

  Kiasi kikubwa cha fedha kilichotozwa na kampuni ya BAE System ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania rada ya kijeshi kilichochea kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo.

  Mwaka jana, baada ya BAE kukiri kushindwa kutunza kumbukumbu zake kuhusu mauzo hayo, kampuni hiyo ilikubali kulipa kiasi cha dola milioni 46 kwa Tanzania kama fidia ya mauzo kutokana na ulaghai uliofanyika.

  Fedha hizo zilikubalika zitumike kununulia vitabu vya shule na vifaa vingine. Lakini Bunge la Uingereza limesikitishwa kuwa fedha hizo bado hazijalipwa kwa Serikali ya Tanzania.


   
 17. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #17
  Dec 1, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Ina Maana Uncle Fisadi Chenge? CC na NEC wameshindwa...
   
 18. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #18
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  [h=1]Wahusika wa kashfa ya BAE TZ kushtakiwa[/h]
  Imebadilishwa: 30 Novemba, 2011 - Saa 03:05 GMT

  [​IMG]Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza


  Kundi la wabunge kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini Uingereza limetoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi ya mtu yeyote aliyehusika katika kashfa ya ufisadi na rushwa kuhusiana na mauzo ya rada yaliyofanywa na kampuni ya vifaa vya ulinzi ya BAE Systems ya Uingereza.
  Kampuni ya BAE Systems tayari imekubali kulipa takriban dola millioni 46 kama fidia kwa Tanzania kwa kukosa kuweka kumbukumbu zake za mahesabu kuhusiana na mauzo hayo yenye utata.


  Lakini kamati ya maendeleo ya kimataifa ya bunge la Uingereza imeishutumu kampuni hiyo kwa kuchukua muda mrefu kurejesha kiasi cha fedha ilichozidisha katika mauzo ya rada hiyo.
  Kiasi kikubwa cha fedha kilichotozwa na kampuni ya BAE system ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania rada ya kijeshi kilichochea kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo.
  [h=2]uchunguzi[/h]Uchunguzi huo ulifanywa na Shirika la Kupambana na Ufisadi la Uingereza, Serious Fraud Office.
  Mwaka jana, baada ya BAE kukiri kushindwa kutunza kumbukumbu zake kuhusu mauzo hayo, kampuni hiyo ilikubali kulipa kiasi cha dola milioni 46 kwa Tanzania kama fidia ya mauzo kutokana na ulaghai uliofanyika.
  Fedha hizo zilikubalika zitumike kununulia vitabu vya shule na vifaa vingine.
  Lakini bunge la Uingereza limesikitishwa kuwa fedha hizo bado hazijalipwa.
  BAE systems inasema kwa sasa inawasiliana na shirika la misaada la kimataifa la Uingereza kuona namna fedha hizo zitakavyotumika.
  Japokuwa BAE systems haikupatikana na hatia ya rushwa, lakini watu binafsi waliohusika na kashfa hiyo wanaweza kushitakiwa.
  Wabunge wa Uingereza wamesema wako tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mahakama zake kuendesha mashtaka dhidi ya watu wanaohusika na ulaghai huo.  SOURCE: BBC SWAHILI
   
 19. OSOKONI

  OSOKONI JF-Expert Member

  #19
  Dec 1, 2011
  Joined: Oct 20, 2011
  Messages: 10,809
  Likes Received: 3,893
  Trophy Points: 280
  [h=1]Wahusika wa kashfa ya BAE TZ kushtakiwa[/h]
  [​IMG]Kampuni ya BAE Systems ya Uingereza


  Kundi la wabunge kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini Uingereza limetoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi ya mtu yeyote aliyehusika katika kashfa ya ufisadi na rushwa kuhusiana na mauzo ya rada yaliyofanywa na kampuni ya vifaa vya ulinzi ya BAE Systems ya Uingereza.
  Kampuni ya BAE Systems tayari imekubali kulipa takriban dola millioni 46 kama fidia kwa Tanzania kwa kukosa kuweka kumbukumbu zake za mahesabu kuhusiana na mauzo hayo yenye utata.


  Lakini kamati ya maendeleo ya kimataifa ya bunge la Uingereza imeishutumu kampuni hiyo kwa kuchukua muda mrefu kurejesha kiasi cha fedha ilichozidisha katika mauzo ya rada hiyo.
  Kiasi kikubwa cha fedha kilichotozwa na kampuni ya BAE system ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania rada ya kijeshi kilichochea kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo.
  [h=2]uchunguzi[/h]Uchunguzi huo ulifanywa na Shirika la Kupambana na Ufisadi la Uingereza, Serious Fraud Office.
  Mwaka jana, baada ya BAE kukiri kushindwa kutunza kumbukumbu zake kuhusu mauzo hayo, kampuni hiyo ilikubali kulipa kiasi cha dola milioni 46 kwa Tanzania kama fidia ya mauzo kutokana na ulaghai uliofanyika.
  Fedha hizo zilikubalika zitumike kununulia vitabu vya shule na vifaa vingine.
  Lakini bunge la Uingereza limesikitishwa kuwa fedha hizo bado hazijalipwa.
  BAE systems inasema kwa sasa inawasiliana na shirika la misaada la kimataifa la Uingereza kuona namna fedha hizo zitakavyotumika.
  Japokuwa BAE systems haikupatikana na hatia ya rushwa, lakini watu binafsi waliohusika na kashfa hiyo wanaweza kushitakiwa.
  Wabunge wa Uingereza wamesema wako tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mahakama zake kuendesha mashtaka dhidi ya watu wanaohusika na ulaghai huo.

