Hatimaye serikali yakosa pesa za kulipa mishahara ya wafanyakazi muhimbili-mnh | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hatimaye serikali yakosa pesa za kulipa mishahara ya wafanyakazi muhimbili-mnh

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lu-ma-ga, Mar 2, 2011.

 1. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Kuna taarifa za uhakika kwa 100% kuwa serikali imeshindwa kukidhi kulipa madai ya malimbikizo ya mishahara ya wafanyakazi katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.Malimbikizo hayo yametokana na nyongeza ya mishahara iliyotangazwa mwaka jana na serikali( salary in arrears) kwa kipindi cha july to February.
  Jana kaimu Mkurugenzi mkuu wa hospitali pamoja na viongozi wa chama cha wafanyakazi MNH waliongozana kwenda wizarani kujua kulikoni pesa za malimbikizo ziwasilishwe kidogo.
  Sasa tunaanza kuamini kuwa serikali imefilisika kama inashindwa kulipa hata mishahara ya wafanyakazi( preferential obligations).
   
 2. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Ila za kulipa DOWANS zipo....
   
 3. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  sio MNH tu...ni idara zote za seikali mpaka sasa bila bila,kasoro wanajeshi tu
   
 4. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kweli account nyingi za wafanyakazi wa idara mbalimbali ziko empty mpaka tunavyoongea.
   
 5. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2011
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Hata mimi ni mfanyakazi wa serekali, sijapewa mshahara
   
 6. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Thread yako inakinzana yenyewe, na kuonyesha haiko makini, soma kwenye red. Hapo yaonyesha wameshindwa kulipa malimbikizo ya nyongeza na si mshahara, kama mtu alikuwa analipwa Tshs 6 na akaongezwa ikafika Tshs 10, hapo inaonyesha nyongeza ya Tshs 4 ndio haijalipwa ila Tshs 6 inalipwa kama kawaida, hapo ndipo nasema maelezo yako hayako makini
   
 7. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  mishahara mingi haijatoka babu wewe acha ubishi
   
 8. I

  Idofi JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 1,542
  Likes Received: 820
  Trophy Points: 280
  maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana "JK"
   
 9. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Unapoongelea malimbikizo ya mishahara maana yake ni mishahara, umesoma shule gani rafiki, pia kumbuka yalipashwa kulipwa wakati muafaka lakini ikashindikana kutokana na ukata.kinachoongelewa hapo ni mishahara.period
   
 10. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #10
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Wewe ndio hujaelewa sasa na yaonekana si mfuatiliaji wa mambo, hakuna taasisi ya serikali na hasa muhimbili kutolipwa mshahara tangu July 10 - Feb 11, linaloongelewa hapa ni nyongeza (kuwa muelewa nini maana ya nyongeza ). Sasa unaposema nyongeza , huwezi sema wameshindwa kulipa mishahara. Na elewa nyongeza ilikuwa ni kiasi kidogo hakizidi 10%, kwa hiyo 90% zimelipwa, hapo utasemaje mishahara imeshindwa kulipwa? acha kuwa mchicha mwiba wewe
   
 11. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Watu tumeisha lipwa na tumeisha umaliza mshahara wenyewe
   
 12. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #12
  Mar 2, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,319
  Likes Received: 439
  Trophy Points: 180
  na wewe si umo katika wale?
   
 13. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #13
  Mar 2, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hutaki kuaamini?? Wenzio walio serikalini wanakwambia hawajalipwa sasa ubishi wa nini mkuu?? Kama una uhakika kuwa mishahara imelipwa basi tuambie. Nakubaliana nawe mtoa mada wa kwanza kaweka utata kidogo kwa kusema nyongeza.
   
