Hatimaye serikali yasalimu amri, itaonyesha live vikao vya bunge

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Baada ya kelele nyingi kutoka kila mahali na kila kona ya nchi, usiku huu tena kimya kimya imetangaza kurusha live majadiliano ya wabunge wakati wa vikao vya bunge.

Imetangazwa kwamba matangazo hayo yatarushwa kupitia TBC 2 kuanzia kesho.

Chanzo: TBC 1
 
Kama hii ni kweli basi bomba sana, hongera sana UKAWA kwa kusimama imara kupinga Bunge kufanywa kama UNYAGO (kutawaliwa na siri kubwa) na hongera Watanzania wote popote pale mlipo katika kupinga ubakwaji wa demokrasi nchini. Nadhani hili la Wabunge wa UKAWA kujirekodi wakiwa wanachangia mijadala mbali mbali ndani ya Bunge na kuhakikisha wanatuma mitandaoni limewapiga bao hao wabakaji demokrasi na wakawa hawana jinsi ya kulizuia si ajabu kupiga marufuku kuingia na simu Wabunge wengi wa chama cha majipu hawakuliafiki. Tusubiri kuthibitisha ukweli wa hii habari.
 
Kama hii habari ni ya kweli, huu bila shaka utakuwa ni uamuzi wa kikao cha Baraza la Mawaziri killichofanyika hapa Dodoma siku ya jana.Naamini hii ilikuwa ni moja ya agenda ya hicho kikao cha jana baada ya kugundua wamechemsha.

Sasa tujiulize kama kweli Serikali hailiindeshi Bunge kama linavyotaka.

Inawezekana pia Mbinu ya UKAWA ya kujirekodi na kurusha clip mitandaoni na matamko yaliyotolewa na Taasisi mbalimbali kupinga uamuzi huu umewaishitua hawa jamaa.

Hata hivyo,nawashauri UKAWA mbinu hiyo waiendeleze licha ya serikali kusalimu amri maana bado ina faida.
 
Upuuzi mtupu. Bunge limekuwa likionyeshwa live miaka vote na halikuweza kutatua kero za wananchi wala kupambana na ufisadi zaidi ya kuendelea kuwa sehemu ya michezo ya kuigiza tu miaka nenda rudi na Shida ziko palepale.

Nashukuru magufuli katuonyesha tofauti ya kuwa hata kama bunge liko live au la yeye kkwake hapa ni kazi tu...ametatua kero za watu bila bunge kuwa live.
 
Kama hii ni kweli basi bomba sana, hongera sana UKAWA kwa kusimama imara kupinga Bunge kufanywa kama UNYAGO (kutawaliwa na siri kubwa) na hongera Watanzania wote popote pale mlipo katika kupinga ubakwaji wa demokrasi nchini. Nadhani hili la Wabunge wa UKAWA kujirekodi wakiwa wanachangia mijadala mbali mbali ndani ya Bunge na kuhakikisha wanatuma mitandaoni limewapiga bao hao wabakaji demokrasi na wakawa hawana jinsi ya kulizuia si ajabu kupiga marufuku kuingia na simu Wabunge wengi wa chama cha majipu hawakuliafiki. Tusubiri kuthibitisha ukweli wa hii habari.
Hivi walikuwa na mpango wa kupiga marufuku wabunge wasiingie Bungeni na simu?!!!!
 
Upuuzi mtupu. Bunge limekuwa likionyeshwa live miaka vote na halikuweza kutatua kero za wananchi wala kupambana na ufisadi zaidi ya kuendelea kuwa sehemu ya michezo ya kuigiza tu miaka nenda rudi na Shida ziko palepale.

Nashukuru magufuli katuonyesha tofauti ya kuwa hata kama bunge liko live au la yeye kkwake hapa ni kazi tu...ametatua kero za watu bila bunge kuwa live.
Unadhani kwanini bunge lilishindwa kutatua kero za wananchi? Bunge linatumia demokrasia ya ndiyo au hapana. Hii ndio culprit ya bunge kushindwa kufanya kazi.
 
Hapana Mkuu ila niliona mahali watu wakijadili maamuzi ya Wabunge wa UKAWA kujirekodi wanapochangia kwenye mijadala mbali mbali na kisha kuzituma hizo recordings zao katika mitandao mbali mbali nchini, mmoja wa wachangiaji katika mjadala huo akaandika kwamba hatashangaa kama chama cha majipu pamoja na Serikali kupiga marufuku Wabunge kuingia na simu bungeni na kuanza kupekuliwa na atakayekiuka amri hiyo basi anaweza kufukuzwa bungeni kwa wiki au hata zaidi.

Hivi walikuwa na mpango wa kupiga marufuku wabunge wasiingie Bungeni na simu?!!!!
 
Baada ya kelele nyingi kutoka kila mahali na kila kona ya nchi, usiku huu tena kimya kimya imetangaza kurusha live majadiliano ya wabunge wakati wa vikao vya bunge.

Imetangazwa kwamba matangazo hayo yatarushwa kupitia TBC 2 kuanzia kesho.

Chanzo: TBC 1
Kumbe inawezekana tukipambana!?sasa kilicho baki ni kwenda kudai katiba mpya!
 
kwa hili la kukataza wananchi kuwafuatilia wabunge wao nini wanakifanya huko dodoma serikali yetu tukufu chini ya mh. magu ilichemsha. kama serikali imeamua kurusha live ni jambo jema, unapokosea ni vema kujirekebisha. wasirushe Kwa TBC2 tu tunataka TBC warushe live maana ndo TV inayopatikana maeneo yote nchi nzima.pia waaruhusu TV binafsi kurusha pia bunge hilo LIVE.
 
Back
Top Bottom