Ni kwanini Serikali hailipi Malimbikizo ya mishahara ya Watumishi wake?

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
26,130
34,099
Habarini Wadau

Hakika kuna jambo linashangaza sana, serikali inapokea mikopo ya Mabilioni kila Mara na hata Trillion kadhaa na bado inakusanya kodi, LAKINI inashindwa kutenga bajeti ya billion chache kulipa Watumishi wake Madai yao ya mishahara iliyokaa kwa miaka kadhaa.

Mtu anadai malimbikizo na Arrears amejaza inakaa miaka mitatu mpaka mitano, wakati huohuo hatuna umeme, barabara zimesimama kwa sasa hazitengenezwi.

Sasa hii mikopo inafanya nini? Kama hata kwenye miradi ya muhimu haipo?

Serikali ilipe Watumishi malimbikizo yao ya mishahara.

Nawasilisha.
 
Inaudhi sana kwa kweli. Wengine wana madai ya miaka 7 na bado hawalipwi.
 
Back
Top Bottom