 14. Lu-ma-ga

  Lu-ma-ga JF-Expert Member

  #14
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 2,848
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  psychiatric case wewe
   
 15. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #15
  Mar 2, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Serikali haiwezi kukosa pesa ya mishahara kwani kila siku TRA wanakusanya; kama ni kweli jambo hili linaweza kuwa limechangiwa na mikopo iliyotolewa kwa Wabunge maana TShs. 90,000,000 X wabunge 350 = 31.5 billion zimetoka February 2011. Tuwe na subira kodi za mishahara ya February 2011 toka secta binafsi zitalipwa kabla ya tarehe 7/3/2011 na pesa ya mishahara yetu itapatikana tuu. Tuendeleze uhusiano mzuri na wenye maduka, wauza maziwa nk. ili wasisitishe bill
   
 16. PrN-kazi

  PrN-kazi JF-Expert Member

  #16
  Mar 2, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 2,890
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Msimu huu ni kimbembe kwa wafanyakazi: JK alikataa kura zetu, sisi tukajipendekeza kumpa sasa tutakoma.
   
 17. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #17
  Mar 2, 2011
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Huyo mtu anayejiita Think Twice ni aidha hana akili timamu au ametumwa na chama kuvuruga jamvi. Kwasababu kila mara anaandika opposite na wengine. Ni sawa na beattle anayeviringisha mavi kinyume nyume.

  Serikali iliongoza mishahara ya wafanyakazi tangia July 2010. Kwa wafanyakazi wengi tuliendelea kulipwa mishahara ya zamani hadi November 2010 ndipo tulipoanza kupokea mishahara mipya. Hivyo basi tunadai malimbikizo ya mishahara ya miezi 4 i.e. from July-October (Malimbilkizo hayo ni mshahara mpya July - Mshahara wa zamani).

  Baada ya chama chetu cha wafanyakazi TUGHE kukaa na menejimenti ya utumishi wa umma na Hazina mwezi Dec/Jan(?) walikubaliana kwamba Serikali italipa malimbikizo mishahara mwezi February. Sasa serikali imeshindwa kutumiza ahadi yake. Kumbuka nyongeza hii ya mishahara iko kwenye budget ya 2010/11. Lakini pesa ya kulipa DOWNS ambayo haiko kwenye budget ipo.

  Sasa je wafanyakazi tukigoma JK kweli atasingizia CDM?!. Maana tumepitia taratibu zote kama zilivyoaanishwa kwenye sheria za kazi na majadiliano.

  Mimi nafikiri serikali hii ya awamu ya nne imeshindwa kazi. TUGHE itisheni mgomo wa nchi nzima maana hii serikali ni punda na bila mturinga hatutalipwa sitahiki zetu.

  Kama ni watendaji wa serikali ndiyo wanamuangusha JK ili serikali yake ichukiwe na wananchi kwanini basi hawachukulii hatua za kinidhamu na kisheria?

  Ukweli ni kwamba JK is the weakest president this country had never have. Hata mzee Rukhusa alikuwa na ahueni.
   
 18. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #18
  Mar 2, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Wewe upo idara gani ya serikali? Maana sisi wa wizara ya elimu tumepewa barua kabisa kutujulisha kwamba mishahara itachelewa mwezi huu. Hadi hivi sasa, hatujaona mshahara. Wewe unayesema umeshamaliza, bila shaka ni uzao wa mafisadi. Au unafanya kazi Ikulu? Maana nyie kwa kupendeleana hamjambo, na hilo ndilo litakalowafanya msidumu hapo Ikulu hadi 2015. Maana matendo yenu yanatutia hasira sana.
   
 19. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #19
  Mar 2, 2011
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  duh yani apo uwa kana matatzo kuanzia kwa wakubwa wa hapo wana urasimu adi kwa wadogo kuna majungu.... mnazani solidarity itatoka wapi??? mimi nlikimbia hapo ndani ya siku mbili 2 tokea niwe appointed
   
 20. Makanyaga

  Makanyaga JF-Expert Member

  #20
  Mar 2, 2011
  Joined: Sep 28, 2007
  Messages: 2,503
  Likes Received: 133
  Trophy Points: 160
  Ahsante sana. Sikujua kama "shipilingitya" anaitwa hivyo kwa kiingeereza. Nadhani wewe ni daktari!
   
Loading...