  SOURCE: BBC-SWAHILI
   
 20. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #20
  Dec 1, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"][/TD]
  [TD="class: buttonheading, align: right"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Wednesday, 30 November 2011 21:26[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD][​IMG]Boniface Meena
  SAKATA la ununuzi wa rada kutoka kampuni ya BAE ya Uingereza limerudi kwa sura mpya baada ya Bunge la nchi hiyo kuitaka Serikali ya Tanzania iwafikishe mahakamani watu wote walioshiriki mchakato wa ununuzi wake na kuingiza nchi katika hasara ya mabilioni ya fedha.

  Kupitia kamati yake ya Maendeleo ya Kimataifa, Bunge hilo limesema lingependa kuona watu wote walioshiriki kwenye mchakato wa ununuzi wa rada hiyo, wakifikishwa mahakamani kujibu tuhuma za ufisadi.

  Taarifa ya kamati hiyo iliyonukuliwa jana na Shirika la Habari la Uingereza (BBC), ilieleza kuwa wajumbe wake ambao ni wabunge kutoka vyama mbalimbali, watatoa ushirikiano wa dhati kwa Tanzania iwapo itaamua kuwashtaki watuhumiwa hao nchini Tanzania au Uingereza.

  Wabunge hao walisema kuwa mbali na kurudishiwa fedha iliyozidi kwenye ununuzi huo, Tanzania inapaswa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wote ili haki itendeke.

  Wito huo wa wabunge wa Uingereza umekuja wakati tayari Kampuni ya BAE System, iliyoiuzia Tanzania rada hiyo, ikikubali kuwa kulikuwa na kasoro katika mchakato wa ununuzi wa rada hiyo na hivyo kuirudishia Tanzania Dola za Marekani 46 milioni kama fidia.

  Hoseah adai mkanganyiko
  Alipotakiwa kuzungumzia suala hilo jana, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah alisema; "Kama Bunge la Uingereza linasema wafikishwe mahakamani na hukumu ilitolewa huko huko Uingereza, hapa kuna mkanganyiko."

  Aliongeza: "Niko Tanga, sijapata taarifa, lakini ni vizuri ukasoma hukumu iliyotolewa Uingereza, ina ushahidi mwingi halafu tujadiliane kwenye hilo."

  DPP: Tupeni ushahidi
  Akizungumza na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen, Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP), Eliezer Feleshi alisema, "Kama Uingereza wana ushahidi, tuko tayari kwenda mahakamani hata kesho kwa sababu ofisi yangu inahitaji ushahidi ili iweze kupeleka kesi mahakamani."

  Wito huo wa wabunge wa Uingereza umekuja miezi kadhaa tangu Serikali ya Tanzania itume wabunge wanne, wakiongozwa na Naibu Spika, Job Ndugai kwenda Uingereza kufuatilia suala la malipo ya fedha iliyozidi kwenye manunuzi hayo ya rada.

  Wabunge wa Tanzania

  Wabunge wengine walioambatana na Ndugai katika msafara huo ni Mussa Azzan, Angella Kairuki na John Cheyo.
  Katika Mkutano wa Nne cha Bunge la Kumi, timu ya wabunge hao walioenda nchini Uingereza kufuatilia malipo ya rada kwa Serikali ya Tanzania ilikabidhi ripoti yake kwa Spika wa Bunge iliyopendekeza mambo mawili, ikiwamo kushtakiwa kwa wahusika wa sakata hilo hapa nchini.

  Kwa nyakati tofauti, wabunge hao waliwaeleza waandishi wa habari kuwa waligundua madhambi ya kutisha katika sakata la ununuzi wa rada hiyo ya kijeshi yanayoweza kuwatia hatiani wahusika.

  Ingawa wajumbe hao hawakuwataja watuhumiwa hao kwenye mkutano huo na waandishi wa habari, aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Andrew Chenge, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Bariadi Magharibi (CCM), ni mtuhumiwa namba moja.

  Wakati wa uchunguzi wa sakata hilo, Kampuni ya SFO ya Uingereza, ilibaini kuwa zaidi ya Dola za Marekani 1.2milioni kwenye akaunti ya Chenge iliyoko katika kisiwa cha Jersey nchini Uingereza.

  Lakini, alipohojiwa na waandishi wa habari, Chenge alisema, "hivi ni vijisenti tu."[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  chanzo: Uingereza yawataka kortini waliohusika kashfa ya rada
   
Loading...