Salamu wakuu!
Mtakumbuka siku za hivi karibuni ndugu Mbatata alitoa yake ya moyoni, naomba ujisomee.
Mtoto wa rafiki yangu ni Mwandishi wa habari wa chombo kimoja maarufu hapa Nchini. Baba yake ni kiongozi katika moja ya Taasisi kubwa za umma ambazo hivi sasa zipo katika kipindi kigumu cha kuchunguzwa na hatimaye kufanyiwa marekebishio al maarufu "kutumbuliwa majipu'.

Rafiki yangu ananiambia kila akipigiwa simu na mtoto wake huyo (Mwandishi) huishiwa nguvu maanake anahofu ya kuambiwa "Baba leo tulikuwa Ikulu kumsikiliza Katibu Mkuu Kiongozi akitueleza maamuzi ya Rais"! Ingawa mtoto hajui, lakini baba mtu hubaki akikosa pumzi mpaka mtoto amalize salaam na kuaga ndipo apumue. Hili linanikumbusha hali ilivyokuwa Miaka ya huko nyuma.

Miaka ya 1990 nikiwa mwajiriwa wa serikali kama Karani katika wizara mojawapo yenye nguvu na kongwe, Serikali hii iliamua kuendesha zoezi la kupunguza watumishi, maarufu kama 'Redundancy'. Viongozi wakuu walikuwa wakijifungia kwenye vikao vya siri kujadili mwenendo wenyewe na wakitoka huko Mkuu wa Utawala anakuwa amebeba kabrasha lenye maamuzi yote.

Siku zilizofutata Mwangalizi wa Ofisi (au OS yaani - Office Supervisor) alikuwa akiitwa kwa Mkuu wa Ytawala na kupewa kazi ya kusambaza barua kwa watu waliokuwemo katika orodha ya hao walengwa kwa kuwafuata maofisini na kuwakabidhi barua zao. Ama kweli kilikuwa kipindi kigumu, na huyo Bwana OS ilipokuwa akiingia ofisi fulani hali hubadilika kabisa na furaha na vicheko vinavyoendelea hutoweka kama chumvi kwenye maji.

Na huyo OS (ni Marehemu sasa - Mungu amlaze pema huko aliko - sijui?) alikuwa akisha ona utulivu na woga umeshawapata watu, husema kwa sauti ya mamlaka: "E,Ndugu fulani yupo hapa?" Mtume! Macho yote hukodolewa kuelekea kwa mwenzetu mtajwa masikini na kushuhudia anavyosainishwa barua huku akititetemeka kwa simanzi.

Acheni bana, siku hizo ajira serikalini ilikuwa na "security" ya nguvu, uhakika wa maisha. Basi huyo Bw. OS akiondoka huku nyuma huacha watu wakimfariji mwenzao huku wakijiuliza sijui kesho zamu ya nani tena?

Bwana OS aliifanya kazi hii kwa bidii, kwa kujituma na kwa kujiamini kwa vile aliona "mteule mahsusi' hadi akajenga tabia ya kuona ufahari fulani akiingia mahali na kuona watu wanapomwona tu wanatamani kujificha chini ya meza!

Siku ya siku naambiwa Bw.OS alienda kukabidhi Despatch Book kwa Mkuu, na kutoa taarifa kwamba amemaliza kazi ya kuwakabidhi barua walengwa wote. Baada ya kufanya hivyo Mkuu akamwambia "OS, umefanya kazi nzuri, sasa na wewe saini hapa uchukue barua yako!'

Bwana Sefue unavyoongea na waandishi huku ukichekelea kusema hayo uliyoagizwa (huwa nakuona ukitabasamu),angalia yasikukute kama haya ya OS huyo - labda kama unastaafu kazi kwa umri kesho kutwa!