Hatimaye ufafanuzi wa kina umetolewa juu ya nyongeza ya mishahara

msuyaeric

JF-Expert Member
Dec 18, 2014
838
1,167
Ufafanuzi wa kina uliotolewa na Waziri Mkuu leo hii umeondoa propaganda za watu wachache waliolenga kupotosha jamii. Kama mtumishi wa umma napenda kuwakumbusha Watanzania mambo mazuri tuliyofanyiwa mpaka sasa na Rais Samia kama watumishi wa umma;

1. Nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma kulingana na madaraja huku kipaumbele kikiwa kwa wenye mishahara midogo.

2. Kupunguza kodi(PAYE) kwa kuifikisha 8% na kupandisha kiwango cha chini cha kukatwa kodi, suala hili lilipoteza kiwango cha takribani Bilioni 14 ya fedha zilizopaswa kukusanywa na serikali.

3. Katika mifuko ya hifadhi ya jamii kupandisha kiwanga cha malipo ya mkupuo kwa kufikia asilimia 33 kutoka 25% iliyokataliwa na wadau mwaka 2018.

4. Kupandishwa madaraja WATUMISHI laki moja tisini elfu na miatano sitini na mbili~ 190,562 (Kwa wasioelewa, hii imeigharimu Serikali kiasi cha takribani TZS BILIONI 39.6).

5. Taasisi zote zenye uhitaji wa wafanyakazi kupewa vibali vya ajira mpya na kutolewa vibali kwa watumishi walioomba kubadilisha vituo na kwenda kuongeza taaluma kwa mujibu wa taratibu na sheria za utumishi wa umma.

6. Kuanzia Mwezi March 2021 hadi January 2022, Rais Samia amewezesha ulipwaji wa madeni na malimbikizo ya watumishi wa umma wapatao 65,391, madeni yenye thamani ya takribani TZS BILIONI 90.7.

7. Kuondolewa kwa mzigo wa tozo ya 6%(VALUE RETENTION FEE) kwa watumishi waliokuwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Kiwango hiki cha 6% kimekuwa mzigo mzito kwa watumishi hususani vijana wanaotoka Vyuo Vikuu, Rais Samia atakumbukwa sana kwa hili.

8. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi ya watumishi. Hii inatupa hamasa watumishi kutoa huduma bora na kuhakikisha wananchi wanapewa wanachostahiri.

Itoshe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameweka rekodi ya aina yake kama Mkuu wa nchi anayejali watumishi wa umma. Tumuunge mkono azidi kuijenga Tanzania yetu.

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
 
Kweli kabisa japo sipo kwenye mifumo yenu hyo ya Ajira za Serikali
 
lakini kusema ukweli wamejitahidi sana na nawapngeza kwa kuongezea mshahara wale wa kima cha chini, walikua wanalipwa fedha kidogo sana acha wawainue walau imefika laki tatu take home
 
Ko hizo arrears zilipokoma kulipwa mwezi january 2022 kwa nini mpaka leo kimya kwa waliobaki kulipwa au bado ile kauli pendwa ya tunahakiki inaendelea kutamalaki?Nchi ngumu sana hii imejaa visingizio kwenye haki za watu
 
Yaani Nchi Nzima Wewe Tu Ndiyo Umemuelewa Kassimu
Acha Utani Wewe, Hakuna Ufafanuzi
 
Ufafanuzi wa kina uliotolewa na Waziri Mkuu leo hii umeondoa propaganda za watu wachache waliolenga kupotosha jamii. Kama mtumishi wa umma napenda kuwakumbusha Watanzania mambo mazuri tuliyofanyiwa mpaka sasa na Rais Samia kama watumishi wa umma;

1. Nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma kulingana na madaraja huku kipaumbele kikiwa kwa wenye mishahara midogo.

2. Kupunguza kodi(PAYE) kwa kuifikisha 8% na kupandisha kiwango cha chini cha kukatwa kodi, suala hili lilipoteza kiwango cha takribani Bilioni 14 ya fedha zilizopaswa kukusanywa na serikali.

3. Katika mifuko ya hifadhi ya jamii kupandisha kiwanga cha malipo ya mkupuo kwa kufikia asilimia 33 kutoka 25% iliyokataliwa na wadau mwaka 2018.

4. Kupandishwa madaraja WATUMISHI laki moja tisini elfu na miatano sitini na mbili~ 190,562 (Kwa wasioelewa, hii imeigharimu Serikali kiasi cha takribani TZS BILIONI 39.6).

