Hatimaye wabunge wa Uingereza waungana kuhimiza wahusika kashfa ya rada kuwajibishwa

Hivi Uingereza ikisema itasimamisha misaada mpaka Tanzania itakapowafikisha watuhumiwa mahakamani, bado tutaleta nyodo kama zile kuukataa ushoga? Kwamba misaada yenu huko huko, lakini hafikishwi mtu mahakamani? Kwamba Uingereza kutulazimisha kuwafikishwa watuhumiwa mahakamani ni kinyume na utamaduni wetu?

Hoseah anasema "Kama Bunge la Uingereza linasema wafikishwe mahakamani na hukumu ilitolewa huko huko Uingereza, hapa kuna mkanganyiko." Lakini wakifikishwa mahakamani hapa na hukumu kutolewa hapa hapa kuna mkanganyiko? Kama Uingereza ikiamua kuwashtaki hao watuhumiwa kwenye mahakama zao, Tanzania iko radhi kuwa-extradite?
 
Commenting on today's report, Chandu Krishnan, Executive Director of Transparency International UK said: "This report should be welcomed by all those who are concerned about bribes paid overseas by British companies. Bribery is not a victimless crime and it is important that reparations are also made to the countries whose citizens suffer when bribes are paid.

"The long saga of allegations about corruption involving BAE Systems has been a national embarrassment to both the UK and Tanzania, and it is astonishing that no individual has yet been found guilty despite the company having to pay fines and reparations of $450 million for Tanzania and other cases. We are pleased to hear that the Tanzanian government may prosecute individuals, and hope that the UK authorities will cooperate fully if UK nationals are found to have broken Tanzanian law. We particularly endorse the suggestion that the Government's Anti-Corruption Champion should publish annual reports on his work."
 
WanaJF,Sakata la Rada limeibuka tena upya na wakati huu baadhi ya Wabunge wa Uingereza kuonesha uchungu na nchi yetu kuliko hata viongozi wetu! Kabla ya hapo pengine mnakumbuka jinsi Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza Claire Short alivyopinga suala la Tanzania kununua Rada hiyo ambapo alidai kuwa kulikuwa na mazingira ya rushwa. Mama huyo aliwahi kufunga safari kuja Tanzania lakini Rais Mkapa aliamua kula na mafisadi hadi Rada iliponunuliwa.Baada ya hapo tumeshuhudia mazingaombwe yaliyofuata.Sasa hivi Wabunge wa Uingereza wameendelea kuondesha kuwa na uchungu na "wafiwa" kuliko uchungu unaooneshwa na "wafiwa wenyewe!"Fuatilia habari hii hapa chini:

