Hatimaye vyuma Vyalegea

Mzunguko wa fedha umeongezeka sana awamu hii kwa mafisadi!.
Kwa wanyonge haujawafikia bado.
 
Katika habari zote mlizoleta hapa CCM hii ndio ya kweli
Uchawi upo na wewe ni mchawi vilevile,wazabuni wanadai madeni ya ndani katika taasisi huyo bibi halipi,bajeti ina deficit katika maeneo kibao na madini hatujui yanapunguza lini mzigo wa mkopo tuliopewa na bibi muuza chai ya iriki.
 
Kwa hakika Rais Samia ni Zawadi kwetu watanzania tunayopaswa kuitunza kwa wivu mkubwa sana
 

Kuna vitu viwili vya kuzingatia;
1. Kuongeza au kupunguza mzunguko wa fedha sio kazi ya Rais. Ni kazi ya benki kuu ambayo haipaswi kuingiliwa na siasa.
2. Kuongezeka kwa kiwango cha fedha kwenye mzunguko sio taarifa nzuri kila wakati. Fedha nyingi kwenye mzunguko zinaweza kushusha thamani ya sarafu na kuondoa motisha ya kuzalisha mali kwa bidii.

Rais amefanya mengi mazuri ya kujivunia. Tuchagua namna sahihi ya kunadi mazuri yaliyofanywa.
 
Huo mzunguko wahi hizo 54 Trioni unawahusu watu wangapi among 65 miliontuliopo TZ? Utakuta circle ni ndogo sana so impact yake haiwezi kuonekana in a positive way, badala yake huwenda inasaidia kwenye kuongeza pengo kati ya walionacho na wasionacho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…