5. Taasisi zote zenye uhitaji wa wafanyakazi kupewa vibali vya ajira mpya na kutolewa vibali kwa watumishi walioomba kubadilisha vituo na kwenda kuongeza taaluma kwa mujibu wa taratibu na sheria za utumishi wa umma.

6. Kuanzia Mwezi March 2021 hadi January 2022, Rais Samia amewezesha ulipwaji wa madeni na malimbikizo ya watumishi wa umma wapatao 65,391, madeni yenye thamani ya takribani TZS BILIONI 90.7.

7. Kuondolewa kwa mzigo wa tozo ya 6%(VALUE RETENTION FEE) kwa watumishi waliokuwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Kiwango hiki cha 6% kimekuwa mzigo mzito kwa watumishi hususani vijana wanaotoka Vyuo Vikuu, Rais Samia atakumbukwa sana kwa hili.

8. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi ya watumishi. Hii inatupa hamasa watumishi kutoa huduma bora na kuhakikisha wananchi wanapewa wanachostahiri.

Itoshe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameweka rekodi ya aina yake kama Mkuu wa nchi anayejali watumishi wa umma. Tumuunge mkono azidi kuijenga Tanzania yetu.

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
Upumbavu mtupu, aibu kubwa.Unawezaje kuahidi usichoweza kutekeleza? Hakuna hoja hapo endeleeni tu na sisi tutaendelea, Kuna siku mungu atasimama upande wetu
 
Hakika mama Samia ameupiga mwingi. Kafanya makubwa kwa kipindi kifupi Sana. Yule shetani ndiye kamwachia mama zigo zito, maana alivuruga mpangilio wa nyongeza za mishahara kwa kuisimamisha.
 
Ufafanuzi wa kina uliotolewa na Waziri Mkuu leo hii umeondoa propaganda za watu wachache waliolenga kupotosha jamii. Kama mtumishi wa umma napenda kuwakumbusha Watanzania mambo mazuri tuliyofanyiwa mpaka sasa na Rais Samia kama watumishi wa umma;

1. Nyongeza ya mshahara kwa asilimia 23.3 kwa watumishi wa umma kulingana na madaraja huku kipaumbele kikiwa kwa wenye mishahara midogo.

2. Kupunguza kodi(PAYE) kwa kuifikisha 8% na kupandisha kiwango cha chini cha kukatwa kodi, suala hili lilipoteza kiwango cha takribani Bilioni 14 ya fedha zilizopaswa kukusanywa na serikali.

3. Katika mifuko ya hifadhi ya jamii kupandisha kiwanga cha malipo ya mkupuo kwa kufikia asilimia 33 kutoka 25% iliyokataliwa na wadau mwaka 2018.

4. Kupandishwa madaraja WATUMISHI laki moja tisini elfu na miatano sitini na mbili~ 190,562 (Kwa wasioelewa, hii imeigharimu Serikali kiasi cha takribani TZS BILIONI 39.6).

5. Taasisi zote zenye uhitaji wa wafanyakazi kupewa vibali vya ajira mpya na kutolewa vibali kwa watumishi walioomba kubadilisha vituo na kwenda kuongeza taaluma kwa mujibu wa taratibu na sheria za utumishi wa umma.

6. Kuanzia Mwezi March 2021 hadi January 2022, Rais Samia amewezesha ulipwaji wa madeni na malimbikizo ya watumishi wa umma wapatao 65,391, madeni yenye thamani ya takribani TZS BILIONI 90.7.

7. Kuondolewa kwa mzigo wa tozo ya 6%(VALUE RETENTION FEE) kwa watumishi waliokuwa wanufaika wa mikopo ya Elimu ya juu (HESLB). Kiwango hiki cha 6% kimekuwa mzigo mzito kwa watumishi hususani vijana wanaotoka Vyuo Vikuu, Rais Samia atakumbukwa sana kwa hili.

8. Kuboreshwa kwa mazingira ya kazi ya watumishi. Hii inatupa hamasa watumishi kutoa huduma bora na kuhakikisha wananchi wanapewa wanachostahiri.

Itoshe kusema kwamba Rais Samia Suluhu Hassan ameweka rekodi ya aina yake kama Mkuu wa nchi anayejali watumishi wa umma. Tumuunge mkono azidi kuijenga Tanzania yetu.

Sent from my SM-A325F using JamiiForums mobile app
Tulia kwanza kabla ya kuandika.

Naona umeandika kwa haraka. Najiuliza kama ulimsikiliza Mhe. Majaliwa vizuri au ndo yeye kasema.hayo?
 
Alafu ukute na ww ni baba unayetegemewa kabisaa na familia...
💩💩💩💩
 
Back
Top Bottom