dubu
JF-Expert Member
- Oct 18, 2011
- 3,496
- 3,461
Asalaam aleyku,
Sasa ndo nmeanza kuelewa kwanini rais Magufuli anasema tumuombee. Nami naungana naye kusema tumuombee.
Hatimaye Serikali ya rais Magufuli Pumzi imekata, moja haikai mbili haikai. Wasaliti wote wamerudi CCM, sasa hatuna wa kumsingia, Jeshi la Polisi limewakamata wote wanaofanya uchochezi mtandaoni hadi wameisha hawana wa kumakamata. Lakini bado CCM imeshindwa kuishauri Serikali.
Sasa hivi kila Mtanzania kakaa pembeni anaangalia Jinsi Serikali ya Magufuli inavyopambana na Mabeberu. #HAPAKAZITU! imegeuka na kuwa hapa #JANJAJANJATU! mradi siku zisonge..
Na wale walio karibu na rais endeleeni hivyo hivyo, kila anachoongea mpigieni makofi na Vigelegele asijesema hamumuungi mkono mkatumbuliwa.
Kwasababu anaona mawazo yake ndo sahihi yaweza endesha nchi, tumuunge mkono amalize muda wake, ila msitegemee jipya zaidi ya hotuba zake kila siku kuongea Mabarabara, ndege, flyovers watumishi hewa vyeti hewa. Hotuba haibadiliki miaka mitatu sasa. Hii inamaanisha hakuna jipya.
Habari mpya kutoka kwake wananchi wanaoisubiria kuisikia ni kamtumbua nani, kamchagua nani na kamfokea nani.
Hakuna anayetegemea Magufuli aongelea ni jinsi gani au mpango mkakati gani alio nao wa kuondoa umasikini..
Kwa upande wangu naona analalamika kwamba nchi hii imeibiwa sana, nchi hii ni tajiri. Lakini hachukui hatua, wanaishia kukamatwa Wakina Kisena na Wanachama wa vyama vya Upinzani utafikiri ndo walikuwa madarakani kabla yake.
Kama tusipomuombea atukwamue hapa tulipo, sisi Wananchi ndio tutakao umia, sababu yeye, mke wake na Wanaye wanaendelea kula kodi zetu huku wakipiga mluzi sababu hawana cha kupoteza.
Ukiona Miradi mikubwa ya nchi, hapa namanisha ile miradi ambayo haizinduliwi na mwenge.. ukiona imeanza kusitishwa jua mbele giza kwa mkuu.
Sasa kupanga ni kuchagua. Tuendelee na Miradi mkose mishahara na madawa au tusitishe miradi muendelee kupata mishahara? Tumuombee rais wetu ili Mungu amfanyie wepesi kutuletea maendeleo
Mradi wa Stiegler's gorge hela iliyotengwa haitoshi, nasikia inatakiwa kuongezwa na mkuu hela hana sababu TRA hawasomeki.
SGR inaweza ikaishia Morogoro kama hali itaendelea kuwa hivi. (Kwa ufupi hela ya mradi wa SGR imekata)
Sasa hivi wakienda kuomba msaada wanaambiwa ngoja tuangalie Demokrasia nchini mwako ipoje.. Wakishaangalia wanasema tunapitia mkataba upya, nchi inaendesha bila kufuata misingi ya Demokrasia. Ndo maana tunahitaji kumubea Mungu amuepushe na Magumu anayopitia.
Wawekezaji wa kujenga Viwanda hamna wapya wanakuja sababu ya Sera mbovu ya uwekezaji na mabadiliko ya kodi yasiyotabirika
Hadi atakapotoa na kufuta kabisa akili mwake mawazo ya kuwaona wapinzani wake wa kisiasa au watu wasio CCM sio watanzania. CCM haiwezi kuiletea Maendeleo Tanzania, na Magufuli kuendelea kuwakumbatia CCM anakumbatia Umasikini.
Tanzania inatajengwa na Watanzania wote. Lakini bila kuwa na umoja hatuvuki hapa. Tunatakiwa tuwe kitu kimoja, hii ya kuwabagua baadhi ya Watanzania huwezi fika popote.
Rais Magufuli asione aibu, amuite Hashim Rungwe, Zitto Kabwe, Freeman Mbowe, Maalim Seif, Lipumba, Mbatia na wengine, wakae pamoja waangalie ni namna gani tutatoka hapa kama nchi.
Siasa ni maendeleo, bila siasa hakuna maendeleo. Na siasa ni wanasiasa. Lakini tusipoungana kama watanzania hata hizo ndege tutashindwa zipeleka gereji.
Nashukuru Mungu CCM wamemchoka na 2020 hawamrudishi Madarakani.. Atapata kura 32, Membe kura 2,080 halafu ndo wafuate hao wakina Januari.
Tumuombee amalize kipindi chake salama akapumzike Chato ale hela za kustaafu.
Wapinzani ukiwakataza kufanya siasa Majukwaani, wanaenda kufanyia Siasa kwenye chanzo chako cha fedha. Wapinzani ndo walipa kodi Wakubwa, sasa wamesusa kulipa na TRA inateteleka.
Bila kuwaaweka Watanzania Pamoja, kila siku itakuwa Mabeberu Mabeberu.

Kisutu: Robert Kisena afutiwa Mashtaka ya utakatishaji fedha na Mahakama. Yeye na Mkewe wakamatwa tena, wafunguliwa mashtaka mapya
Mahakama ya Kisutu imewafutia mashtaka Mkurugenzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (UDART), Robert Kisena na wenzake watatu waliokuwa wakikabiliwa na mashtaka 19 likiwemo la utakatishaji fedha Washtakiwa wengine kwenye kesi hiyo ni Kulwa Kisena (33), Charles Newe (47) na Cheni...
www.jamiiforums.com