Sakata la rada laibuka upya •

Wabunge wataka wahusika washitakiwe na Shabani Matutu

SAKATA la tuhuma ya ufisadi wa mauzoya rada kutoka Kampuni ya BAE Systems limeibuka upya na sasa kundi la wabunge wa vyama vya siasa nchiniUingereza limesema liko tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwashitaki watu wote waliohusika na kashfa hiyo. Vyombo kadhaa vya habari vya kimataifa vimewakariri wabunge hao wakisema kuwa pamoja na kwamba BAE Systems iliyoliuzia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) rada hiyo kwa bei ya kutisha haikupatikana na hatia ya rushwa, lakini watu binafsiwaliohusika na kashfa hiyo wanaweza kushitakiwa kwa kosa hilo. Wabunge hao pamoja na kutaka wahusika kushitakiwa, wameonesha kusikitishwa kwao na ucheleweshwaji wa malipo hayo unaofanywa na kampuni hiyo tangu kumalizika kwa uchunguzi uliofanywa na Shirika la Kupambana na Ufisadi la Uingereza la ‘Serious Fraud Office' na kugundua kutumika kiasi kikubwa cha fedha kinyume cha bei halali. Kampuni ya BAE Systems imekubali kuilipa Serikali ya Tanzania dola milioni 46 (zaidi ya sh bilioni 75), kama fidia ya kukosa kuweka kumbukumbu zake za mahesabu kuhusiana na mauzo hayo yenye utata. Kampuni hiyo imedai hivi karibuni kuwa imewasiliana na shirika la misaada la kimataifa la Uingereza kuona namna fedha hizo zitakavyotumika, kauli ambayo imepingwa vikali na wabunge hao. Wabunge hao wamedai kuwa tayari Serikali ya Uingereza ilikwisha kutoa mwongozo ikitaka fedha hizo zitumikekununulia vitabu vya shule na vifaa vingine vya maendeleo. Miezi kadhaa iliyopita, urejeshaji wa fedha hizo ulizua tafrani kubwa baina ya serikali ya Tanzania na ile ya Uingereza, baada ya taifa hilo kubwa duniani kukataa kurejesha fedha hizo kupitia hazina kwa kile walichodai kuhofia kutumika vibaya. Hatua hiyo iliichefua Serikali ya Tanzania ambayo ililazimika kujibu kwa ukali, ikitaka Uingereza kulipa fedha hizo bila masharti yoyote. Hata hivyo, habari zinadai kuwa hadi sasa fedha hizo hazijalipwa, hatua iliyowasukuma kundi la wabunge wa nchi hiyo kuamua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wahusika. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, hakuweza kupatikana kwa njia ya simu, baada ya kuelezwa kuwa alikuwa nje ya nchi kikazi. Membe ndiye waziri aliyesimama kidete kupinga uamuzi wa kurejeshewa fedha hizo kwa masharti. Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Mathias Chikawe, alipoulizwa juu ya msimamo wa Tanzania ikiwa watakubaliana na pendekezo la wabunge hao wa Uingereza, alikataa kusema chochote akidai kuwa hawezi kuwasiliana na magazeti kwa njia ya simu. Hata hivyo Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, Job Ndugai, ambaye aliongoza ujumbe wa wabunge kwenda Uingereza kufuatiliafedha hizo, alieleza kusikitishwa kwake na ucheleweshaji wa malipo ya fedha hizo. Ndugai alisema madai yanayotolewa na kampuni hiyo kwamba hawawezi kuzitoa kwa serikali kwa hofu ya kutumika vibaya ni ya kuzusha kwa sababu kwa miaka mingi, Uingereza imekuwa ikitoa fedha za misaada ambazo zimetumika kikamilifu na hakuna malalamiko. Aliongeza kuwa Tanzania itazidi kuzidai fedha hizo, pamoja na riba, kwa kuwa zimechelewesha mambo mengi ya msingi. Ununuzi wa rada hiyo uliofanyika mwishoni mwa miaka ya 1990 ulilalamikiwa na kupingwa vikali na wabunge kadhaa wa Uingereza kiasi cha kumlazimisha aliyekuwa Waziri wa Uingereza wa Masuala ya Afrika, Clear Shot, kujiuzulu. Shot alidai kuwa kitendo cha serikali yake kufumbia macho wizi huo mkubwa kilikuwa ni fedheha, kwa nchiyake na hakuwa tayari kuwa miongonimwa viongozi waliokubaliana na sualahilo. Sakata hilo kwa hapa nchini lilileta tafrani kubwa baada ya waliokuwa wakisimamia ununuzi huo, akiwamo aliyepata kuwa Mwanasheria Mkuu waSerikali kwa miaka hiyo, Andrew Chenge, kutuhumiwa kuhusika na ununuzi huo. Hata hivyo, Chenge amekuwa akikanusha tuhuma hizo, licha ya sakata hilo kuingia bungeni na ripoti kadhaa za uchunguzi kuonesha kuwa alinufaika na manunuzi ya rada hiyo."
Source: Tanzania Daima.
 
Tatizo wafiwa walishiriki kumuua marehemu kwa manufaa yao wenyewe, watakuwaje na huzuni?
 
Si washasema hawana hatia na vyombo vyetu vya kupalilia rushwa vikasema bnavyo kuwa hawana hatia sasa hapo utamshtaki nani
Na ushahidi upi
Wafiwa hawana haja tena ya kuhangaika maana wahakula mpaka pesa za sanda
 
Kundi la wabunge kutoka vyama mbali mbali vya siasa nchini Uingereza limetoa wito wa kufunguliwa mashtaka dhidi ya mtu yeyote aliyehusika katika kashfa ya ufisadi na rushwa kuhusiana na mauzo ya rada yaliyofanywa na kampuni ya vifaa vya ulinzi ya BAE Systems ya Uingereza.

Kampuni ya BAE Systems tayari imekubali kulipa takriban dola millioni 46 kama fidia kwa Tanzania kwa kukosa kuweka kumbukumbu zake za mahesabu kuhusiana na mauzo hayo yenye utata.

Lakini kamati ya maendeleo ya kimataifa ya bunge la Uingereza imeishutumu kampuni hiyo kwa kuchukua muda mrefu kurejesha kiasi cha fedha ilichozidisha katika mauzo ya rada hiyo.

Kiasi kikubwa cha fedha kilichotozwa na kampuni ya BAE system ya Uingereza iliyoiuzia Tanzania rada ya kijeshi kilichochea kufanyika kwa uchunguzi dhidi ya kampuni hiyo.

Uchunguzi huo ulifanywa na Shirika la Kupambana na Ufisadi la Uingereza, Serious Fraud Office.

Mwaka jana, baada ya BAE kukiri kushindwa kutunza kumbukumbu zake kuhusu mauzo hayo, kampuni hiyo ilikubali kulipa kiasi cha dola milioni 46 kwa Tanzania kama fidia ya mauzo kutokana na ulaghai uliofanyika.

Fedha hizo zilikubalika zitumike kununulia vitabu vya shule na vifaa vingine.

Lakini bunge la Uingereza limesikitishwa kuwa fedha hizo bado hazijalipwa.

BAE systems inasema kwa sasa inawasiliana na shirika la misaada la kimataifa la Uingereza kuona namna fedha hizo zitakavyotumika.

Ijapokuwa BAE systems haikupatikana na hatia ya rushwa, lakini watu binafsi waliohusika na kashfa hiyo wanaweza kushitakiwa.

Wabunge wa Uingereza wamesema wako tayari kushirikiana na serikali ya Tanzania katika mahakama zake kuendesha mashitaka dhidi ya watu wanaohusika na ulaghai huo.
 
Back
Top Bottom